Immigration KIA

Easymutant

R I P
Jun 3, 2010
2,564
1,129
kwa siku nyingi sana nimekuwa nikisikia hawa ma officer walioaminiwa na serikali ya CCM kusimamia wanaoingia nchini kwetu lakini kwa rushwa hawa wajamaa ni zaidi ya kupimwa DNA, wazungu wanaingia wanagongea fake na hawapewi receipt na wanadai $100 kwa kila aingiaye sasa kimbembe kikaja dereva aliyewapokea wageni akauliza je mmepewa receipt wazungu hapana! Akawaambia nendeni mkadai receipt kwani wakati wa kutoka mtasumbuliwa wazungu wakawa wekundu wakarudi kudai receip just imagine a group of 26pple, sijajua nini kiliendelea but alitoka officer mmoja na kuuliza nani dereva kiongozi wa hawa wageni jamaa kasema mimi... Kunatatizo??? Hapo ndipo kichekesho kwanza wakamtisha uzuri jamaa hatishiki akajibu nanukuu "PELEKENI UPUUZI WENU MSIFABYE SISI WEHU KAMA NINY TOENI RISIT NI HAKI YAO NA KWA KUW MMEKUJA KUTUANGALIA MARA MBILI MBILI ITABIDI NA RISIT TUZITOE KOPI ILI TUONE KAMA NI VILE VITABU MLIVYOIBA" wakaenda zao ndani wazungu wakapewa risiti but Kwa nn hawa watu walazimishwe kutoa risiti kwa wageni??? Huyu ni dereva mmoja ambaye kaamua kukomaa nao je how many hawapewi risit kwa kutojua?
 
Nendeni kule mji wa Bomang'ombe muone maMansion yao. Serikali kimya!! Kila mmoja serikalini anakula urefu wa kamba yake. Heri wenye kamba ndefu kama . . . . Wanakula dunia nzima!
 
Hao ndio tatizo jingine katika hii nchi kazi kutujazia wageni tu humu ndani, sisi wenye hatutoshi bado wao wanajazaa watu kuja kutuibia rasilimali zetu
 
Hao ndio tatizo jingine katika hii nchi kazi kutujazia wageni tu humu ndani, sisi wenye hatutoshi bado wao wanajazaa watu kuja kutuibia rasilimali zetu

sasa nyie mlitakaje? Kama umewaona wakamate ni jukumu la kila raia kuilinda Tanzania, na la wanyama 116 je? JAIRO na wenzake, Rostam vp? VASCO da Gama suti kwa Rasimali madini, Ardhi nk za nchi, pesa za madeni ya EPA? Mabilioni ya pesa walipwayo wabunge Bungeni kama Posho ikiwa mishahara yao mikubwa na wanaozikusanya kupewa Mishahara ya kutumia isimalize mwezi hadi wanaishi kwa madeni? Sukari, mafuta bei juu na maisha magumu je tunategemea wao waishi kuwakusanyia mafisadi pesa ili wazipeleke Kwenye Kampeni na KUKESHA ANGANI KAMA BUNDI AMA JUMBO JET,FLY EMIRATES kila siku? Hayo imeyaendekeza serikali inayowalipa Usalama wa Taifa Pesa nyingi ikiwa Wanaozikusanya za kuwalipa mishahara mikubwa Usalama wa Taifa ambao kazi yao kubwa kuchakachua matokeo ili kukiwezesha chama magamba kubakia madarakani na wao kulipwa mishahara ya kukosa hata mafuta ya taa jioni kwa mwezi mzima. Kama mzungu ndie kaliwa ulitaka ziliwe zako, mbona wanaokula pesa za wananchi na kutushindisha na kutulaza Njaa hatusemi na kusababisha Mgawo wa giza (TANZAGIZA) Migodi inahodhiwa na wageni sisi kulala njaa tunafurahia, kama vijana wa KIA Kuna wanachokifaidi kweli waache wafaidi wao kwanza sisi Baadae. Haiwezekani akina Riz wakamiliki Mabilioni peke yao na waambata wa jeshi pia. Je zingekomaliwa hizo tukagawana tungepata ngapi ngapi mimi na wewe? Kula uliwe!
 
ukitaka kuona makubwa nenda dar uwanja wa ndege utalia na kusaga meno....waarabu wanaingia na kutoka kama kwao nchii hii.
 
Nijuavyo mimi risit ni haki ya yeyote atoaye malipo. Lakini iliwahi nikumba hii pia pale Sirali. Mgeni wangu alitozwa viza pale na hatukupewa risiti. tulipohoji, nadhani yule ndo alikuwa mkuu wao alituchukua pembeni na kudai wana waraka toka kwa Kamishna wao ukiwataka kutokuzitoa hizo risiti. tuliondoka kwa kutotaka kuendeleza malumbano.
 
sasa nyie mlitakaje? Kama umewaona wakamate ni jukumu la kila raia kuilinda Tanzania, na la wanyama 116 je? JAIRO na wenzake, Rostam vp? VASCO da Gama suti kwa Rasimali madini, Ardhi nk za nchi, pesa za madeni ya EPA? Mabilioni ya pesa walipwayo wabunge Bungeni kama Posho ikiwa mishahara yao mikubwa na wanaozikusanya kupewa Mishahara ya kutumia isimalize mwezi hadi wanaishi kwa madeni? Sukari, mafuta bei juu na maisha magumu je tunategemea wao waishi kuwakusanyia mafisadi pesa ili wazipeleke Kwenye Kampeni na KUKESHA ANGANI KAMA BUNDI AMA JUMBO JET,FLY EMIRATES kila siku? Hayo imeyaendekeza serikali inayowalipa Usalama wa Taifa Pesa nyingi ikiwa Wanaozikusanya za kuwalipa mishahara mikubwa Usalama wa Taifa ambao kazi yao kubwa kuchakachua matokeo ili kukiwezesha chama magamba kubakia madarakani na wao kulipwa mishahara ya kukosa hata mafuta ya taa jioni kwa mwezi mzima. Kama mzungu ndie kaliwa ulitaka ziliwe zako, mbona wanaokula pesa za wananchi na kutushindisha na kutulaza Njaa hatusemi na kusababisha Mgawo wa giza (TANZAGIZA) Migodi inahodhiwa na wageni sisi kulala njaa tunafurahia, kama vijana wa KIA Kuna wanachokifaidi kweli waache wafaidi wao kwanza sisi Baadae. Haiwezekani akina Riz wakamiliki Mabilioni peke yao na waambata wa jeshi pia. Je zingekomaliwa hizo tukagawana tungepata ngapi ngapi mimi na wewe? Kula uliwe!

Sijajua wakati unajibu ulikuwa umekalia nini !! Ila unajazba sana nahisi nawe mgao unakuhusu mie nimesema tu jombaaa ..eti wakiliwa wazungu inakuhusu nini?? You must b in toilet...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom