Inadaiwa nyoka akifa anaweza kufufuka kwa kupewa majani ya mti wa ajabu na nyoka mwenzie

Mkuu story yako pia nilishawahi ambiwa na watu wa makabila mawili tofauti nilipotembelea vijiji vyao. Ila mie nilichowahi ambiwa ni kwamba, ikitokea ukaujua huo mti au jani ambalo nyoko huyo kachuma unakuwa umebahatika kujua dawa asili ya kutibu sumu ya nyoka aina yeyote yule.

Note: Nyoka huwa anachuma hilo jani kwa umakini mkubwa sana ili asionwe na binadamu yeyote yule. Ila swala la kuhusiswa na M/Mungu au ukimwona lazima akuue hii sijui na sijawahi sikia.

Hivyo basi sikuwa interested sana na story ile. Bt wew sasa unakuwa mtu wa 3
Kuhusu umakini ni kweli. Kuhusu kukuua nayo ina kaukweli. Lakini uwezo wa mwenyezi Mungu hapo kasingiziwa. Maana asipokuoona ndio ushakuwa mganga mkuu
 
Hadithi kama hizi husimuliwa watoto kabla ya kwenda kulala baadaye huwa wanaogopa hata kuingia chumbani mwao kulala.

Leo wanasimuliwa watu wazima alafu asubuhi.
UONGO AMBAO WATOTO HUWA WANASIMULIANA WAKIWA MAPUMZIKO AU WANARUDI NYUMBANI TOKA SHULE.
Hakuna jinsi,TV zote msiba, acha atupige kamba
 
1ef83982dc243bea98594cd1b7b58353.jpg
 
Hizi story zina uhalisia hususan hiyo ya kumkata kichwa nyoka baada ya kumuua maana usipofanya hivyo inasemekana wenzake watamfufua.Pia kikwetu katika kabila letu ukitamka neno nyoka lazima uteme mate kaskazini huku ukitamka maneno fulani ili kuepusha kuumwa na nyoka. Ambalo nimethibitisha na nina uhakika nalo ni urafiki kati ya nyoka na kinyonga.Inasemekana ukimuua kinyonga nyoka anaweza kumfufua na ukimuua kinyonga lazima nyoka alipize kisasi.Nilipokuwa mdogo nilimkuta kinyonga aliyekufa nikaanza kumchezea kwa kumtoboa macho.Nilipowaeleza ndugu zangu waliniambia nikamuombe msamaha huyo kinyonga haraka ila nikawa mkaidi.Siku hiyo hiyo nikiwa na wenzangu kama 9 tukicheza nje ya nyumba alikuja nyoka mkubwa sana cha ajabu nyoka yule alikuwa ananifuata mimi tu... bahati nzuri wenzangu walinisaidia kwa kumuua yule nyoka haraka.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu story yako pia nilishawahi ambiwa na watu wa makabila mawili tofauti nilipotembelea vijiji vyao. Ila mie nilichowahi ambiwa ni kwamba, ikitokea ukaujua huo mti au jani ambalo nyoko huyo kachuma unakuwa umebahatika kujua dawa asili ya kutibu sumu ya nyoka aina yeyote yule.

Note: Nyoka huwa anachuma hilo jani kwa umakini mkubwa sana ili asionwe na binadamu yeyote yule. Ila swala la kuhusiswa na M/Mungu au ukimwona lazima akuue hii sijui na sijawahi sikia.

Hivyo basi sikuwa interested sana na story ile. Bt wew sasa unakuwa mtu wa 3
Unajuaje kama huyu ni mtu wa tatu...??? Je pengine ni mmoia kati ya walewale wawili waliokuambia....kaamua kujiunga jf
 
Jamani eeh hivi mnajua kwamba nyoka hawafagi?

Nyoka ndugu zangu hawafagi kiholela holela. Hawaumwagi magonjwa hovyo hovyo. Kama kufa labda auliwe na watu au afe kwa kupigana na nyoka mwenziwe au mnyama mwengine.

LAKINI HATA AKIFA BADO ANAWEZA KUFUFUKA TENA
Nyoka yeyote kama akifa huku akuwa hajapondeka kichwa au kukatwa kiwili wili. Basi anaweza kufufuliwa tena na nyoka mwenziwe na akarudi kwenye uhai tena.

