Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 299,611
- 752,018
Tamaduni mila desturi na imani ni vitu vya kushangaza mno...ni sawa na kuumba roho ambazo hazipo na kuzifanya ziwe live ziishi na kuathiri maisha yetu kwa njia moja au nyingine
Tukianza na wazungu wenzetu hawa wana shida na namba 13 nakumbuka marehemu Michael Jackson aliwahi kufanya kila liwezekanalo mwanae asizaliwe tar 13 kwakuwa si siku nzuri
Kule china kuna namba nne! Kiasili hii si namba nzuri kwakuwa kwenye matamshi kuna tofauti ndogo sana ya kifo na nne.hivyo basi kwa china ya zamani ilikuwa ni jambo la kawaida kukosa ghorofa ya nne
Lakini ni hawa hawa wachina ambao kwao kutembelewa na bundi ni bahati kubwa sana
Ukija kwetu Africa ni balaa kubwa kumuona bundi karibu na nyumbani kwako au hata kusikia sauti yake
Nimetoa mifano hiyo michache ukiacha ile ya wahindi kuabudu ng'ombe na ukimpa mhindu nyama ya ng'ombe anaweza kufa kwakuwa ni kama amemla mungu wake...hii ni imani na imani huumba roho
Cha kujiuliza inakuwaje bundi huyo huyo awe ni baraka kwa wengine na nuksi kwa wengine?
Iweje namba fulani iwe ni mikosi kwa wengine na kwa wengine isiwe na madhara yoyote? ?
Dunia ina mengi ya kujifunza!hata kama huamini kwa dhati ya moyo kabisa kuwa kitu fulani hakipo lakini ukiishi na jamii husika inayoamini uwepo wake..kitu hicho chaweza kukuathiri kwa namna yake
Tujifunze kutomdharau mtu au kitu kuna mengi tusiyoyajua bado na imani huumba na kinachoumbwa ni roho yenye nguvu mno...mtu akikwambia hakuna Mungu mwambie hewala bwana....! Mtu akikwambia hakuna uchawi mwambie tawile...!unajua ni kwa nini? ?? Usibishane naye....amezingwa na nira za ufahamu finyu ...huwezi kwa hakika kumwambia mtu Ladha ya halua kama hajawahi kuila.....!!!!!bali wewe jifunze ili upate ufahamu