Inahitajika miaka 1,000 kumfahamu rais Magufuli

Inahitajika miaka 1,000 kumfahamu rais Magufuli

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Inawezekana labda tukisie miaka hio. Kwenye jamii kumekuwa na masuali mengi sana kuhusu wapi tunaelekea. Wanaomuunga mkono Rais Magufuli wamekuwa wakijifariji kuwa watu hawamuelewi Mh rais wanaserma bado ni mapema mno, Lakini njia ndio muhimu , watu wanatafuta njia (Road Map) hawamuoni alivyochora ramani, haonekani kwenye ilani ya chama chake Lakini unamuona Magufuli binafsi.

Masuali yanakuja hivi kweli Rais watu hawamuelewi au haeleweki ? Inawezekana kuna tatizo kubwa. Hebu tuangalie kwa mifano.

Rais anasimamia ajenda gani kwa sasa ?

Tuanze na hapo. Mwanzo tuliamini anasimamia sheria, haki na usawa kwenye jamii. Ajenda hii ilifika mwisho kwenye zoezi la kuhakiki vyeti na kuanza kubagua, tuliendelea kuona zoezi la kutumbuwa lilivyochagua mwahala mwa kupita na kuwaacha wengine wanaoharibu hadi leo bila kuguswa.

Vipi ajenda ya ufisadi, Hatujui ni ufisadi upi anasimamia , unaweza kudhani pengine anashughulika na ufisadi mkongwe na kushughulikia wale mapapa yaliyoitia hasara nchi huko siku za nyuma, Hapana mara unamuona anakemea wengine . Hatukutegemea ndani ya miaka miwili kunaibuka ufisadi mpya wa 1.5 trilioni hazijulikani zilipo. Hatumuoni akikerwa yeye na wasaidizi wake zaidi ya kujikakamua kutetea na kutisha wengine. Anapata wapi tena uhalali wa kuwashughulikia wengine ilihali utawala wake umeshindwa kutuonesha fedha hizo zilipo.

Vipi Tanzania ya Viwanda na kuwa Rais wa Wanyonge. Hivyo viwanda haviakisi chochote kwenye walau bajeti ya maendeleo hii ya mwaka wake wa pili wa urais. Ndio kwanza tunalumbana na mgao wa maji si ya kunywa wala ya kumwagilia mashambani kupata mazao na maji ya kusafishia mekanikia zetu. Hao wanyonge ni wepi mbona kodi ni nyingi na fursa za ajira hazionekani.

Jambo lengine kubwa ni kushindwa kuinyoosha nchi na serikali kwenye sura ya taasisi. Kilicho wazi ni kumuona Rais Magufuli pekee. Unamuona rais Magufuli akiamua mambo kwenye maeneo ambayo pengine yalipaswa yafanywe kwenye ngazi ya wizara au halmashauri. Unaweza kujiuliza hivi kumekosekana vikao vya ndani vya serikali au wasaidizi wa rais hawamuelewi kiongozi wetu au kuna nini ? Kitendo cha kila baada ya muda kumuona rais anatolea ufafanuzi mambo fulani tena madogo tu kinaleta taswira kuwa pengine wasaidizi wana uoga au wamegoma kimya kimya au hawamuelewi. Hayo ni baadhi ya maeneo tu.

Halafu hii tabia ya kusubiriwa Rais ndio aelezwe changamoto kwenye mikoa ndio kusema wasaidizi wake huko chini wameshindwa kweli ? Zile jitihada za waziri Lukuvi kwa mfano kwenye migogoro ya ardhi zimegonga mwamba au kuna nini huko ?

Nani anapaswa kumuelewa Mh rais ?

Kwa maoni yangu waliopaswa kumuelewa Rais kwanza ni wasaidizi wake wakuu wakiwemo Makamo wa rais na waziri Mkuu, baadae lije kundi la mawaziri na watendaji waandamizi serikalini, wafuate viongozi wa mikoa , wilaya , mihalmashauri, majiji na manispaa, kata tarafa, vijiji na mwisho wanaanchi wa kawaida.

