Inashangaza lakini ndo ukweli wa maisha. "Ujapo wema , maumivu yafuata".
Ndugu Yako anafariki, unaamua kuwachukua wanae uishi nao na kuwasaidia kuendelea na masomo ila mwisho wa siku watoto wataanza kutoa shutuma, baba mdogo /mjomba / shangazi wanatubagua na kutunyanyasa. Mgogoro wa kifamilia hutokea.
Unakutana na watu kwenye maisha wanapitia changamoto za maisha , mambo Yao hayaendi , kila wanaowajua wamewapa mgongo. Unasema isiwe taabu unaamua kuruhusu waishi kwako ili watulize akili na kujitafuta. Baada ya kuzoea wanakupiga tukio , eidha wanabaka wanao, au wanakuibia na kutoroka. Wema wako unageuzwa maumivu.
Wakati mwingine unajitoa sadaka ya kuteketezwa Kwa mpenzi. Unaghalamia pesa, vitu, na muda wako. Unawekeza hisia as if ndo umetumwa na mbingu kuja kumtunza mtoto wa mamamkwe. Umejisahau kidogo unapigwa tukio hadi ukiwaza njaa usikiii na usingizi hauji na afya inazoofu.
Wakuu ebu tieni neno kwenye huu Uzi kuonyesha uzoefu wenu. Biblia yenyewe mahala flani imeandika Kwa sababu ya maovu kuongezeka upendo wa wengi utapoa.