In, Within and Out

In, Within and Out

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
525
Reaction score
2,951
Nimekaa usiku saa 5 usiku ni kiwaza na kuwazua,wapi nchi yetu inaelekea juu ya Tukio la kushambuliwa kwa Kiongozi,Mbunge,Rais wa TLS,Mwanasheria ,nikafumba macho nikamuombea Dua kwa Mungu.

Nikaketi chumbani kwangu,Mawazo yakinijaa nikijiuliza ni kundi gani waliofanya huu ,unyama.Nikaamua kutafuta kitabu nisome Katika *MAKTABA YETU* ,ili angalau nipunguze stress.

Nikaona kitabu cha *Nicole Machiavelli* kinaitwa *Prince* how to acquire and maintain political power(Namna ya kupata mamlaka na kuyalinda mamlaka hayo dhidi ya wengine),nikaanza soma Nadharia za huyu mwanafalsafa ,moja inasema *For a prince to maintain his political power should be cruel than merciful*(ilikiongozi mkuu aweze kulinda madaraka yake ya kisiasa lazima awe katili zaidi ya mwenye huruma),nikaendelea soma Nadharia zingine " *Prince is safer to be feared than loved*nyingine amezungumzia *ready to kill so as to survive* prince anatakiwa awe tayari kuuwa ili kuendelea kuishi ktk madaraka.yote haya yalifanya nirudishe fikra tena Juu ya Tundulisu huko alipo anaendeleaje, niliamua kukiacha kitabu hiki na kuinama zaida ya dakika 15 nikimuombea dua huko alipo,na nilitafuta kutafuta kitabu kingine hiki sikukipenda.

Nilipata kitabu ,kingine cha *Thomas Hobbes* kinaitwa *Leviathan* humu anazungumzia ,juu ya Nguvu ya Monarch kuwa king anatakiwa awe na nguvu zaidi ya yeyote ,na yeyote anayepinga mamlaka ikiwa anaishi vizuri kwa amani anatakiwa akomeshwe,King should be powerful , unconstrained ,ulimited by any body and the one who protests against regime while is given physical protection should be hurt" hapa bado mawazo yakarudi kwa Mh. Tundulisu,nikahisi kuvurugwa ,nikaamka nikaenda kitandani ila mawazo yakawa yamejaa .usingizi ukawa haupatikani.

nikaamka tena kwenda kutafuta kitabu kingine,kizuri kinaitwa *THE HISTORY OF THOMAS ISIDORE NOEL SANKARA* .huyu alikuwa Rais wa bukinafaso(UPPER VOLTA) Aliyeingia madarakani mwaka August, 4 ,1983,yeye na rafiki yake kipenzi Blaise Compaore,Compaore alikuwa ni mtu wa tamaa ya madaraka kabla ya kufanya mapinduzi yeye na Thomas Sankara yale ya 1983 dhidi ya meja ,Jean Baptiste Ouedraogo,nyuma alikuwa na stori ya kufanya mapinduzi katika nchi kadhaa afrika kabla hajakutana na Thomas Sankara akawa Rafiki yake 1976 Morroco katika military training.

Walikuwa viongozi wa chama kimoja,national revolutionary Council, walifanya kazi wote kama Rais na Makakumu ,Sankara Rais,Compaore makamu.

Compaore alikuwa na nia ya kutawala ,nia ya madaraka,na akamuona Sankara anakubalika na wananchi,anapendwa,akaona hatowahi kuja kuongoza Burkina Faso kama Thomas Sankara Yupo hai ,mwaka 1987 akampindua na kumuua Rafiki yake kipenzi kwa sababu ya madaraka ya kuongoza. *nikajiuliza hivi inawezekana mtu wa karibu yako akuangamize sababu ya tamaa ya madaraka*??

nilipofika hapa nikawaza jaribio dhidi ya Tundulisu, mawazo yakarudi kwa kasi ya ajabu nikafunika kitabu ,Saa 8 :23 usiku sina usingizi ,vitabu vyote viliendelea nipa stress.

Nikawaza kitabu kimoja ,niliwahi ambiwa nikisome na mwalimu wangu,Dr.Hadija Mwenda,na Sir.vedasto hamza kinaitwa *The looting Machine* nikaenda kukiangalia bahati mbaya sikukikuta kilikuwa katika flash niliyomuazima Rafiki yangu *Kingu Gerald*,katika tafuta tafuta nikakuta mtihani wangu wa IR by Moham. Nyirabu umeandikwa Go and read: *politics among the Nations*:struggle of power and peace by Hans Morgenthau ,nilikidownload haraka nikaanza kukisoma ,yote mstari niliufikiria zaidi ni ule usemao *international politics is struggle for the power* [emoji15],nikaendelea kusoma nikakutana na maneno kuntu *state must think on and protect it's national interest*(nchi lazima ilinde maslahi ya taifa lake kwa namna yeyote )

All states within the system are the unitary rational actors
1.tend to pursue self interest.
2.Groups strive to attain as many resources as possible.,states strive to take wealth and being rich through another state by any means(relative gain)

kuwa mataifa ya nje yapo kulinda maslahi yao ,na hupambana kujipatia mali kupitia nchi zingine ambazo hazina nguvu.

Hii ilinishtua saana nikawaza tuliwahi tolewa mfano,Darasani kuhusu nchi ya Libya.

Kuwa mataifa ya nje yakiwa yanataka maslahi Fulani katika taifa fulani kukiwa na kikwazo ,labda viongozi,Rais aendani na wao humtafutia chokochoko aonekane mbaya ili machafuko(political chaos)yatokee ili wampindue na waweke Rais anaye endana na wao.

