Ilikuwa ajali au ndege ilidunguliwa?

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,108
Reaction score
34,933

​
Maafisa nchini Ukraine wanasema kuwa ndege ya abiria iliyoanguka nchini humo ilidunguliwa katika eneo la mashariki mwa taifa hilo ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali


​
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 298 ikiwemo watoto wadogo watatu. Ilikuwa safarini kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur


​
Mabaki ya ndege ilitapakaa kila sehemu katika ajali hiyo iliyotokea Alhamisi usiku






Haya ni baadhi ya masalia ya ndege hiyo ya muundo wa jet karibu na kijiji cha Grabovo, kinachodhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine


​
​
Ndege hiyo nambari MH17 ilikua inakaribia kuingia anga ya Urusi mawasiliano yalipokatizwa.



​
Rais wa Ukraine Petrop Poroshenko alielezea tukio hilo kuwa ni tendo la kigaidi huku waasi wakikanusha kuidungua. .


 

​
Inaaminiwa waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine walizidungua ndege mbili za jeshi la Ukraine katika eneo hilo hivi karibuni.
 
Reactions: prs

​
Inaaminiwa waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine walizidungua ndege mbili za jeshi la Ukraine katika eneo hilo hivi karibuni.

Mkuu, hata Putin mwenyewe jana kasema ndege hiyo ya kiraia ilidunguliwa na majeshi ya Ukraine walidhani yeye was among ya passengers!! Wamazo ya kushangaza kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…