In CCM there are some great leaders, but (....)

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,427
Ndani ya CCM kuna viongozi wazuri lakini katika mazingira na jamii ya Kitaanzania. Ukienda katika level za kidunia ambapo sasa dunia inaunganishwa kuwa kama jumuia moja; wengi tutakubaliana kwamba bado tupo mbali kidogo na ni lazima kufanya kitu zaidi. Kwa mantiki hiyo,ni vyema kila mtu kujitahidi kuji upgrade na kuwa bora zaidi kimtizamo na kimatendo.

Watanzania tuna tabia ya kukatishana tamaa. Ni kweli mtu anaweza kukosea lakini badala ya kumkatisha tamaa, inafaa kumshauri mbadala wa kufanya kwani kila mmoja akimkatisha mwenzake tamaa matokeo yake ni kila mmoja kujikuta anapoteza matumaini ya anachofanya. kadhalika mtu unapokuwa umekata tamaa unajikuta kwenye hali inayokufanya kushindwa kutumia uwezo ulionao kikamilifu na kwa usahihi kuleta matokeo bora.Matokeo ya haya yote tunajikuta wote hapati mafanikio ya kutosha kwa wakati.Msikubali kukatishwa tamaa na mtu.

Kitendo cha ninyi kufanikiwa kuwa Chama tawala ni fursa ya kipekee ya kila mmoja wenu kutumia uwezo uliopo ndani yake kufanya kitu kikubwa sana kwa watu wa nchi hii. Mnauwezo mkubwa ndani yenu ambao bado hamjautumia na mkiutumia kikamilifu mtabadili vitu vingi kwenye nchi hii. Msikubali kukata tamaa kwa sababu yoyote ile. Ninyi ndio viongozi, hakikisheni kila siku ipitayo kila mmoja kwa mazingira na nafasi yake anajitahidi kufanya kitu bora kuzidi cha siku ya kabla.

Ikitokea leo umefanya makosa; Tathmini makosa uliyoyafanya leo na hakikisha kwamba kesho hayajitokezi tena na fanya hivyo kila siku na matokeo mazuri yatapatikana. Fanya hivyo ukifiria hatima ya kizazi cha leo na kesho huku ukitanguliza dhamira njema na mambo mengine yote yatakwenda sawa.

Ubora hauna mipaka, kwa hiyo unaweza kuwa bora miongoni mwa watu kadhaa lakini katika scope pana zaidi, ukawa bado unahitajika kufanya kitu zaidi. Lakini ili kufanikisha hili, ni muhimu pia kujitahidi kujifunza kitu kipya kila siku kwani ili uwe kiongozi bora ni lazima pia uwe mwanafunzi.

Fikirieni kutumia vipawa mlivyonavyo to the maximum kuwafanya wengene wawe na furaha na kupitia misingi wa KARMA; sio wale mnaowahudumia tu ambao watakuwa na furaha bali miale ya mwanga wa furaha hiyo itaakisi juu ya nyuso zenu na mtajikuta mkiwa na maisha yenye furaha kuliko hapo kabla kwa upande mmoja, na nchi ikisogea kwenye hatua nzuri zaidi kwa upande mwingine.
 
Ujasiri wa kusimamia ukweli haupo mioyoni mwa viongozi wa Tanzania. Si ccm tu hata upinzani.
 
Ujasiri wa kusimamia ukweli haupo mioyoni mwa viongozi wa Tanzania. Si ccm tu hata upinzani.
Tanzania tuna tatizo la watu. Tuna watu wengi ambao namna wanavyofikiri kuna changamoto kidogo. Hii ndio jamii yetu au ndivyo tulivyo. Hata hivyo tunaweza kubadilika hata kama ni taratibu.
 
Tanzania tuna tatizo la watu. Tuna watu wengi ambao namna wanafofikiri kuna changamoto kidogo. Hii ndio jamii yetu au ndivyo tulivyo. Hata hivyo tunaweza kubadilika hata kama ni taratibu.
Mabadiliko lazima yaanzie ngazi ya familia. Usitegemee kuwa na jamii au taifa lenye uadilifu kwa familia za ovyo ovyo zisizo na maadili.
 
Washauri pia ile tabia ya kutoka na mabox ya kura kisha kwenda kuyajaza na kuyarudisha yakiwa na kura yanawaharibia mno.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom