Imani ya ushirikina ulivyoharibu ratiba ya mazishi jana

kwa hio tangu jana hadi leo unaporudia tena msiban, huyo baba na mganga bado hawajarudi tuu?
 
Jana baada ya kupata taarifa ya jamaa yetu kufiwa na kijana wake (ameacha watoto 3 na mke mmoja) ikiwa ni siku ya pili tangu marehemu afariki, ilinibidi nisitishe shughuli zangu kuwahi mazishi ambayo yangefanyika saa 10 jioni japo ilibidi kuahirisha kutokana na sitofahamu iliyojitokeza hapo.

SAKATA LENYEWE ,Sakata lilianza baada ya mke wa marehemu na watoto kupandisha mashetani (mizimu) na kumshushia kipigo mama mkwe wake ambaye ni mama wa kambo wa marehemu akimtuhumu kumuua mme wake {ilibidi aokolewe na ndugu na jamaa na kutolewa eneo husika} huku akisema mme wangu yuko hai ndani ya nyumba na kama mnakataa mfuateni mganga (akamtaja) aje awaoneshe.

Baba wa marehemu bila kuchelewa akaanza safari kwa pikipiki kumfuata mganga umbali kama wa km 85. Hadi naondoka eneo husika mganga na mfiwa walikuwa hawajafika hivyo wananchi wakatangaziwa warudi makwao hadi leo 11/7/14 huku maiti ikifikisha siku tatu pasipo hata dawa ya kuifanya isiharibike.

Tafadhali mkuu usisahau kutupa mrejesho nyuma juu ya sakata hili.
 
Ng'wanapagi hukurudi tena msibani? Unatafutwa huku ulete mrejesho wa kilichojiri mara baada ya prof. Maji Marefu kiletwa kuichunguza maiti!
 
Back
Top Bottom