Inaonekana wanasiasa hawajajua matatizo ya Walimu bado au Walimu hawajui matatizo yao.

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Nampongeza mbunge wa Mtwara mjini Maftaha Nachuma kwa kuwanunulia walimu mabasi mawili ya usafiri. Ni jambo zuri si baya. na anaonesha upendo. sijui niseme kwa kuwanunulia au kwa kuwaazima? maana bila shaka hayo mabasi yameandikwa majina yake kama mmiliki. lakini si hoja amewaazima wayatumie kwa usafiri.

Nimekuwa mara nyingi nikijiuliza matatizo ya walimu ni nini? na pengine kumekuwa na tatizo katika namna ya kuyakabili matatizo ya walimu. nadhani katika kada yenye wafanyakazi wengi sana serikalini Ualimu inaongoza ikifuatiwa na za jeshi au polisi. kama nimekosea mtanisahihisha. na kama si ualimu basi hazijaachana sana na kada hizo hapo juu.
najiuliza je walimu tatizo lao kubwa ni usafiri? niliona bwana makonda alipotangaza kuwa walimu wasafiri bure hapa dsm. na walimu walishangilia sana jambo hili. wakasahau shida zao za malimbikizo ya madai na mshahara usiotosheleza. wakasahau kuwa hawana marupurupu na kuwa wanafanya kazi ktk mazingira magumu. nao wakaimba chorus ya wimbo huo huku wakiruka ruka kwa furaha.

mbunge wa mtwara naye ameamua kuwasaidia kwa nia njema nampongeza. lakini hii misaada si endelevu kwa walimu. haiwasaidii.

walimu walipaswa wasaidiwe walipwe vizuri halafu nauli wajilipie tu kama kawaida. wakilipwa vizuri watavaa vizuri,wataishi vizuri, watapata pesa ya nauli n.k
walimu wana madeni mengi sana serikalini. walipwe pesa zao wafanye mambo ya maendeleo, wasaidiwe kupata mikopo ya kuwasaidia kiuchumi, waboreshewe mazingira yao ya kazi, usafiri watajilipia tu wenyewe wala sidhani kama ni issue kubwa sana
inaonekana viongozi wengi hawajui matatizo ya walimu, ama walimu wenyewe hawajui matatizo yao. sioni wakifanya jitihada za kuongea na wabunge kuwaelezea changamoto zao. kuwakusanya wabunge wote wa vyama vyote na kuwaambia nini matatizo yao. kufanya jitihada za kuonana na waziri au rais kumweleza chabgamoto zao na suluhisho la changamoto hizo.

mimi nlitaman kuwa wangefanya juhudi hizo kwa nia njema pasipo kuja kusubiri kutangaza mgogoro na serikali. na kama wamefanya wananchi tujulishwe nini maazimio yao.

wabunge wengi hawajui wazungumze nini kuhusu walimu, wengi hawana data au pengine hawajui matatizo ya kuanguka kwa elimu ni nini. walimu ni wadau wakubwa katika hili. tukubali tusikubali. tunaweza kuwa na big results now tukajidanganya kwa takwimu za kupika lakini ukweli ukabaki kuwa walimu wengi wamekata tamaa na maisha ya ualimu isipokuwa wachache wanaojua nin wanafanya.

tuwaheshimu walimu hawa waliotutoa mbali tunapata laana kuwa kuwadhalilisha na kuwasahau kana kwamba si kitu cha kufaa maishani mwetu.

WALIMUE ELEZENI MATATIZO YENU NA KAMA HAMYAJUI SEMENI SISI TUWASAIDIE KUYAORODHESHA. LAKINI SIAMINI KUWA TATIZO LENU KUWA NI USAFIRI.
 
Back
Top Bottom