Inakuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakuwaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Adili, Jan 5, 2009.

 1. A

  Adili JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,009
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Mwaka 1993, Judge (balozi) James Kateka alitunukiwa nishani hii hapa chini.....
  Papal Honour of the Grand Cross with the Star of the Order of Pius IX (1993).
  Judge Kateka ni mLutheri wa kuzaliwa. Nina dukuduku kidogo. Kuna mwanaukumbi anafahamu ni kipi mzee Kateka alifanya mpaka Vatican ikamtunikia nishani hiyo?
   
 2. m

  mwabaudi New Member

  #2
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu, zingatia kwanza kwamba Vatican ni nchi yaani State na ina mahusiano ya kibalozi na nchi nyingi ikiwemo ya kwetu Tanzania, Balozi kateka alikuwa Balozi wa Tanzania huko Vatican akiwa na makazi Bonn Ujerumani ( Kwa taratibu za kidiplomasia balozi aliye na makazi Roma Italia hawezi kuwakilisha nchi yake Vatican ndio maana yeye akawa balozi huko akiishi Bonn wakati huo mji mkuu wa ujerumani sasa ni Berlin) Nishani uliyoitaja ni nishani iliyotolewa kwake na nchi ya Vatican kama Balozi aliyemaliza kazi na kwa kipimo cha Vatican naamini ni kwamba waliona alistahili heshima hiyo kwa kazi aliyofanya katika kuendeleza mahusiano mema kati ya Vatican na nchi yake Tanzania. La msingi nishani ni ya nchi ya vatican si ya kanisa katoliki, hivyo hakupewa nishani hii kwa misingi ya imani yake ya roho aidha naamini kwamba nishani hii anaweza kutunukiwa mtu wa dini yeyote kwa kipimo cha nchi ya Vatican. Aidha ifahamike kwamba nishani zote wapewazo watumishi wa nchi yetu na nchi za nje hutolewa kwa ridhaa ya nchi yetu kupitia taratibu na kanuni zilizowekwa kwa mujibu wa sheria. Naamini kwamba haya yatakusaidia, Ahsante
   
Loading...