Kwanini usiongee naye?
Mkuu mbona kama unaikimbia Neema.
Mke anapaswa kumtunza mmewe
Ha ha ha mkuu tatizo liko wapi hapo sasa? Au una guilty concience? Mke anayesali na kukutii ndo mke mwema au unataka awe mcharuko asiyejali. Ila nahisi kapita sehemu flani nilikopita mimi na Evelyn Salt amepata mafundisho mazuri.
We jamaa hujipendi kabisa upendo wote huo tena mwanakarsmatiki hawa watu hua wana maono sana msikilize mkeo na fanya kila anachokueleza ni mke ambae namtamani maishani
Ninachoona hapa anakupenda sana na ana wasiwasi na imani yako huenda shetani akakupitia
Dah!
Munisijo,
Kwanza kabisa nakupa "hongera" kwa MUNGU wa ELIYA, 1 falme 18:21-40, kwa kukupa mke mwema sawa na Mithali 31:10-31, tena ningekushauri kuanzia muda huu unapo soma huu ushauri wangu, ungeandaa sadaka ya shukurani kwa mungu kwa kukupa mke mwema, kwa ajili ya kwenda kuitoa madhabahuni pale anapoabudu mke wako mwema. Maana kwa kufanya hivyo utapata kibali tena , yaani kumrudishia shukurani MUNGU kwa ajili ya mke wako. Ndiyo tena MUNGU atamtengeneza vile unavyotaka wewe awe tena. Maana sadaka itaunganisha moyo wako na moyo wa MUNGU na utakupa matamanio yako juu ya mkeo .
Pili , Wanaume wengi wamekuwa wakitafuta kuwa na mke mwema, lakini wanaishia kukutana na michomeko, wewe inakubidi umsikilize na umfuate kwa jinsi anavyokuongoza kwa maombi, maana neno linasema katika Yeremia 31:22imeandikwa MUNGU amefanya jambo jipya kwamba mwanamke atamlinda mwanamume. Sasa ni bahati kubwa sana MUNGU ametupa alafu unakuja kulalamika kitandani. Inakubidi utubu hakika.
Ongea naye kuhusu urefu wa hiyo sala hata mimi nasali asubuhi na jioni sometimes mchana nikiwa nafunga ila siwezi kuwa kwazo kwa watu wa nyumbani kwangu kutokana na sala zangu. Jaribu kuzungumza naye hope atakuelewa shida hapo ni urefu wa sala asio? Ila mshukuru mungu sana kwa huyo mwanamke usije ukamfanyia ubaya hata kwa kuficha, unaweza ukupata balaa.Ibada 2 kila siku, kabla ya kulala ... na asubuhi kabla ya kwenda job, sala zakuombea mpaka sahani, vikombe na bakuli. Dah nahitaji muda ama miujiza kwenda sawa, sitegemi kuwa na imani kiasi hicho kwa haya madhehebu na wachungaji wa siku hizi ...
Ongea naye kuhusu urefu wa hiyo sala hata mimi nasali asubuhi na jioni sometimes mchana nikiwa nafunga ila siwezi kuwa kwazo kwa watu wa nyumbani kwangu kutokana na sala zangu. Jaribu kuzungumza naye hope atakuelewa shida hapo ni urefu wa sala asio? Ila mshukuru mungu sana kwa huyo mwanamke usije ukamfanyia ubaya hata kwa kuficha, unaweza ukupata balaa.