Saa 10:36 usiku,usingizi ulipungua kutaka kujua ,nini kuhusu Libya ,nikapata andiko mtandaoni linaitwa "Why was Ghaddaf overthrown"?

Haya yalikuwa ni kama mahojiano kati ya prof.Horace campel anayefundisha African America studies and political science. At Syracuse Univ.akihojiwa na Noor Paul Jay,(Editor).

Prof.Horace anasema ,Libya was stable African society in northern Africa.Libya wanted to reconstruct water resources, oil resources and financial resource for the Africans themselves and not foreign nations.

Ghaddaf alitaka rasilimali za afrika zitumiwe na waafrika wenyewe na sio nchi za nje.

Ghadafi alitaka kuanzisha "African monetary fund" ,kuanzisha African central bank",na kutumia sarafu moja Africa nzima hivyo kupunguza matumizi ya Euro na dollar,alitaka kushawishi nchi zote za umoja wa waarabu wataifishe makampuni yote ya mafuta ya kibepari yaliyo nchi za kiarabu.

Alitaka waache kutumia Dollar na Euro kama Reserve currency ,badala yake watumie African resources kama dhahabu (gold) kama Reserve currency.

Utawala wa Ghadafi ulikuwa mchungu ,na usionufaisha nchi za Magharibi,kilichofanyika ilikuwa ni kukuza chokochoko ,dhidi ya utawala wake .

Kilitengenezwa kikundi kikidhaminiwa na ufaransa ,ukisoma andiko la Bernard Henri Levy (BHL) spy journalist (muandishi mpelelezi) title *RIPPED FROM HILLARY'S EMAILS, FRENCH PLOT TO OVERTHROW GADDAF and help it's self to Libya's oil*

Mfaransa alikuwa anahitaji mafuta kupitia makampuni yake ,ila Ghadaf alionekana mgumu,hivyo kuzima National interest ya taifa la ufaransa.moja ya email iliyokamatwa ni Rais wa ufaransa Nicoles sarkozy akisema "we are going to fight to save dollars ,and Euro"

Kulianza kutumika vikundi vya watu wachache dhidi ya utawala wa Ghadaf na maandamano,Bayda,zintan,Alquba,Derna,na maandamano makuvwa ya 17,February 2011,wakiimba "the end of the regime" wakidai kuwa Gaddaf ni dikteta ,anaua watu wake wanaompinga,kikatengenezwa kikundi cha waasi kinaitwa NATIONAL TRANSITION COUNCIL (NTC),chini ya mwamvuli wa Rebels (waasi) wakiongozwa na mustafa Abdul Jalili,na Gen.Fatah Younis.

Kikundi cha intellegensia cha ufaransa ,kinaitwa GENERAL DIRECTORATE FOR EXTERNAL SECURITY (DGSE) ,kikaingia makubaliano na kikundi cha waasi Libya kipewe full support ,watalipwa fedha wazitakazo ,viongozi hawa wawili wa kundi la waasi NATIONAL TRANSITION COUNCIL , kwa lengo la kumtoa Ghadaf ili aingia kiongozi atakaye Linda maslahi yao,wakapewa silaha za kutosha kupambana na serikali yao (chini ya Ghadaf).hii inaitwa "Divide and Rule"

Pande zote walianza mapambano,Ghadaf akitumia jeshi lake alikuwa akishtumiwa na kuuwa watu wake "Ghadaf kills civilians" wakati wengi walikuwa wanauliwa na waasi.vyombo vya habari BBC,CNN zikaingia kazini kumchafua.

Baada ya kupata sababu , 17/march 2011 suala la Ghadaf likapelekwa UN ,idara ya UNSC united Nation security council,wakapitisha Resolutions kumpiga Ghadafi ,sababu anauwa watu wake.ili kwenda Linda raia.

Matokeo yake Ghadaf alipigwa,akauwawa.

Utawala ulioingia ulikuwa usio na vikwazo,mfaransa September 2011 alitoa report Imepata mafuta asilimia 35 kwa ajili ya makampuni yake kama TOTAL.

2013 ,Mfaransa akaanza kupata faida ya kifedha kutoka Gulf cooperation council, ilikuwa ni rahisi kuingia hata katika nchi zingine za kiarabu sababu kikwazo,hakipo tena ambaye ni Ghadaf.

Mfano,mmarekani ,muingereza wakapata nchi za kirafiki said Arabia,Qatar,United Arabs of Emirates hii ikawapa mwanya wa kujipanua na kupata rasilimali ya mafuta kirahisi kutoka kanda za nchi za kiarabu.

Saa 12:08 asubuhi nikapitiwa na usingizi ,ni kaota ndoto juu ya juu ya makampuni yanayosumbuliwa hapa Tanzania, yalipe kodi ,yalipe fedha tunazowadai,wazuie kusafirisha madini ,mchanga,,nikaota kuwa makampuni haya yanaanza kufirisika wakaanza kutafuta njia za kiintelejinsia dhidi ya Rais ,ili wafanye kama walivyofanya Libya .(DIVIDE AND RULE)

Nikashtuka kumbe ilikuwa Ndoto,hapo hapo nikasimama nikamsualia MH.TUNDULISU, Nikamuombea Dua.Mungu amjalie huko alipo.

WATANZANIA NAWAPENDA SAANA,NAIPENDA NCHI YANGU.

TUELEWE VITA TULIONAYO NI KUBWA SAANA NA NI PANA.

Abdul Nondo.
0659366125.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom