Inafaa kumpa maziwa ya ng'ombe mtoto wa mwezi mmoja?

Kuna aina tatu kuu za ulishaji wa mtoto...
Exclusive breast feeding- hapa mtoto anapewa maziwa ya mama TU kwa muda wa miezi 6
Replacement feeding..hapa badala ya maziwa ya mama mtoto anapewa vyakula vingine esp maziwa kuna aina mfano Lactogen milk

Mixed feeding....mchanganyo huu

Kitaalamu mtoto wa mwez 1 haruhusiwi kupewa maziwa ya ngombe kwani yanamweka mtoto katika hatari ya kupata magonjwa hasa ya kuharisha maziwa ya ngombe yana fat nyingi sana hivyo mtoto hushindwa kumengenya hiyo Fat utumbo wake bado hujakomaa.

Pia maziwa ya Mama yana VIRUTUBISHO VYOTE MUHIMU KWA MTOTO MCHANGA na pia kunyonyesha kunapromote upendo kati ya mama na mtoto na pia maziwa yana joto linalotakiwa na mtoto.

Kama unashida ni vizuri kumwona dr za ushauri zaidi.
 
Hapana,kama mama yake anatoa maziwa vizuri apatiwe maziwa ya mama tu kwa muda wa miezi 6. Na kuanzia miezi 6 kuendelea anaruhusiwa kupewa hata na maji lakini yasiyo na sulpher ndio mazuri kitaalamu inashauriwa hivo. Incase mama mzazi hatoi maziwa atafune mihogo mibichi,Mchele uliolowa,Katanga mbichi,ndizi bukoba na vyakula vitakavyo pelekea kuzalisha maziwa. Lakini mfano mama hayupo tumia lactogen but kuwa makini maana yameingia fake now days,lakini pia tuma maziwa ya infacare.
 
Hapana aisee,maziwa ya ng'ombe ni kuanzia mwaka mmoja,Tafuta maziwa ya kopo ya kuendana na umri wake yale ya infants 0-6 months.Katafute Lactogen 0-6months in case upo Tanzania.
 
kama mama yupo na anamaziwa ya kutosha ni vema msimpe asipewe hayo ya ng'ombe, ikishindikana apewe lactogen.
hii tabia ya kutonyonyesha watoto ndio inapelekea wakikua wanakua bashite na kupata fa fa fa na kufanya maamuzi mabovu!
 
Ukizingatia lishe ya mtoto. Mtoto atukua kwa raha. Kuna wengine mwezi mmoja anampa uji. Wewe mtoto mnyonyeshe mpaka miezi sita tu. Usimpe chochote. Na ikifika miezi 6 sio kumpa maziwa na uji wa ulezi. Chukua blenda na vyakula kama njegere, ndizi, samaki, carrot, parachichi. Mtengenezee chakula. Kuna app za kukuonesha mtoto stage ya kukua na vyakula anavyostahili kula download au subscribe email ndo maana ya smartfone. Ukizingatia lishe mtoto wako atakua kwa raha.
Kama maziwa ya mama hayatoshi kuna maziwa spesho ya mtoto.
 
Maziwa ya ngombe ni chakula cha ndama yakizidi kwa ndama ndo tunayapata sisi binadam kama chakula/kinywaji wengine refreshment cold drink

Kuna Dhana imekaa kichwani pa wanawake wengi wa kisasa kwamba kunyonyesha kunaharibu maumbile
Kwamba maziwa ya mama hayatoshi kwa mtoto?
Kwamba mtoto anapata kiu anahitaji maji?
Kwamba anafanya kazi kwa hiyo lazima mtoto apate mbadala wa maziwa ya mama.

Hizo zote ni dhana potofu
Maziwa ya mama ndo chakula sahihi kwa mtoto mchanga mpaka miezi Sita
Yana maji ya kumtosha mtoto
Ni natural
Yanajoto linaloendana namtoto
Yana kinga dhidi ya magonjwa mengi ya utotoni n.a. uzeeni
Yanafanya makuzi ya mtoto deveplopmental Mile stone ziende vizuri
Yanatengeneza bond Kati ya mama n.a. mtoto
In summary sababu za kumyonyesha mtoto maziwa ya mama hazilinganishwi wala hazina mbadala
Mama anahitaji matunzo wakati wa kunyonyesha ili aweze kupata maziwa yanayomtosha mtoto
Anahitaji psychological support kitendo cha kunyonyesha kinahitaji utulivu wa ajili/stress free
Sio gharama kumnyonyesha mtoto kama kununua maziwa

Maziwa ya ngombe ukimpa mtoto wawezategemea yafuatayo
KUHARISHA ZAIDI KULIKO ANAYENYONYA
MAGONJWA YA MFUMO WA HEWA ZAIDI
UZITO USIOENDANA NAMTOTO ZAIDI
KUCHELEWA HATUA MUHIMU ZA KUKUA MF KUKAA KUSIMAMA KUTEMBEA KUONGEA
MAGONJWA YA ALLERGY ZAIDI
MAGONJWA YA PRESSURES N.A. SUKARI UJANANI NA UZEENI
KUPOTEZA KUMBUKUMBU KATIKA UMRI MDOGO
N.A. MENGINE MENGI

