Imetokea kweli, japo bado siamini...

Kupenda mno nako huwa kunageuka kero kwa mpendwaji.
 
Hongera sana my wee.jipenzi hilo ,jimwage mamiii kwa raha zako.maisha yenyewe ndo haya haya.we only live once yu know!so furahi mamii.let love lead the way BAK payia wifi ya mimi wimbo wa TLC red light special.
Enjoy sakapal
Asante wifi yangu naelea elea tuu kama mbayuwayu hata sioni tofauti ya mchana na usiku.
 
he he heeee, nasikia harufu ya mwanachama mpya.....
karibu kwenye chama chetu cha mateja....
cc; BAK, snowhite, Arushaone, Nicas Mtei........

FP mie nina wasiwasi na sakapal. Huyu kama vile ni experienced member ages ago.

Vingenevyo atakuwa anawaingiza chaka na threads zake.

Ina maana kesha divorce? Rejea threads zake za nyuma.

Ipo moja ya jirani kuomba lift kwenye kibabaji chake na mumewe mpaka kumnyima raha ya kuongea na mumewe.

Kwa hiyo sasa watakuwa watatu au wanne kwenye kile kibabaji chao?

Kama ni hivyo, namwonea huruma yule jirani aliyekuwa akiwaomba lift kila asubuhi unless awe ni yeye anayesifiwa kwenye huu uzi.

Pia rejea thread yake ya kutaka ushauri wa kumfanyia mumewe surprise siku ya birthday yake.

Pia atamfanyia birthday surprise huyu mpya kama alivyotaka kumfanyia mume wake?

I mean kumchukua kazini jioni na kumpeleka restaurant wakapate dinner for two or probably itakuwa for three now?

Halafu abook hotel (not guest house) wakalale huko (threesome?) baada ya kupata dinner na kuamkia hapo next day, wapate break fast then awapeleke job?

NAJUA YUKO SERIOUS MATANI NIACHE KWANI ANA MUDA MCHACHE WA KUFANYA HAYA.

cc. BAK, Paloma, Mentor, Roulette, Mwanaweja, SURUMA, Kipipi, Blue G waliompa likes
 
huyo sie muhusika ajafika,ila aliniambia amemtuma mjumbe aje akwambie atakuja mda si mrefu,sa nashangaa mjumbe ndo kawa soulmate tena,au kwasababu alijiwekea marashi ya muhusika? hold a litle longer he will be there.
 
du! rafiki una kumbukumbu!
mi hayo yooooteeee yalijificha, lol!
ngoja sakapal aje atufafanulie ipi alikuwa anatuzuga na ipi ya kweli.
 
Last edited by a moderator:
du! rafiki una kumbukumbu!
mi hayo yooooteeee yalijificha, lol!
ngoja sakapal aje atufafanulie ipi alikuwa anatuzuga na ipi ya kweli.

Nakumbuka watu tulijipinda hapa kutoa maushauri ya kumpa mumewe masuprasi kumbe tunapoteza muda.

Ndo maana siku hizi niko very caution kutoa ushauri kwenye hili jukwaa.

Majority ya stories ni za kutunga au ni fantasies za watu; they wish wafanye au wafanyie but they can't.

cc nyumba kubwa, King'asti Kaunga
 
umenishika masikio mkuu.....
hapa ngoja niwaongeze pia na washauri wengine gfsonwin na snowhite...
kweli inaumiza sana mtu unajipinda kutoa maushauri kumbe mambo siyo ya kweli.
kama unamwombea ushauri rafiki yako ni bora ikawa wazi, ila kama ni hapo zamani za kale........:A S 39:!
sasa watatukosesha ushauri sisi ambao kweli tunauhitaji
 
Last edited by a moderator:
Reactions: EMT

Bora ku-hypothesize story kuliko kuifanya ni ya kwako. Najua wapo watakaonipinga kwa hili kama ilivyowahi kutokea huko nyuma.

Lakini siku sakapal na wengine wanaofanya hivyo wakiwa na shida ya ukweli na kutaka ushauri wanaweza kuchukuliwa ni wale wale tuu wa threads za kutunga.

Pia mtu mwingine anaweza kuwa na tatizo la ukweli na kuomba ushauri lakini mtu akadhani ni wale wale kama sakapal.

