Ilibaki kidogo tu nafsi iuache mwili

Ilibaki kidogo tu nafsi iuache mwili

EEX

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2014
Posts
4,312
Reaction score
13,966
Tarehe kama ya leo mwezi kama huu, huyu msichana alitukana na kuapia Miungu yote kuwa hatujui na wala hajawahi kutuona maishani mwake(msichana huyu alikuwa mpenzi wa rafiki yangu).

Wacha jamaa tuliyemkuta nae na washikaji zake waanze kutushushia kipondo.

Jamaa yangu akatimka mbio nyingi sana nikabaki mimi na mwili wangu wa ukibonge nikiendelea kusulubiwa vilivyo huku watu wakizidi kuongezeka.Akili ikanituma nijifanye nimekufa,nikawa nawasikia wananchi wakisema "achomwe moto tu huyu" wengine liacheni limeshajifia hili likibaka.
Mungu mwema wakati wale wananchi wanajadiliana nini cha kufanya akatokea msamaria mmoja aliyenitambua na akawaambia huyu dogo sio kibaka mpaka kwao napajua.

Na hiyo ndo ikawa salama yangu.

Nilipoteza viatu,simu,miwani,fulana na pesa kiasi.Wapenzi hususani dada zangu jaribuni kuwa na mioyo ya huruma kwenye mazingira kama haya.
 
Haha dah mkuu pole sana sikupatii picha na huo ubonge wako, anza basi mazoezi madogo madogo
 
pole sana hii story ni kama wewe ndo uliniadisia au huyo rafki yako au kuna mtu ilimtokea hivi hivi yaani pale coco
alipigwa kama mwizi
 
Haha dah mkuu pole sana sikupatii picha na huo ubonge wako, anza basi mazoezi madogo madogo
Nimekimbia sana lakini wapi,nimekunywa maji yenye malimao yenye uvuguvugu nayo ni kama bure tu,nikafanya ka"diet" ka uongo na kweli hakuna mabadiliko.Watu wanadai ni limwili la asili.
 
Nimekimbia sana lakini wapi,nimekunywa maji yenye malimao yenye uvuguvugu nayo ni kama bure tu,nikafanya ka"diet" ka uongo na kweli hakuna mabadiliko.Watu wanadai ni limwili la asili.

Mkuu inabidi uache kula sasa....
 
Hahahahahaha nimecheka hadi chozi ila pole jaman sipati picha kutandikwa hadi kujifanya maiti! iyo noma
 
Tarehe kama ya leo mwez kama huu,huyu msichana alitukana na kuapia Miungu yote kuwa hatujui na wala hajawahi kutuona maishani mwake(msichana huyu alikuwa mpenzi wa rafiki yangu)
Wacha jamaa tuliyemkuta nae na washikaji zake waanze kutushushia kipondo.Jamaa yangu akatimka mbio nyingi sana nikabaki mimi na mwili wangu wa ukibonge nikiendelea kusulubiwa vilivyo huku watu wakizidi kuongezeka.Akili ikanituma nijifanye nimekufa,nikawa nawasikia wananchi wakisema "achomwe moto tu huyu" wengine liacheni limeshajifia hili likibaka.
Mungu mwema wakati wale wananchi wanajadiliana nini cha kufanya akatokea msamaria mmoja aliyenitambua na akawaambia huyu dogo sio kibaka mpaka kwao napajua.Na hiyo ndo ikawa salama yangu.
Nilipoteza viatu,simu,miwani,fulana na pesa kiasi.Wapenzi hususani dada zangu jaribuni kuwa na mioyo ya huruma kwenye mazingira kama haya.

Huyo demu alikua wenu au wake? na wewe na ubonge wako utakaaje mpaka dakika ya mwisho wakati demu hakuhusu?
 
ulikagua rasilimali zako?? usijekuta watu waligundua gas wakaexploit
 
Huyo demu alikua wenu au wake? na wewe na ubonge wako utakaaje mpaka dakika ya mwisho wakati demu hakuhusu?
Alikua demu wa mshikaji wangu,jamaa yangu aliniomba nimsindikize kwa huyo mwanamke.
 
Back
Top Bottom