Imetokea mtaani kwetu...mzee anaugua presha sasa.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imetokea mtaani kwetu...mzee anaugua presha sasa..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Mar 20, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Akijiamni kuwa haitatokea siku mambo yakawa hadharani, Mzee ambae mtaani tunamheshimu hali yake ni mbaya sana, presha inamsumbua. Kisa alikuwa na nyumba ndogo binti wa staili ya kuitwa mwanafunzi (sidanganyiki), alimpangia chumba na kuzaa nae kwa siri aliendelea kutoa huduma.

  Kumbe wakati wakila raha, wakati fulani binti alichukua namba ya simu ambayo Mzee aliiandika "home" sammbamba na simu ya mzee huyu wa makamo.

  Wiki tatu zilizopita, Mzee alikuwa amesafiri kikazi nje ya nchi na hakuweza kumwaga binti (nyumba ndogo kuwa atasafiri). Kutokana na binti kusumbuliwa na matatizo ya kulea mtoto na matumizi na kodi ya nyumba, alipoona anashindwa kumpata mzee, aliamua kupiga namba ambayo aliipata katika simu ya mzee siku za nyuma ile imeandikwa "home". Katika kupiga, mama mwenye nyumba, mke wa ndoa wa mzee anapokea simu na kuuliza wewe nani, binti hakuwa na ajizi akajitambulisha mimi ni mchumba wake mzee fulani, mama akashtuka lakini hakutaka makeke, akamuuliza upo wapi, binti akajibu alipo, mama akasema basi mimi ni dada yake, binti pasipo uelewa akajibu aliwahi kuniambia anaishi na watoto na dada zake tu na mkewe wa ndoa waliachana zamani sana.

  Mama akamwambia basi kama unamtafuta, jamaa amesafiri nje ya nchi, ila kama unashida yeyote tunaweza kuoana tu hapana shaka..binti kwa kujua yote sawa, akasema basi ntakutafuta. Kesho yake wakapanga kuonana sehemu, mama akaenda na mdogo wake, kufika wakamkuta binti kawahi, stori, storiiii, binti akaeleza yote kuwa anatembea na mzee muda mrefu, wanamtoto mmoja wa kiume, na mzee alimtenganisha na mpenzi wake ambae walikuwa wote chuoni na waliahidiana kufunga ndoa. Ila mzee walisababisah watengane baada ya siku moja mpenzi wa huyi binti kumfumamina binti na mzee. Binti akaeleza pia kuwa walishawahi kutembelea ameneo wanayoishi mzee na dada zake ila ilikuwa usiku. Mama mwenye ndoa yake akavumilia tu...baada ya maongezi hayo akamtoa binti na vijisenti kidogo vya matumizi na akamwambia akirejea (mzee) atamjulisha.

  Siku kama mbili baadae mzee akarejea, mama akasubiri mapka jumapili iliyofuata, mzee yeye ni mtumishi mzuri wa kristo (mzee wa kanisa), siku hiyo ya jumapili walienda kanisani, baada ya kutoka kanisani mama anamwomba Baba Paroko waambatane nae nyumbani, wakati huo mzee alikuwa akihesabu sadaka kanisani...kabla ya hapo mama akampigia simu yule binti, akamwambia mzee kaja njoo, ukifika sehemu fulani panda bodaboda..kisha uliza kwa Mzee fulani watakuelekeza. Binti akasema nakuja fasta kwa kuwa sipo mbali na mitaa hiyo.

  Mama na Paroko walipofika nyumbani, muda mchache mzee anaingia akitokea kanisani, akashangaa kidogo kumwona Paroko, lakini hakujali sana kwa kuwa mama nae ni mzee wa kanisa hivyo akidhani ni maswala ya maombezi tu yatafuata na mtumishi huyo wa kiristu.
  Wakiwa wanajiandaa kwa chakula, mara mlango ukagonjwa, ghafla binti anaingia kwa mbwembwe asijuie hili wala lile, anashtuka kumwona Paroko na Mzee, anamsalimia mzee kwa tabasamu, mzee nae anashtuka sana ...Mama mwenye nyumba anahamaki, anamwomba binti akae chini, mzee anataka kusimama, mama anamkalisha chini (unakwenda wapi??)..Paroko anashangaa...ghafla mama anamwomba samahani Paroko na kumwambia binti "mimi ndie mke wa ndoa wa huyu Mzee hapa..haya eleza yote uliyonieleza siku ile.." Binti anaogopa sana na kuanza kueleza yote..huku akitoa ,machozi....Baada ya kuhitimisha..Paroko anataka kuingilia kati kuhusu "utaratibu"....mama anamuuliza "haya mzee ipoje..wewe jitu zima na wajukuu unaenda kuzaa na binti mdogo kama huyu??...Mzee anajiumauma ..ghafla anataka kunyanyumka ..anapamua mdomo lakini anashindwa ..anaanguka chini anazimia..(Presha imepanda).

