Imenigusa sana

Kipindi hiki vyombo vyetu vya ulinzi vimejitahidi sana tena sana!

Wakati msafara uliobeba mwili wa mpendwa wetu Jpm ukipita maeneo ya mkwajuni kuelekea magomeni mapipa,

Niliona Police wakiwasogeza wananchi walioingia barabarani na kuzuia msafara, kwanjia ya ustaarabu sana, waliwaondoa barabarani polepole bila kuwasukuma wala kuwaumiza, kiustaarabu na kiungwana sana mpaka nikashangaa!

Hapa tena naona mwanajeshi military police amembeba mlemavu wa miguu ili nae aweze kumuaga aliyekuwa Rais wake mpendwa Jpm. Kweli majeshi yetu yamepiga hatua kubwa sana! Nijambo jema la kupongeza!

Niwape kongole sana kwao!


Jpm

Apumzike kwa Amani,

Amina!
 
Umeyasema yote yaliyokua Moyoni mwangu.

Kongole kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…