Kila nikijaribu kutathmini sioni hivyo. Na tatizo Kubwa ni kuwa Rais haonekani rangi yake halisi. Anabadilika kila wakati na kuyumbisha wasaidizi wake. Viongozi wangapi wamefanya maamuzi lakini baadae rais anatengua maamuzi na kuweka ya kwake ? Utajuiliza hivi hakuna hata vikao elekezi ? mbona kila wakati kuna kutengua au kubadilisha maamuzi ?


Kwa maelezo hayo machache na tafakuri hio nadhani kuna tatizo. Rais anapaswa kujichora sura halisi ili watanzania waweze kumuelewa.

Kwa sasa bado hali hairidhishi.



Kishada.
 
Jiwe limekua jiwe kwelikweli
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Rais anaamini miundombinu na kununua nsege na magari ndio kila kitu na ndicho atakachokuja kujitapa kwenye kampeni za 2020 kuwa watanzania nimenunua ndege, nimejenga barabara, nimejenga sgr, sasa sijui waziri wa uchukuzi naye atasemaje
 
rais magufuli anaeleweka kabeba agenda ya viwanda kuifikisha tanzania uchumi wa kati..hilo wote wanalijua wanafki na wasio wanafki
 
Nsege ndio nini?
Rais anaamini miundombinu na kununua nsege na magari ndio kila kitu na ndicho atakachokuja kujitapa kwenye kampeni za 2020 kuwa watanzania nimenunua ndege, nimejenga barabara, nimejenga sgr, sasa sijui waziri wa uchukuzi naye atasemaje
 
Nasemaa Achaa tunyookee... Mikopooo Asitoee kama alivyosemaa... Mafutaa bei juu... Sukarii beii chafu... Hadi 2020 labda ndo akili zitaturudiaa... Akazee vyumaa mpaka mwisho
 
  • Thanks
Reactions: PNC
rais magufuli anaeleweka kabeba agenda ya viwanda kuifikisha tanzania uchumi wa kati..hilo wote wanalijua wanafki na wasio wanafki
Hivi huo uchumi wa kati hauhitaji ushirikishi wa wasaidizi wake au ndio kaubeba yeye binafsi na kuchagua wapi apeleke rasilimali na wapi atengue na kupunguza ?

Tunamuona Magufuli na si Serrikali kama serikali.

Hata Pole pole anashindwa kuitetea serikali ya chama chake.

Kwanza yuko wapi Katibu Mkuu Kinana aje aeleze ufanisi wa serikali ya Viwanda.
 
Yeye mwenyewe alisema urais alisukumiziwa hakujiandaa. Labda tumpe mpaka mwaka 2030 ili ajiandae vizuri
 
Ukijifanya unatumbuwa kama afanyavyo yeye mara anatenguwa, ukijifanya kunyamaza bila kuchukuwa hatua jumba linakuangukia.
 
Sasa hivi kuna trends za baadhi ya wasaidizi kupiga ukimya utafikiri hawapo, mazingira yanawatesa kumsema RC fulani hata kama anavunja sheria wazi wazi kwa kuogopa kutumbuliwa. Si hayo tu kuna muingiliano wa majukumu lkn rais haoneshi njia .
 
Mlivaa manguo yenu yenye rangi ya mbogamboga mkiimba 'acha waisome namba eeh' mlidhani hizo namba wasomaji ni akina Mbowe,Lowassa wake zao?
Hao wala hawasomi hizo namba zenu.

Pambaneni na hali zenu.
 
rais magufuli anaeleweka kabeba agenda ya viwanda kuifikisha tanzania uchumi wa kati..hilo wote wanalijua wanafki na wasio wanafki
Ni washamba na Mambubu tu, ndio waliobakia kuaminishiwa hivyo, lakini wenye upeo kidogo walisha badilisha muelekeo, wanajua jamaa badala ya kujaribu kuleta maendeleo kwa Watanzania, yeye ameamua kjiletea maendeleo binafsi na jamii ndogo inayomuhusu yeye tu.
 
Back
Top Bottom