  Wiki sasa mzee hali yake ni mbaya, Mama anauguza kwa shingo upande..Hali ya mzee inachangiwa na fedheha iliyoipata mbele ya Paroko na watoto wake. Bado yu hoi kwa Presha...Binti aliruhusiwa kuondoka bila kudhuriwa ..mama alieleza kuwa binti hana kosa lolote na akamuonya asithibutu kuwaamimi wazee wa umri ule kuwa hawana watoto au ndo.
   
 2. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  nzuri lakini umetunga,haijatokea kweli.....
   
 3. k

  kisukari JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,766
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  nampa big up huyo mama,wazee kama hao,wapo wengi tu,kujifanya dini imewaingia huku kuendelea kuwadangawa mabinti.kwa nini hawaridhiki?
   
 4. mbota

  mbota JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 745
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 60
  umejitahidi waweza kuandika kitabu na ukatoka pia
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kuepuka haya ndio maana nataka kuengeza. Gari bovu huhitaji gari zima kubururwa!
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mwenye njaa mimi unafikiri utajuwa kiasi gani imenikamata? Na uliona wapi kitu kubeba zaidi ya uwezo wake?
   
 7. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  huyo mzee akifa ataachiwa mzigo. Asume mzee ndo mtoaji wa mlo na kila kitu. Walitakiwa walishane pembeni wakishindwana ndo wayapeleke kwa wengine.
   
 8. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Si useme kwa nini unadhani ametunga hii habari kama unasababu kweli au unaishi mtaa mmoja na mwandishi.

  Ila mie nimesikia yanayotokea ni zaidi ya haya ya ustaarabu.
   
 9. Twande

  Twande JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lol. .
   
 10. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Yaweza kuwa kweli.Nakumbuka kesi moja miaka ya nyuma ambapo bi mkubwa baada ya kusikia nyumba ndogo ya mzee imejifungua alifunga safari NA wanae wakapeleka zawadi NA nguo kwa mzazi.Ulitokea mshtuko WA ajabu eneo la tukio.Yanatokea hay a.
   
 11. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Haya mambo siyo ya kutunga dadangu, hii ni habari ambayo imetokea..sikuwahai kuwaletea nyingine hii:

  Yupo Mwanaume Mwnigine mtu mzima mtaani kwetupia yalimkuta, alimtongoza mpwa wa Rafiki yake, anawa anamsumbua kwenye simu sana, binti alisave jina lake halisi (mzee mwa....) sikumoja binti aliacha simu mezani akiwa jikoni mzee akapiga, shangazi yake Binti akaiona namba inaita kwa jina la Mzee.
  Akamwita Binti, akamuuliza imekuwaje uwe na namba ya mzee huyu...(..) anakutafutia nini.."? Binti kwa hofu anaeleza kuwa aalinitongoza siku moja alipokuja hapa nyimbani, akaomba namba yangu akani bipu, nikaisave ili akipiga nisipokee...
  Shangazi akahoji sana hili....lakini baadae akiwa amehakikishiwa kuwa binti hakuwahi kutembea na huyo mzee, shangazi akaona ni vyema aandea mtego wa kumkamata huyo mzee, akaenda kumweleza Mkuwe kuwa Mume wake anamtaka Mpwa wao. Mke akawa amehamaki lakini mwenzie akamsihi waweze kuthibitisha hilo..wakamweleza yule Binti am bipu mzee, amweleze ana hamu ya kitimoto, wakutane mahali ili amnunulie, mara mzee alipoona beeping akaruka hewani, Binti alipewa maelekezo aweke simu yake katika Spika za juu (Loud Speaker) . Mzee akasikika upande wa pili "Vipi we mtoto kimya sana.. unasemaje, mimi nakutaka unanidengulia." mkwewe akiwa anamsikia mzee akibwabwaja bila kujua anategwa..Binti anampa shida yake kama alivyoelekezwa na Mke wa Mzee , "Naomba kama vipi tukutane leo, nina hamu ya Kitimoto.." Mzee hakuwa na ajizi anamwelekeza wakutane saa kumi jioni katika eneo ambalo ni maarufu kwa Kitimoto na pana gesti pia. ..mzee akaomba pale pale .."sasa vipi leo si utanipa hiyo kitu mama??" ..binti akaelekezwa kwa ishara na wale akina mama amjibu ndio ' binti akajibu tutaangalia".

  Jioni ya saa tisa binti akiwa amaembatana na akina mama wale (Mke wa Mzee na Shangazi yake Binti) wakaenda eneo walilopanga kukutana. Binti akaka eneo la wazi,wale akina mama wakajificha ila wakamwelekeza wakimaliza kitimoto amobe waingie gesti chumbani, wakifika awatumie ujumbe (Sms) wapo chumba gani,...muda mzee alipofika anakaa na binti kwa maongezi marefu, na baada ya kutandika K' MOOO giza liliingia wakaanza kushikana, mzee akaomba waningie gesti..wakaingia. Kufika chumbani, binti akaomba kwenda chooni akatuma sms (Tupo Chumba kimeandikwa "Marangu" ..akarejea. Mzee akiwa amevua, mara akasikia sauti za mhudumu akibisha na watu kwenye varanda, ghafla mlango wake ukafunguliwa, kumbe mhudumu mmoja alichoropoka..akamwambia mzee unafumaniwa kimbia...Mzee akakurupuka na chupi, yule muudumu akamwelekeza chumba wanacholala wahudumu, akaingia huko ..mhudumu akampa suluali ya Jeans na fulana na kumtaka akimbie kupitia mlango wa nyuma (dharura)...mzee akakimbilia huko ambaklo kuna kolongo, pori kubwa lenye miiba ..akatokea barabara kuu ...