Yaani nyoka wamepewa bahati kubwa na mwenyezi Mungu. Hawa nyoka wana mti wao maalum. Mti huo wanautumia kwa kurudisha uhai pindi wanapokufa kama wakiwa hawajapondwa kichwa wala kukatwa kiwiliwili.

Nyoka yeyote atakaye muona nyoka mwenzie amekufa. Anawahi haraka kwenye mti huo anachuma jani kwa mdomo na anaenda kumuwekea nyika mwenzie ambae amekufa. Na yule nyoka aliyekufa akishawekewa lile jani la huo mti. Anarudisha uhai pale pale na anaendelea kuishi kama zamani.

(Hili suala la nyoka kufufuana kwa kutumia majani ya huo mti ni kweli kabisa Mimi mwenyewe niliwahi kushuhudia kwa macho yangu. Zamani sana nilipokuwa mdogo. Nilikuwa darasa la pili.

Nakumbuka nilikuwa naenda shule nikaona nimpitie rafiki yangu ili tuende pamoja. Sasa wakati tunaenda shule mimi na rafiki yangu tukafika sehemu fulani yanye njia panda. Tukamuona nyoka amekufa. Tukaenda hadi pale alipokufa nyoka. Alikuwa ni nyoka wa vichwa viwili. Wakati tunamshangaa yule nyoka. Ghafla!. Tukasikia sauti ya mchakacho kwenye majani. Tukashtuka na kugeuka.

Tukamuona nyoka anakuja kwa speed huku kang'ata jani mdomoni. Tuliogopa tukakimbia mbio. Lakini wakati huo tulikuwa hatujui lolote kuhusu historia hii).

UTAKUWA MWISHO WA MAISHA YAKO UKIMSHUHUDIA NYOKA ANAPOCHUMA JANI
Ukimshuhudia nyoka wakati anachuma jani kwenye huo mti wao wa uhai. Lazima ufe hauwezi kuishi. Tena atakuuwa nyoka huyo huyo uliyemshuhudia. Atakukimbiza kwa speed ya ajabu mpaka ahakikishe amekung'ata. Na akisha kung'ata hauwezi kuwa na muda mrefu wa kuishi utakufa mapema kabla haujatoa siri.

Inasemekana kwamba mti huo haitakiwi aufahamu mwanaadamu yeyote maana. Tukiufahamu tunaweza kuutumia kwenye kufufuana kama wanavyofufuana nyoka.

Hivyo yule nyoka anapokukimbiza baada ya kumuona anavyochuma jani. Ni kwamba anapewa uwezo na mwenyezi Mungu ili uthibitiwe kabla siri haijatoka.

Mimi na yule rafiki yangu nafikiri tulinusurika kwa sababu hatukumuona wakati anachuma jani. Tulimuona alipokuwa analeta jani kwa mwenzie la sivyo tungepotea zamani.

NYOKA HAWAFI HUWA WANAPAZWA
Kisa cha nyoka kutokufa hovyo na kupewa chance ya uhai kupitia mti wa ajabu. Ni kwamba inasemekana nyoka huwa wanaishi muda mrefu sana. Na wakishazeeka. Wanashindwa kusogea popote wanaishi hapo hapo hadi mchwa wanawajengea katika miili yao. Huo ndo unakuwa wakati wao wa kupazwa.

Wanapazwa kwa uwezo wa mwenyezi mungu. Huwa wanafungwa nyororo inayotokea mbinguni na kuvutwa kurudi mbinguni. Wakati wanapopazwa unatokkeaga upepo mkali unaozunguka au wingu zito leusi...
duh nyoka mwenye vichwa viwili then nyie hamkuuliwa
 
Mkuu story yako pia nilishawahi ambiwa na watu wa makabila mawili tofauti nilipotembelea vijiji vyao. Ila mie nilichowahi ambiwa ni kwamba, ikitokea ukaujua huo mti au jani ambalo nyoko huyo kachuma unakuwa umebahatika kujua dawa asili ya kutibu sumu ya nyoka aina yeyote yule.

Note: Nyoka huwa anachuma hilo jani kwa umakini mkubwa sana ili asionwe na binadamu yeyote yule. Ila swala la kuhusiswa na M/Mungu au ukimwona lazima akuue hii sijui na sijawahi sikia.

Hivyo basi sikuwa interested sana na story ile. Bt wew sasa unakuwa mtu wa 3
Huu ndio uhalisia ulioandika, huyo ndugu story yake angeishia para ya pili tu.
 
Back
Top Bottom