Inaashiria nini kumuota x girlfriend mara kwa mara.

Inaashiria nini kumuota x girlfriend mara kwa mara.

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
10,082
Reaction score
2,358
Mambo vip wadau?kuna dada niliachana nae muda kidogo,na nakumbuka huyu dada hatukuachana kwa amani{tulitoleana lugha chafu}ila baada ya muda tulitafutana tukaombana msamaha,tukakubaliana kwamba hata kama tunaachana basi tuachane kwa uzuri..imepita miaka miwil sasa tangu tupigane chini,ila me tangu huu mwezi umeanza nimejikuta namkumbuka na namuota mara kwa mara{for good things}wakati mwingne najaribu kutafuta hata number yake ili nianze kumchokoza kwa kumchombeza lakn nafsi inasita..sasa wadau nyie mnanishauri nin,nijaribu kujipendekeza kwake kwa kumtafuta tena au nikifanya hvo ataniona bushoke but kikwel nahisi kumkumbuka na kumpenda flani hvi ila nkikumbuka that day tulivoznguana nakosa pozi la kumwingia.
ANGALIZO:kama huna kitu cha kunishauri,naomba upite kimya kimya tu ili tusikwazane.
 
We bado unampenda na kumuwaza mara nyingi na ndo maana unamuota hyo mpenzi wako kila siku as ndoto ni mazao ya mawazo yetu ya mara nyingi zaidi au mambo tuliyofanya wakati wa mchana.Usilazimishe mapenzi yaliyokufa tayari unless uwe na uhakika kuwa zilipendwa wako pia anakupenda bado coz what if zlipendwa wako hana tena feelings na wewe au keshaolewa utalazimisha kurudisha mahusiano?jipange utazame future yako and you can make it.
 
hahahahahahaha uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii binadamu wengine shughuli ipo mtu mmeshaelewana iwe mwisho,kila mtu kapita njia yake ww unamuwaza mwenzio afu unasingizia ndoto loh hiyo ndo imeshatoka ulimuona wa kazi gani wenzio waliwaza utamuacha lini...........tafuta wa kwako.
 
Mara nyingi ndoto huwa ni replay ya yale uliyoyaweka akilini mwaka hivyo basi huyo bado unampenda na unamfikiria sana

Vinginevyo alikuroga wakati wa kugegedana
 
We bado unampenda na kumuwaza mara nyingi na ndo maana unamuota hyo mpenzi wako kila siku as ndoto ni mazao ya mawazo yetu ya mara nyingi zaidi au mambo tuliyofanya wakati wa mchana.Usilazimishe mapenzi yaliyokufa tayari unless uwe na uhakika kuwa zilipendwa wako pia anakupenda bado coz what if zlipendwa wako hana tena feelings na wewe au keshaolewa utalazimisha kurudisha mahusiano?jipange utazame future yako and you can make it.

uliyoyasema ni ya kweli mkuu,na ndio kilichokua kinanitatza zaidi.ila what if nikitest zali,maana nimechungulia profile yake ya fb kaandika yuko single...hicho si ni kiashiria cha kwamba naweza pewa chance au?
 
Acha kuchelewa wewe!
We mtafute, kuandika fb yuko single siyo lazima iwe kweli!!!
Lakini, wakati mnaachana kwa mara ya kwanza nani aliyekua chanzo cha matatizo...????
Kama alikua yeye usimtafute, ila kama wewe ndo ilikua sababu mtafute omba msamaha, ila kwakua unaogopa yawezekana yeye ndiye alikua chanzo!
Kama bado unamtaka serious na wewe ndiye ulikua chanzo rudi, ila kama hauko serious achana nae.. Siyo vizuri kuchezea tym ya mtu!!!
 
Daaaah! No wonder mnamchango mkubwa kwenye maumivu yenu!
Alaf ukitoka uko una lalamika.

Hivi tabia ya kula matapishi yenu mtaacha lini?
 
Chelewa chelewa utakuta mwana si wako nenda kajisalimishe mapema
 
Mkuu fanya hivi, achana na yaliyopita,inawezekana hata yeye anapata wakati mgumu kama wewe,kamata simu pigia yeye mengine yatajiseti huko mbele polepole.Jishushe tu.
 
anakuvuta kwa mganga kimya kimya lazima urudi tu

Mambo ya kiswahili hayo - waganga wa wapi; sema dem huyo ameenda kwa Kakobe akaombewa na sasa mpango wa muumba wa wapendanao unataka kujirudia.
 
pole kaka.
hizo kumbukumbu wala sio tatizo zinatokea maana ni mtu ambaye alikuwa sehemu ya maisha yako. sasa wewe potezea hizo feeling na plz plz husimtafute ng'ooo ukimuanza tuu utakuja kujilaumu baadae
 
Vitu vingine si lazima uvilete kwenye mitandao kisa huonekani! Mlipokuwa mnazinguana na huyo manzi ulikuja kusema kwe mitandao? Kama si uzombi ni nn?
 
Usidhubutu kumtafuta kabisa. Hakikisha huna mawasiliano nae na fb mu unfriend ila kama unataka upara na kuwa kichaa wa mapenz mtafute.
 
Vitu vingine si lazima uvilete kwenye mitandao kisa huonekani! Mlipokuwa mnazinguana na huyo manzi ulikuja kusema kwe mitandao? Kama si uzombi ni nn?[/QUOTeh teh teh.....c uliombwa upite jaman!
 
Vitu vingine si lazima uvilete kwenye mitandao kisa huonekani! Mlipokuwa mnazinguana na huyo manzi ulikuja kusema kwe mitandao? Kama si uzombi ni nn?

mkuu,samahani,nimetoa angalizo,umeliona au nkuonyeshe?
 
Inaashiria wewe ni looser ambae even after two years u have failed to get over a woman..cna uhakika kama yeye anakukumbuka au vipi..hicho ndo kinachoashiria..!
 
Back
Top Bottom