Inakuaje mpaka mtu anafeli O'level?

Mkuu kama ww ulifaulu,mshukuru Mungu tu,...umeeleza wazi kua Advance Physics ilikukimbiza,..na wenzako pia O'level ndio iliwakimbiza kama ww ulivyokimbizwa na hiyo Physics...ww ulipewa laki 5 ukasome tuition,wengine hawana huo uwezo wa kupelekwa masomo ya ziada....kuna ugonjwa kipindi cha mitihani,misiba n.k n.k,kwa hiyo kama ulifaulu shukuru Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa gharama ulizotumia ukaishia kupata C ya physics A level, ungepitia njia zetu za watoto wa wakulima (bila tuition) ungepata F wewe! Ila naungana mkono na ww kuwa advanced physics ndio somo gumu sana kusoma katika maisha yangu! Somo lilinitesa sana nikaishia kupata C kama ww, na sitamani kulirudia!
 
Wakifaulu wote nani atatukaangia chips yai, nani atatupigia debe, nani atatuendeshea boda, nani atatupokea mizigo pale ubungo. Maisha lazima yabalance kiroho safi.
 
nna division 4 ya form 4,mwana nilifeli now nna degree na nipo kwenye kufanya research kwa ngazi ya master +my own company ambayo naiongoza swali kwako mleta mada hyo 1 yako ya form 4 imekufanyia nn?


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ila maisha yanabadilika, ivi kweli mtu anapata 4 o level still anaweza kusoma degree na anafaulu??? Ingekua ni 4 ya a level inawezekana kwa sababu mambo yana change sana from o to a level. Mm niamini kitu kimoja kwako, matokeo yako ya o level yaliathiriwa na labda Mazingira ya shule, walimu hawakuwepo vzr, hukuwa na exposure na wanafunzi wa shule nyingine, walimu walikuwa wanafundisha matango pori, ulikuwa unmatured (siku izi watu wanamaliza form 4 na miaka 16). Mkuu hayo niliyoongea hapo juu yanachangia kwa asilimia kubwa! Tukubaliane tu na mtoa mada kuwa o level ni hatua moja rahisi sana kwa MTU kufaulu kuliko hatua nyingine(achana na primary ambapo siku izi wanalazimishwa kufaulu huku wengine wakiwa hawataki). Wewe inawezekana hukuweza kupata Mazingira mazuri ya kuperfom ukiwa o level japo ulikuwa na uwezo! Believe me or not
 
Ukifanya research utanyamaza.
Kuna watu wanadhani mazingira na changamoto za wanafunzi wote nchini zinafanana.
Kafanye research

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mtu Mimi nilipata division four iliwezekana tena very simple sababu kubwa kabisa nilikua sina NIDHAMU.. Hili swali LA kwenye interview "ULISHA WAHI KUFANYA MAKOSA" KOSA GANI then NINI ULIJIFUNZA nililijibugi kwa makosa hayo. Na nini ulichojifunza.. Wale wazee walipigiaa makofi. Wakaniambia after 4 weeks Kitaeleweka, Thanks God tunakula mema ya nchi kwenye maofisi yenu ya mapato [emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilitarajia ungewashauri vijana sasa wasomeje ili walau waepuke na zero....umeishia kupiga porojo tu....
 
Hapana Wala sivuti bangi mama, Ila inawezekanaje mtu kuondoka na division 0 or four O'level?
Ukishangaa hivyo kuna anayekushangaa kwa nini ulishindwa kuondoka na 1 ya pointi 7 o level na 1 ya point 3 a level. Tutaendelea kushangaana hivyo yaani.
 
nna division 4 ya form 4,mwana nilifeli now nna degree na nipo kwenye kufanya research kwa ngazi ya master +my own company ambayo naiongoza swali kwako mleta mada hyo 1 yako ya form 4 imekufanyia nn?


Sent from my iPhone using JamiiForums
JF hatari hainaga kapuku,wote wasomi matajiri
 
kwenye ofisi zetu za mapato huwa hakuna hayo maswali...
 
Shukran kwako Mwl Mtiga, ile tuition yako matata sana
Kutoka kwetu mpaka mapambano ilikua mbali lakini ulinisaidia
Ila mkuu acha mbwembwe ( sijafeli form four)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio wote wana akili ya kuelewa masomo ya darasani. Wengine akili zao ni kwenye sanaa kama mbwana samatta, barnaba na diamond

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote tusome PCM chief????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
H e Chi Ji Ero ndio nini ?Kama umekusudia tahasusi ya HGL ulipaswa kuandika hivi Eich Ji Eil.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…