GE2025 Inakuwaje kati ya wagombea wote wa urais ni mabango ya Samia tu ndiyo yametapakaa mitaani?

GE2025 Inakuwaje kati ya wagombea wote wa urais ni mabango ya Samia tu ndiyo yametapakaa mitaani?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Intricate

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
395
Reaction score
1,232
KUlikuwa na haja gani ya kuwa na huu uchaguzi ikiwa ni maigizo matupu.

Nimezunguka Dar yote sijaona picha wala bango la mgombea mwingine yeyote wa Uraisi mbali ya Samia.

Ikija kwa wabunge na madiwani ni wa CCM tu ndio wametanda. Kwa picha chache za upinzani zilizopo ni vikaratasi vya A4 ambavyo vimemezwa na mipicha mikubwa ya wana CCM.

Huu uchaguzi umekuwa mithili ya mechi ya mpira ambayo wachezaji wa timu zote mbili wanafungia goli moja na point zote zinaenda kwa timu moja tu.
 
Wagombea wengine hawana time ya kuweka picha zao. Wanakula vacation ya kuzurula nchi nzima kwa magari ya kifahari waliyopewa.
 
Juzi nimeona picha za wagombea ubunge na udiwani kwa ccm na upinzani ila sijaona picha yeyote ya mgombea urais wa upinzani, yani nimeanzia tandika hadi mbagala ni hivyo hivyo tu unamuona Samia pekee.
 
Mabango ni mengi kama tangazo la kampuni ya simu. Ni aibu mno, kila mahali mpaka natamani kuayashusha. Lakindo hivyo unaweza ukatekwa ndani ya dakika ukiyashusha
 
Huu mwaka tume ingese.a kampeni ziwe wiki mbili tu alafu tuingie kwenye uchaguzi, uchaguzi wa kitapeli sana huu
 
KUlikuwa na haja gani ya kuwa na huu uchaguzi ikiwa ni maigizo matupu.

Nimezunguka Dar yote sijaona picha wala bango la mgombea mwingine yeyote wa Uraisi mbali ya Samia.

Ikija kwa wabunge na madiwani ni wa CCM tu ndio wametanda. Kwa picha chache za upinzani zilizopo ni vikaratasi vya A4 ambavyo vimemezwa na mipicha mikubwa ya wana CCM.

Huu uchaguzi umekuwa mithili ya mechi ya mpira ambayo wachezaji wa timu zote mbili wanafungia goli moja na point zote zinaenda kwa timu moja tu.
Bi Chura ni 🚮🚮🚮🚮, halaf hata haelewi kuwa mwakani majira kama haya tumeshaanua majamvi na kumsahau
 
Na watu wa mabango walahi wasilalamike!
WAnapiga hela ya KUFA MTU!
Ukisikia wakidai hakuna hela ya kununuwa mabasi ya watoto shule za kata, afya, elimu ujuwe hawataki tu!
 
Back
Top Bottom