  Wale akina mama walifanikiwa kumsukuma mhudumu yule mwaingie, wakatinga chumba "Marangu" na kumkuta binti amevua blauzi yake akiwa na blazia tu...wakapiga kelele wapi mzee "Mwa...."
  Binti akasema amekurupuka, wakatoka nje kumtafuta, kumbe mzee alikwisha chukua bajaji, akatimkia home, akiwa nyumbani ile anaingia tu anakutana na kijana wake, anamuuliza baba mbona umevaa jeans tena hjaikutoshi na pia sio kawaida yako?..Mzee anamjibu acha tu..nitakueleza ..anakimbilia chumbani na kuchenji nguo..Mara dakika chache wale kina mama wanaingia ndani wakiwa na nguo za mzee alizoacha geti na binti ..wanajaza watu nyumbani ..Mzee anakana mzala huo lakini baadae mwanae anamuumbua, "Baba ndio nimekuona umekuja na Jeans" mzee akapaki kinywa wazi, baada ya tafrani kubwa na mama kuomba talaka, ndugiu walifika, binti akaulizwa kulikoni, akamwaga mpunga wote ...Mzee kwa aibu akaona ni busara kukiri kuwa alikuwa "akimtania tu binti ...hakuwa serious...wamsamehe kwa yote..Ilimchukua Mkewe mwezi mzima na sasa amemsamehe...
   
 12. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Duuh umenikumbusha tu~vitabu twa MILLS&BOONS...
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mhhh haya mambo haya ni noma
  yako mtaani na sio story za kutunga
  Wazee hawazeeki kabisa
   
 14. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hakukuwa na sababu ya kumwita paroko na mambo mengine wangeongea tu ili wajue wanamsaidiaje huyo binti. Maana kama kutokea imeshatokea na kosa ni kosa. Hapo mzee akifa itam cost yeye na yule binti naye na mtoto watakuwa na maisha magumu sana. Namuombea apone haraka, na ajue kuwasiliana na nyumba ndogo maana ilijue mzee kaitosa ndo maana ikapapalika.
   
 15. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Yani baadhi ya wazee wa siku hizi bana sijui wakoje,
  Wanatumia sana miavuli ya dini au nyadhifa zao kuhadaa wasichana!
  Hebu ona sasa atakufa mapema na presha kwa ubazazi wake!!!

  Natama huyo mama awe japo na roho ya huruma kwa huyo binti amsaidie tu kulea japo huyo mtoto asiyekua na hatia!!
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Lakini upande mwingine
  Binti unadanganywa na mzee kuwa ameachana na mkewe miaka kadhaa
  Umri unauona umesogea kabisa anakaribia saa kumi na mbili
  Hujiulizi huyu mzee ina maana hata kama alitengana na mkewe si atakuwa na watoto wakubwa
  Je watotowa huyo mzee si watakuwa sawa na huyo binti
  Ndio hata kama alikuambia anakaa na dada zake na watoto si ungefanya uchunguzi kabla ya kuingia kwenye mtego wake wa kuzaa nae
  Na mzee kama huyo ambaye unaona kabisa hakuna uwezekano wa kuolewa nae si unajua tuu hapa ni wa muda kwa nini ujiingize kwenye kumzalia mtoto ambaye kwa huyo mzee ni mjukuu wala sio mtoto ambaye maisha iyake yatakuwa ya shida maana babu (baba) yake ataondoka duniani mapema amwache akiwa bado mdogo
  Ahhh kuna mengi sana ya kujiuliza japo tunawalaumu hao wazee ila wasichana nao wana upande wao ambao wanatakiwa kuwa makini sana kabla ya kuingia kwenye mitego ya hao wanaoitwa sugar daddy tena mpaka wanakubali kuzaa nao watoto
   
 17. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu, sio mabinti zetu wote hata waliosoma wanaupeo wa kiona mbali. Maisha ya kitanzania kwa sasa wanawake wengi wanaishi kama ndege waishio mwituni, anafanya yote leo hajui kesho ipoje, hajali hata akisikia hataki kuamini. Wengi maisha yanabana, anaweza kutembea hata na mwanda wazimu ilimaradin tu apate chake kinywani, Ukitaka kuona kuwa pengine kina dada wengi hawana fikra za mbali, angalia wasanii kama akina " Ubaya Chepeto" ..(mtu yeyote anaweza kumpitia, atampa haijalishi ni nani, ilimradi tu aweze kumkidhisha mahitaji yake kwa siku. Wazee ndio wanaoaminika kwa vibinti vidogo kuliko vijana...

   
Loading...