Imei ya simu imefutika..

Imei ya simu imefutika..

prumpeti

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
1,023
Reaction score
2,315
Habari za muda huu watu wa Tech!
Moja kwa moja kwenye mada natumia simu aina ya Note8 ya line mbili kwa muda wa miaka miwili sasa ila leo jioni nilibadilisha line two kutoa voda na kuweka Airtel ikawa inaandika emergency services nilipojaribu kuangalia imei nikakuta moja imefutika zimebaki 00000000000 ila line one IPO sawa hii imekaaje na nini ufumbuzi wa tatizo?
 
unaweza kuona hapo
20221026_212318.jpg
 
Fanya factory reset, lakini kabla ya hivyo ubackup data zako kwanza...
 
  • Piga *#06# kama imei inasoma '000000'
  • Piga #197328640# au *##197328640#*#
  • Chagua No. 6 au 5
  • Chagua FTM, chagua No. 1, kama iko 'on' weka 'off'
  • Zima simu yako, washa tena na uangalie kama Imei yako imerudi
 
Kipengele cha pili code inakataa kujiandika, anza na star, pale kwenye au kati ya ## weka star
 
Imei imecorrupt, hakuna namna ya kurekebisha zaidi ya kuinstall certfile mpya. Nimeshakutana na hizi kesi awamu kadhaa, humu JF khalfan56 anapiga hizi mishe, kumbuka kubadili IMEI ni kosa kwa sheria za sasa za TCRA. Kwahiyo nenda kwa mtu unayemuamini. Mimi nimekutajia huyo hapo kwa hapa Jf.
 
Habari za muda huu watu wa Tech!
Moja kwa moja kwenye mada natumia simu aina ya Note8 ya line mbili kwa muda wa miaka miwili sasa ila leo jion nilibadilisha line two kutoa voda na kuweka airtel ikawa inaandika emergency services nilipojaribu kuangalia imei nikakuta moja imefutika zimebaki 00000000000 ila line one IPO sawa hii imekaaje na nini ufumbuzi wa tatizo??
Omba IMEI namba kwenye mtandao wa simu wowote utapewa kama ni tigo au voda kule kwenye dashboard yao inaonekana Nina experience na hili jambo.
 
Unaombaje maana pia huwa inatokea ukiflash simu za rooted
 
Laini uliyoweka kwenye simu hiyo mfano ni Tigo,unaenda tigo shop unajieleza vizuri wao watakuomba hiyo namba ya simu iliyokuwa ina kaa ndani ya hiyo simu wao wakifutalia tu wanaona.

Nasema hivi kwa sababu nilikuwa kwenye Telecom company kwa miaka kadhaa huwa ni kitu kirahisi tu.

Tena kwenye dashboard yao Kule mpaka aina ya simu uliyonayo inaonyesha.
 
Mkuu kwamba ukiomba wao wanaweza kui insert moja kwa moja au vipi??
 
Hiyo ya Ku insert sijawahi kukutana nayo lakini kama ni shida ya IMEI uzione tu huko kwele Telecom company wanakupa.
 
Mimi tatizo ni errors yani imefutika hivyo line haiwezi kusoma
 
Daaah hii ni case mpya kwangu ...anyway wataalam msaidie huyu mwamba nini cha kufanya.

Pole sana mkuu.
 
Kama upo na box la simu nenda nalo kwa fundi wa software ana andika upya hiyo imei sababu mabix huwa yanakuwa na imei au kwenye hiyo simu huwa zipo kwenye stika au maandishi yaliyo nyuma ya simu chini

Kumbuka kurudisha imei ile ile iliyo corupt kwenye simu husika sio kosa kisheria ila kosa ni kubadilisha imei ya simu A kuiweka kwenye simu B
 
Kurejesha IMEI ile ile ni kipengele mkuu
 
Kama upo na box la simu nenda nalo kwa fundi wa software ana andika upya hiyo imei sababu mabix huwa yanakuwa na imei au kwenye hiyo simu huwa zipo kwenye stika au maandishi yaliyo nyuma ya simu chini

Kumbuka kurudisha imei ile ile iliyo corupt kwenye simu husika sio kosa kisheria ila kosa ni kubadilisha imei ya simu A kuiweka kwenye simu B
Nimeenda na box na imei pia nilikuwa nayo niliwahi kuscreen shoot nikasave mahali ila wameniambia ni kipengele sana kuirudisha naona mafundi wanaziogopa sana note series jamaa ananiambia nimpe laki ajaribu nikaona haina haja.
Wacha nitumie lain moja tu
 
Hao mafundi hawana mabox ya kufkashia hao watakuwa wanatumia odin flash tool

Kwa mtu mwenye z3x box na updated software kwake hiyo ni kazi ndogo sana
 
Back
Top Bottom