The overall impact ni kwamba people will refrain from giving advice, particularly where it is needed.
 
nakubaliana kabisa nawe....
bahati mbaya hilo linaweza tokea kwa mtu ambaye ni ukweli kabisa anahitaji msaada, watu wakapuuzia, halafu dhana nzima ya kupeana ushauri ikapotea.
sijui tufanyeje kuhusu hili?
cc. Dark City, BAK, The Boss, mwaJ, Kaunga, AshaDii na wengine
 
Last edited by a moderator:

Sijui maana unawezakuta wanaofanya hivyo ni wagonjwa pia bila wao wenyewe kujijua.

Inawezekana mtu ana-suffer from attention seeking disorder ambayo ni kawaida lakini inaweza pia kumletea matatizo mhusika.

Wengine ni fantasies tuu or they wish things were they way they wrote, nk.

The best way ni kujaribu kuweka kumbukukumbu kichwani hasa kwenye threads unazochangia.

Ni ngumu lakini tujijengee tabia ka kujiwekea kumbukumbu ya mambo tunayoandika hapa.

Unawezakuta mtu leo anaandika hivi lakini next week anaandika completely the opposite.

Hii inatokea kwa mjukwaa mengi tuu na siyo MMU.

Kwa ujumla stories nyingi hapa JF ambazo huwa zinaandikwa kama za kweli vile ni za kutunga.
 
ha haaa, utaniingiza kwenye kundi la kupiga stori kwenye uzi za watu na siyo kutoa ushauri....
yaani tunavyojipindaga, lol!
haki ya kweli wanatuweza.....
kuna usemi wanasemaga ukiwa....... usiwe msahaulifu, unaukumbuka?
kaazi kweli kweli...
mi nilishamkaribisha shosti sakapal kwenye chama, sasa sijui ni-withdraw karibu yangu! anyway, yeye ndo anaujua ukweli
 
Last edited by a moderator:

Yea, usemi unasema ukiwa mwongo usiwe msahaulifu.

Mtu anaweza kusumbuliwa na usahaulifu au uongo au vyote viwili.

Kanuni ya kuwa mkweli inasema kuwa ukiwa mwongo usiwe msahaulifu na ukiwa msahaulifu usiwe mwongo.

Ukweli ni kwamba ukiwa na sifa ya uongo na usahaulifu ni rahisi kusutwa na kukosa uaminifu.

Lakini watu wanakuwa waongo kwa sababu wanajua sie wabongo tunasahau mambo ya nyuma mapema mno.
 
uuwwwiiii, huo ndo ugonjwa wangu.....
yaani nikikukopesha huwa hadi uone huruma unirudishie....
wakati mwingine naweza kumbuka kuna mtu nilimkopesha ila hata sijui shilingi ngapi!
baada ya kulizwa saaaana sasa naandika na mtu hachukui kitu changu kabla hajasign kwenye kitabu changu.
 
Reactions: EMT

Generali Ulimwengu alishawahi kuandika kuwa usahaulifu ni silaha ya mwonevu.

Kwa hiyo, kama kusahau ni ugonjwa wako, utakuwa unaonewa sana.

Aisee nitakuwa nakuja kukopa kwako kila mara.

Siwezi kusema nina memory ya kukumbuka kila kitu.

Kuna mambo mengi sana yanatokea kila siku ambayo ni vigumu kuyakumbuka yote.

It is OK kusahau. Lakini ukisahahu too much inaweza kuwa ni ugonjwa aka dementia

Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha tusahau mambo mapema.

Lakini nafikiri sie tunaongoza kwa "motivated forgeting". lol.
 

Ndio maana mie mara nyingi ni kusoma uzi na ushauri wa watu tu baasi! Napata mawili matatu ya kujifunza kisha napita zangu kimyaaaa!
 
Ndio maana mie mara nyingi ni kusoma uzi na ushauri wa watu tu baasi! Napata mawili matatu ya kujifunza kisha napita zangu kimyaaaa!
ungekuwa unanitonya basi rafiki......
nini tunaacha tunaumiza vidole kwa makitu yasiyo halisi?
ila ukiona nalia ujue ya ukweli rafiki, uwe unanipa ushauri, sawa?
cc. EMT
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…