Inakuaje mtumishi wa umma unafulia na kukosa hata mia wakati unalipwa mshahara?

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kujibana na kuwa na matumizi mazuri ya fedha. Watu wengi hawajui watumie maneno yapi ili waeleke.
Ndiyo maana ukimuuliza mtu nini tofauti kati ya msichana na mwanamke au kati ya women's day na Mothers' day watakuambia ni kitu kimoja.
Bahati mbaya nina watu wengi ninaowajua waliojibana kwa hali na mali na sasa wako mbali sana tu, possibly let's agree to disagree labda shida ni terms tunazotumia ndio zenye shida:

Kujibana vs Matumizi mazuri ya Fedha.
 
Kujibana,ubahiri,kuwa mchumi yote ni misamiati tu ambayo dhumuni lake kubwa kuwa na nidhamu na pesa.

Ishu inakuja kwamba je unajibana,mbahiri au mchumi kwa dhumuni gani endapo utakuwa unajibana ili uwekeze hicho ndicho kitu cha msingi maana utakula dagaa na ugari kwa kuamua ili siku za baadae uje kula pizza bila shida, ila kama utajibana bila focus yoyote ndipo inapokuwa sawa na bure.
 
Bahati mbaya nina watu wengi ninaowajua waliojibana kwa hali na mali na sasa wako mbali sana tu, possibly let's agree to disagree labda shida ni terms tunazotumia ndio zenye shida:

Kujibana vs Matumizi mazuri ya Fedha.
Hao walikuwa na matumizi mazuri ya fedha ndiyo maana walifika hapo.
Ukisema kujibana ndiyo hiyo ya ubahili.
Mfano. Badala ya kununua sofa, unanunua stuli, Badala ya ununue nyama angalau ule kwa wiki 2 au 3 ni mwendo wa dagaa tu na ugali. wali mpaka sikukuu. Unaumwa sana mpaka unahisi baridi lkn unameza panadol.
Hizi terms zinawachanganya sana watu.
Mbona hiyo ya utofauti haujanibu kati ya msichana na mwanamke? Siku ya women's day na mothers' day?
 
Ebu Angalia hii budget...

Chakula. cha mchana ...4000
Maji yakunywa 1000
Juice .....1000

chakura cha usiku kiko 4000
Balimi 2 Tsh 5000

Hapo ujaweka Usafiri ...pia vocha.... hapo pia ujaumwa ukanunua vidonge. ..hapo mama kijijini ujamtumia chochote ...Tena hayo nimaisha yamtu aliye single ukisema uoe ujue lazima uukimbie mji..yaani iyo laki tano aiwez kutosha.
Sio lazima ule chakula cha buku nne then bajeti ya balimi ondoa ....juice pia sio muhimu kiivyo hapo muhimu maji tu....... Mnafosi matumizi
 
Sio lazima ule chakula cha buku nne then bajeti ya balimi ondoa ....juice pia sio muhimu kiivyo hapo muhimu maji tu....... Mnafosi matumizi
Watu mnajua kuwapangia bajeti wengine. Kiufupi tu kila mtu apambane na hali yake.
Kila mtu ale atakavyo lkn likija kwenye suala la kupigana mizinga hapo ndipo sikubaliani na mtu yyte.
Kupigwa mizinga, kuhonga kuna leta mkosi
 
Sawa wasiwe wanalalama tu kwamba kipato hakikidhi mahitaji sijui nini wakati wanaishi juu ya bajeti iliyopo....... Pesa siku zote haitoshelezi kadri zinavyoongezeka na matumizi yanaongezeka mara dufu cha msingi ni kua na nidhamu kwenye matumizi ya pesa
 
Watu mnajua kuwapangia bajeti wengine. Kiufupi tu kila mtu apambane na hali yake.
Kila mtu ale atakavyo lkn likija kwenye suala la kupigana mizinga hapo ndipo sikubaliani na mtu yyte.
Kupigwa mizinga, kuhonga kuna leta mkosi
Hapana wale uliowasema wanaotumia laki 3 kwa siku,hua wanahonga sana na hawapati mikosi wala nini.
 
Pole sana. Ndiyo tatizo la wafrika hili. Wanapenda sana kujudge bila kuwa na uhakika wanachokisema. Inaonekana ww ulikuwa mpiga mizinga ukastaafu kwahiyo ukimuona mtu unahisi ni mpiga mizinga.
Pole sana tena sana.
Kuna kipindi unaweza pitia hiyo hali especially unapokuwa mwanafunzi.Kuwabomu wazazi,ndugu ,jamaa na marafiki.Ni fedheha kwa mfanyakazi kuwa mpiga mizinga.Sasa wewe mkuu unaonekana kama unampinga mleta Uzi!
 
Hayo ni yako. Unaweza kunionesha ni wapi nimempinga mtoa uzi?
 
Tatizo bado serekali na mashirika au makampuni wanalipa mishahara kishamba. Eti mpaka mwiaho wa mwezi. Wenzetu mshahara unalipwa kwa week. Kama mshahara wako ni 1m basi ugawanywe mara nne uwe unalamba 250k kila week. Huwezi kuishiwa na huwezi kuwa na madeni ya ajabu ajabu

Hasa ndugu zangu waalimu. Hili la kulipwa mwisho wa mwezi ni tabu sana kwao. Mshahara ukitoka tu nikulipa madeni mwisho wa siku anabakiwa na vijihela vya kutumia siku kama 5 anaanza kukopa tena.

Tubadilike. Tulipwe kila wiki badala ya kuaubiri mpaka mwisho wa mwezi
HR wakikusikia....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom