Umenikumbusha mbali sana. ...iliwahi nitokea, ...nilimkuta demu wangu yupo na jamaa wameshiba sana wanakunywa bia maeneo ya jirani na kambi moja ya polisi, kipindi hicho mi nna mwili mwembamba lakini nnajiamini balaa hehehe (changanya na mapenzi), basi nilivyomwona nikasogea mpk pale kisha nikamwomba niongee nae, mshkaji mmoja akamzuia kisha akauliza we nani? Nikamjibu kuwa mi ni mpenzi wake, mpenzi wangu kuulizwa kama ananijua akakana akasema tulishaachana kama miezi mitatu imeshapita wkt jana yake tu tulikuwa pamoja. ......basi ghafla nilijikuta napata ujasiri wa ajabu (kumbuka pale mezani walikuwa wamekaa wanaume wanne wameshiba na wasichana wawili, mmoja ndio huyo mpnz wangu), basi nilimsogelea nikamuuliza unasema tumeachana miezi mitatu nyuma? Akasema ndio, likanitoka kofi moja kali sana, demu akaanguka Chini. ...jamaa mmoja akachukua chupa anipige, wengine nao wakawa wanaamka kwenye vitu, watu nao wakaanza kujaa mmh nikaona hapa nakufa, basi nikawaambia wale jamaa kuwa nyie hapa kama mtanipiga basi mniue lkn mkiniacha hai tu basi mi naenda kusubiri huyu mwanamke getini kwao, mtakuja kwenye msiba wake. .....bahati nzuri kuna jamaa mmoja ni askari alikuwa anapita ananifahamu akaja sehemu nilipo then akaniambia niondoke ila nisiende home kabla ya kwenda police maana wale jamaa wanaweza niwahi.
Nikatoka hapo huku namshukuru Mungu, nilikuwa nimepaki gari mbali hivyo hawakujua kuwa nimekuja na gari, nikaenda mpk police station (ni kama dk 2 kwa gari) nikatoa taharifa ya uongo na kweli pale, wkt naendelea kuongea na police mara naona majamaa nao wanaingia na demu wangu kuja kuripoti hehehehe, waliponiona wakawa wanaambiana, aah nae kaja?
Basi jamaa nao wakasema nimewafanyia fujo kisha nikampiga msichana wao, askari mmoja akawauliza kuwa yaani nyie miili mikubwa hivyo mnaweza fanyiwa fujo na mtu mmoja? Au mmekuja hapa ili kumkomoa baada ya kumchukulia mwanamke wake? ....kesi ikamalizwa kichina mi nikachomoka zangu nikiwa namshukuru mungu kwa mara nyingine. .....yule msichana kwa sasa yupo kitaa choka kweli kweli, nikijaga likizo na nilionana nae huwa ananiuliza kama sijammiss, yaani anaomba tukakumbushie wkt hajui mwenzie nilishafunga ukurasa juu yake