Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,111
- 79,518
ILICHUKUA MIAKA MINGAPI?
Na, Robert Heriel
Siku zinaenda wala hazirudi tena, huchomoza Kwa tumaini na kuisha kwa sikitiko. Siku huja na mambo yake, huja na watu wake nazo huondoka na wasiowake, huacha simanzi Kwa waliobakia. Waliobakia huwajua walioenda, nao wajao hawawajui waliobakia, haya nayo ni masumbuko yasiyo na maana. Looh!
Niite Taikon wa Fasihi mkimbiza siku isiyo na mchana.
Kama nitaulizwa nitajibu, kama sitaulizwa nitakaa kimya nikitafakari maswali ya kuulizwa, lakini sio kila swali watakaloniuliza nitalijibu hata Kama ninafahamu majibu yake. Halikadhalika sio maswali yote nitaweza kuyatafakari ikiwa hawataniuliza.
Kama nikuzaliwa, ILICHUKUA miezi tisa na siku kumi na tano ndipo nilipozaliwa, nikazaliwa Kwa ajabu na walionipokea wakistaajabu kiumbe mpya katika ulimwengu WA zamani uliochakaa. Nikapakatwa, na hata hivyo sikujua mpaka wa leo ni Nani aliyekuwa mtu wa Kwanza kunishika mara tuu nilipozaliwa.
Ninachojua ni kuwa ilinichukua miaka mitatu kujua yupi ni Mama yangu ingawaje mpaka leo sina uhakika ndiye Mama halisi au laa. Hata hivyo ufanano wangu naye unatia moyo, na watu kuniambia ndiye Mama yangu unanifanya nizidi kuamini ndiye Mama yangu. ILICHUKUA miaka Saba kumtambua Baba, hata hivyo sina ushahidi wa hili.
Anyway ningesahau Jambo. Mara nilipozaliwa nilitulia nikitishwa na walionizunguka, waliogopesha, nyuso zao walizilazimisha zionekane zinaupendo, lakini haikuwa hivyo dunia chakavu ilisuta nafsi zao, ikawa dhahiri machoni mwangu kuwa sio watu wema, ILICHUKUA dakika tatu tuu kutambua kuwa dunia sio salama na wakaao ni watu Wabinafsi wenye kutaka mashindano.
Kama vile usiku ushindavyo na mchana ndivyo wanadamu walivyo, nikalia Sana siku Ile na hiyo ndio ishara ya pekee walimwengu waliokuwa wakiisubiria kutoka kwangu. Ghafla nikasikia sauti ya vigelegele na shangwe zikishangilia , hofu ilinizidi nilihisi watanila nyama kwani dhamira zao zilichakazwa na malimwengu. Nikazidi kulia zaidi na zaidi lakini hakuna aliyejali.
Ni mpaka dakika tatu kupita nikakumbatiwa na kuwekwa kwenye Nyonyo. Nikatulia. ILICHUKUA dakika tano tangu nimezaliwa kujua kuwa binadamu hufurahi unapopitia mambo magumu, unapolia wao hushangilia, hiyo huiita no ishara ya Uhai, kilio! Kilio badala ya kicheko. Looh!! Hata hivyo yupo mmoja ambaye atakuwa msaada kwako baada yako, yaani wewe mwenyewe na huyo wa pili, nashindwa kumtaja Mama Kama mtu wa pili baada yako ingawaje Kwa Asilimia kubwa anastahili lakini sio wakati wote. Haya nayo ni masumbuko ya mwanadamu.
ILICHUKUA miaka Saba kutambua kuwa Baba yangu Hana nguvu Kama zile nilizoziunda nilipokuwa tumboni mwa Mama yangu, pengine nguvu ya Shahawa iliniathiri nikajua Baba ananguvu kuliko mtu yeyote, unajua wengine walishindwa kunizaa, kile walichoshindwa watu wote Duniani isipokuwa Baba yangu ndicho nikakibeba kuwa Baba yangu anawashinda wote duniani. Lakini haikuwa hivyo, niligundua Baba hana nguvu baada ya kumuona Mama na wanaume wengine pengine huenda hisia na akili zangu zikabadilika tangu hapo.
Ningefikiri Mama anamheshimu tuu Baba lakini haikuwa hivyo, kumbe kila mwanaume anauwezo WA kuheshimiwa na Mama. Looh!
Sijui itachukua muda gani kujua anayesoma hapa anaelewa nikiandikacho, hata hivyo hilo sio juu yangu.
ILICHUKUA miaka kumi kugundua Mimi ni mwanaume, siku nilipoenda kuwinda Ndege nikiwa na manati yangu, Yule Ndege mwenyewe mbawa mbili na Mkia mrefu, USO wake ulikuwa jeuri na ujanja wa kisasa, Ndege Yule alikuwa jike, akiwa mtini hakujua adui Niko chini namuwinda, nikampogoa kwenye mbawa zake akapogoleka na kuanguka akiwa tayari mikononi mwangu. Kabla sijamchinja ilinichukua nusu dakika kutambua ndege Yule alikuwa jike mzuri ingawaje USO wake ulikuwa wa jeuri. Kama nisingemtunza Ndege jike yule mpaka akapona na nikamuachia huru huenda ingenichukua miaka mia moja kujitambua kuwa Mimi ni mwanaume.
