Inakuhusu; uwe kwenye ndoa au la! Soma ndugu yangu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakuhusu; uwe kwenye ndoa au la! Soma ndugu yangu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tutor B, Jul 27, 2012.

 1. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  [h=3]Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote.[/h] [h=3]“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.[/h] [h=3]Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Jane. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Jane. Kwa kweli nilimdharau mke wangu![/h] [h=3]Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.[/h] [h=3]Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Jane aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.[/h] [h=3]Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.[/h] [h=3]Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Jane.[/h] [h=3]Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.[/h] [h=3]Nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Jane alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Jane tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.[/h] [h=3]Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.[/h] [h=3]Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Jane kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.[/h] [h=3]Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma… mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.[/h] [h=3]Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua…. nikapand ngazi. Jane alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Jane, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Jane, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’[/h] [h=3]Ikawa kama Jane alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.[/h] [h=3]Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Jane. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.[/h] [h=3]Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema….[/h] [h=3]Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu… Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira rafiki ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenue ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao[/h] [h=3]Mungu awabariki nyote mliosoma na kujifunza hapa[/h]
   
 2. M

  Maswi JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 897
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mbona inaonekana kana kwamba umetunga? ze way ulivyomalizia ndo haioneshi kuwa ni wewe, lakini hata kama siyo wewe UJUMBE umewafikia wengi.
   
 3. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  sio kutungwa tu, ni moja ya chain of emails inazozunguka mitandaoni kwa miaka kadhaa sasa.
   
 4. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Inafundisha sana kwa mtu ambaye yupo gizani katika mahusiano.
   
 5. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,142
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  i heard the same story before.
   
 6. ram

  ram JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,225
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Ndefu hiyo, but nimeisoma hadi mwisho, ina mafunzo kwa wanandoa, haya wanandoa someni hii story mjifunze
   
 7. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Vyovyote tutakavyosema ni nzuri sana na fundisho ndani yake.

  Hongereni sana ambao mliisoma message hii before kwani wengine hatukupata nafasi ya kuipata. Hivyo namshukuru mleta hoja.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 8. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hata walio nje ya ndoa yanawahusu ili siku wakiingia ndoani wazingatie kulinda ndoa zao kwa upendo.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 9. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Habari yoyote yenye kufundisha jamii - hapa ndo mahala pake. Itungwe au iwe halisi kinachomata ni je! kuna fundisho lolote kwa atakayeisoma?
   
 10. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  si hivyo tu m2 wangu, walio nje ya ndoa wasiingilie ndoa za watu kwani wanasababisha matatizo makubwa kwenye familia za watu.
   
 11. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Nia yangu ni kusomwa tu! Mboba bible inasomwa kila siku?
   
 12. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,388
  Likes Received: 726
  Trophy Points: 280
  ikiwezekana kila ijumaa tuweke vistory kama hivi vinaweza kusaidia kurekebisha majeraha ya ndoa kwa sababu fedha za outing hatuna lakini kwa story hizi zinaweza kuongeza sanaa na mabadiliko yakawepo
  asante kwa mchango wako mkubwa
  nitakuwa si mwingi wa fadhila nisipo mwomba MUNGU akubariki iwe kwa kukopi kutunga lakini kubwa ni ujumbe umefika
   
 13. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,498
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Av read this b4, bt stil i cnt get enough ov it..dah so sad!
   
 14. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sad story imeniacha mdomo wazi kwa kusikitika. Wish wakina Ray -Vicent Kigosi waitungie movie itakuwa nzturi na yenye kufundisha zaidi.
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mhhhhhhhhh! Kwa sisi vichanga vya mapenzi, ni somo tosha ila kwa wazoefu ni kama mwanaume kumwambi mwanamke eti anampenda hadi akinywa maji anamuna kwa glasi!
   
 16. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Thubutu huw hawana muda wa kupita humu madam. Wako bize na kopi nad pesti za kinaijeria
   
 17. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Safi sana, ni email inazunguka mitandaoni kwa miaka mingi sana. Ila kila mara nikikutana nayo huwa sichoki kuisoma maana inafundisha sana. Mke au mume ni mume/mke tu, usimwache mwenzio kwa sababu ya penzi la nje. Ndoa unaijenga wewe na mwenzio. Once you allowed a third part in between jua hamtadumu, hata kama mtadumu but ni kwa tabu sana. Hawa kina Jane na John wapo tu na kazi yao ni kuharibu tena wanataka wale wanaume/wanawake ambao income zao zimeshaanza kuwa stable ili wafaidi!!! Achana na hawa, na ndoa utafurahia. You will be counting 5, 10, 15, 20, .....50 yrs, 75 years of marriage without regret!!!
   
 18. E

  Emwaay Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana ina mafunzo na mantiki ya kutosha. Shauri yenu mnaosema ametunga,oh mara uliwahi kuisoma! Hatuhitaji kujua wangapi wamewahi kuisoma bali ni wangapi wameifanyia kazi na kufaidika nayo.
   
 19. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kama kichanga si ukalale ili wakubwa tuendelee na mambo ya wakubwa? (jokes usijali ndugu)
   
Loading...