KAMA WEWE NI MFANYAKAZI WA SERIKALI UNAPUNGUZIWA MUDA WA KAZI FROM 3-6MONTH ZA MTOTO UNAWEZA UKAKAMUA MAZIWA YAKO KATIKA HALI YA USAFI N.A. YAKATUNZWA KWA FRIDGE MSAIDIZI ATAMPA PANAPO UHITAJI
WALA HUHITAJI MASHINE
SIJUI KITU GANI FIKA KITUO CHA AFYA PATA ELIMU ELEKEZI JINSI YA KUKAMUA N.A. KUTUNZA MAZIWA

NIMPONGEZE MKE WANGU MAMA B KWA KUMPA MWANETU MAZIWA YA MAMA MPAKA ALIPOTIMIZA MIEZI SITA
KUANZIA MIEZI MITATU ALIKUA ANAMKAMULIA N.A. YALIMTOSHA VIZURI
AMEKUA N.A. AFYA NJEMA SASA NATUMAI AFYA NJEMA ATA BAADAE MAISHANI

WATAALAMU WNASEMA KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA KUPOROMOKA KWA MAADILI N.A. KUKOSA KUNYONYA MAZIWA YA MAMA KWA WATOTO WA KIZAZI CHA LEO
 
Naona tupo tofauti kidogo,,,moyo wngu haujawahi kuyaamin maziwa ya makopo,,muda mwngine hawa watoto kiukwel tinajitahid sana kuwapa lishe bora lakin yaliyonikuta mm mwenzenu Mungu anajua...

Mwanangu alikataa kunyonya siku siku ya kumi baada ya kuzaliwa,,,kiukwel na ndama ndio kwanza alikua ana siku 7 toka kuzaliwa,,aisee Mungu alimsimamia wakashare na yule mtoto wa ng'ombe yale maziwa mpka leo ana 5 years.. Hajawah kuugua wla kupata tatizo mpka leo,, ila kiukwel niliona namtesa lakin ndio hvyo kakua leo anadunda shule fresh kabsa.. Ila tu hali samaki....sijui akikuwa zaid
 
Naona tupo tofauti kidogo,,,moyo wngu haujawahi kuyaamin maziwa ya makopo,,muda mwngine hawa watoto kiukwel tinajitahid sana kuwapa lishe bora lakin yaliyonikuta mm mwenzenu Mungu anajua...

Mwanangu alikataa kunyonya siku siku ya kumi baada ya kuzaliwa,,,kiukwel na ndama ndio kwanza alikua ana siku 7 toka kuzaliwa,,aisee Mungu alimsimamia wakashare na yule mtoto wa ng'ombe yale maziwa mpka leo ana 5 years.. Hajawah kuugua wla kupata tatizo mpka leo,, ila kiukwel niliona namtesa lakin ndio hvyo kakua leo anadunda shule fresh kabsa.. Ila tu hali samaki....sijui akikuwa zaid
Kwako una sababu mtoto alikataa KUNYONYA hivo uliangalia mbadala uliokua karibu nafuu n.a. unaopatikana utakaohakikisha kutokukosekana

Hilo lilikuachaguo sahihi
Kwangu Mimi kama ni kuchagua maziwa ya ngombe au kiwandani nilichagua pia ya ngombe kwa mwanangu wa kwanza mama alipoanza kwenda kazini
 
Naomba kujuzwa kama inafaa mtoto Wa mwez mmoja kupewa maziwa ya ng'ombe
Kuna fomula ya kuumpa mtoto maziwa ya n'gombe, yanaongezwa maji na sukari. Lakini tafadhali uulize kwenye clinic ya watoto ni kiasi gani. Ninavyokumbuka ni theluthi moja maji, ila kiasi cha sukari sikumbuki.
 
Ushasema maziwa ya nģombe kiukweli maziwa ya nģombe hayakuwa yameandaliwa kunywewa na binadamu na kimsingi kumpa mtoto mdogo ni makosa makubwa maziwa ya mama ndicho chakula sahihi cha mtoto kwa miaka 2_3 kwani ni mahsusi kwa maendeleo na ukuaji timamu wa ubongo wa mtoto kiakili ambapo maziwa ya nģombe ni kwa ajili ya mtoto wa nģombe ambaye hahitaji kukua kiakili yanasaidia kukua kiumbo tu lakini akili haikui kwa hiyo uchaguzi ni wako ndugu
 
Naomba kujuzwa kama inafaa mtoto Wa mwez mmoja kupewa maziwa ya ng'ombe
Inawezekana kwa vipimo vya maji maalumu maji zaidi maziwa kidogo ,naomba muone daktari aliye karibu akusaidie mchanganyiko huo na uhakikishe yanachemka sanaaaaa na uwe mwangalifu usafi wa vifaa utakavyotumia kumlisha mtoto .Mungu akutangulie
 
Back
Top Bottom