Mwanaume ni muwindaji, huwinda Kwa akili, hujeruhi na kuua, hata hivyo hiyo haitoshi kuwa Mwanaume Bali akili yenye huruma na hekima humthibitisha mwanaume kamili.
ILICHUKUA miaka sita tangu nilipobalehe kutambua nchi inaweza kuwa huru Ila taifa lisiwe huru. Uhuru wa taifa unajengwa na viongozi kuwa huru, niligundua kuwa viongozi karibu wote wa nchi hii hawapo huru, wapo wapo tuu. Viongozi wasiohuru hulazimisha kuheshimiwa, heshima hailazimishwi, sio ajabu viongozi hujiwekea mishahara mikubwa na kujilimbikizia Mali ili waogopwe na kuheshimiwa,
Niligundua taifa hili halipo huru pale nilipoona wenye mamlaka wanaishi maisha ya kifahari na wananchi wakijizika katika makaburi ya ufukara.
Sisemi nikasema tena, yote yapo yalivyo wala sitaki yabadilike. Yawe Vivi hivi. Huenda ndio hekima kuliko yakibadilika. Nani ajuaye!
ILICHUKUA miaka ishirini tangu nilipozaliwa kujua kuwa watumishi wa Dini Kama wanavyojiita watumishi wa Mungu; Asilimia 90% ni wahuni na matapeli. Sitaki kusema uongo wao, sitaki kusema unyonyaji wao, sitaki kusema propaganda zao ambazo zinawafanya waonekane ni kweli wanaukaribu na Mungu kumbe ni uongo mweupe.
Kama Viongozi wa dini wangenikana na kunipinga na kunishtaki kuwa nimewatukana na kuwasingizia mambo ya aibu na uongo, nakuhakikishia wangekuwa wanasema kweli basi leo hii dunia ingekuwa salama, ingekuwa nadra Sana kuona serikali zikiwa na mafisadi na Rushwa, ingekuwa nadra kuona masikini wa kutupa, ingekuwa nadra Sana watu wa Dunia hii kukutwa na majanga ya Asili Kama matetemeko, njaa, mafuriko na magonjwa ya kutisha kwani wangetupa taarifa siku nyingi kabla mambo hayo hayajatukia.
Viongozi Fulani wa dini hupenda kunitisha Kwa kumtumia Mungu kama chambo ili niogope kuwaambia ukweli. Kila siku nawaambia huyo mnayemtaja hamumjui ndio maana mnamtaja kwenye mambo yenu ya hovyo.
ILICHUKUA miaka kumi na tano kujua kazi ya pili ya uume wangu. Kazi hiyo ndio ikanifanya nione uwepo wa wanawake. Kumbe uume ukisimama wanawake hushangilia, huimba na kucheza chereko chereko. Nikajiuliza mambo haya yanamaana gani, majibu yake niliyaona katika Sura za wanawake, nikasema kumbe ili mwanaume apate majibu basi yampasa autazame USO wa Mwanamke. Looh!
Ati USO wa Mwanamke hushtuka uonapo uume umesimama Dede Kama kigingi, baadaye moyo wake hufurahi na TABASAMU jepesi huchanua usoni mwake, sijui niseme au nisiseme! Acha nisiseme habari za katikati.
Uso wa mwanamke huchukizwa Kwa unafiki Kwa kuona mwanaume legelege, mwanamke huchukia lakini chuki ya kinafiki, yaani haonyeshi kachukia Ila ukweli ni kuwa huchukia mwanaume asiye mwanaume kamili, ninaposema kamili nazungumzia saa ya ukutani yenye mshale uliosomama wima kabisa ukionyesha Majira kamili. Sio nusu au Robo.
Sipendi kusema lakini Acha niseme, mwanamke hutaka kuwa wa mwisho kuingia akute kila kitu, na awe wakwanza kutumia. Hapendi kuhangaika, na kiasili haipaswi ahangaishwe. Hii ni kusema mwanamke Hana uvumilivu. Labda uvumilivu wa kinafiki huo anao na anaumudu.
ILICHUKUA miaka ishirini na tano kujua kuwa Maisha ni safari isiyo na Macho. Huenda hivyo hivyo pasipo kujulikama mbeleni kuna nini. Ikiwa safari haina macho tafsiri yake wasafiri ni vipofu. Naam binadamu ni vipofu katika safari Yao. Hawajui yajayo na Yale waliyonayo hawajui yataondoka lini.
Unajua Taikon alishajua wasomaji wake hawapendi Makala ndefu kwani akili ya binadamu hukinai mapema Jambo, naomba niishie hapa.
Ila naweza uliza haya?
ILICHUKUA miaka mingapi kutambua nchi uliyomo ni Masikini?
ILICHUKUA miaka mingapi kutambua kuwa Dini uliyopo haikusaidii lolote baada ya kufikia umri wa kujitambua?
ILICHUKUA miaka mingapi kutambua kuwa siasa ni vita vya maslahi Kwa Viongozi?
ILICHUKUA miaka mingapi kujua kuwa Mungu hataki umuombe?
ILICHUKUA miaka mingapi kujua kuwa Maisha hayatakuja kukuhurumia?
Tuishie hapa Kwa leo.
Ni Yule Mtibeli
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam