Mtoboasiri
JF-Expert Member
- Aug 6, 2009
- 5,100
- 1,955
Wanaukumbi;
Hii tabia yetu ya kulalamika bila kuchukua hatua hatatufikisha popote. Na kati ya sehemu tunazoibiwa wazi wazi na bila kificho ni Makampuni ya Simu. Kwa mfano, Airtel wanakupa option ya kujiunga na internet "time based" kwa saa moja, siku, wiki, n.k LAKINI BILA KUKUPA OPTION YA KUKATIZA KUJIUNGA KWAKO. Kama kuna mtu anaiona option ya ku-unsubscribe naomba aniambie.
Maana ya hali hii ni nini? MTEJA UTAENDELEA KUKATWA PESA HATA PALE USIPOITUMIA bora tu saa/siku/wiki uliyojiunga imekwisha (hivyo kulazimishwa kujiunga kila saa/siku/wiki inayofuatia saa/siku/wiki uliyojiunga kwa mara ya kwanza). Customer service hawakwambii namna ya kujitoa na mara nyingi hawapokei simu na mara chache wanapopokea wanakwambia "tutashughulikia swala lako na tutakujibu" - and it NEVER happens.
HATUA ZA KUCHUKUA:
Ikitokea malalamiko yako hayashughulikiwi, ANDIKA barua (sio email) na hakikisha inapokelewa na unabaki na nakala ya hiyo barua. Barua hiyo itakuwa ni ushahidi wa wao kupokea malalamiko yako bila ya kuyashughulikia ukiamua kuchukua hatua za ziada (kwa mfano kuwashitaki TCRA). Bila ya kuwa na ushahidi wa maandisi TCRA hawatakuwa na nguvu ya kuchukua hatua maana airtel wataruka kimanga kupongea na wewe for sure.
Naomba tuungane kutoachia hali hii iendelee, na si kwa makampuni ya simu tu bali sehemu nyingine pia.
Nawasilisha!