Ilianza Mt.Kilimanjaro,kisha Tanzanite na sasa ni Olduvai Gorge, Watanzania tunaenda wapi?

Kule Kwetu

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
3,157
1,893
Habarini Wadau,

Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na mfuatiliaji wa maendeleo ya wizara ya utalii hapa nchini,ataweza kushangazwa sana na jambo hili la rasilimali za Tanzania kutangazwa kuwa zipo au zinapatikana Kenya.

MIFANO:

1) Katika awamu ya pili ya uongozi wa serikali ya JMT chini ya Ali Hassan Mwinyi,tuliwahi kusikia na ilithibitishwa kuwa Wakenya walikuwa wanawapeleka Watalii Masai Mara na kisha kuwapandisha Mt. Kilimanjaro kwa njia za upande wa Kenya na kudai Mt.Kilimanjaro ni ya kwao.

2) Wakati Zakhia Meghji alipokuwa Waziri wa Utalii (katika awamu ya3) kuna habari zilienea kwenye magazeti ya huko Uingereza kuwa Tanzanite inapatikana eneo la kisumu huko kenya pekee na si kwingineko duniani. Na issue ilikuwa exposed na wanafunzi wa kitanzania wanaosoma kule Uingereza.

Hiyo ilitokana na kwamba wakenya walikuwa wanakuja kununua Tanzanite huku kwetu (kama brokers) kisha wanaenda kukata, kushape,kuosha na kuzipack na baadaye kuuza Africa kusini, Uingereza,Marekani na sehemu zingine duniani.

Leo hii tunasikia wakenya wakiadvertise kuwa Olduvai Gorge ipo Kenya. Sidhani kama Waziri mwenye dhamana atalikemea na kuhakikisha huu uhaini unaisha. Sanasana najua atalalamika na itaisha bila kufuatiliwa.

IKUMBUKWE KUWA: kwa utafiti wa mwaka 2013, pamoja na Serengeti kuwa mbuga bora Afrika,Ngorongoro ikiwa nafasi ya 5 huku Masai Mara ya Kenya ikiwa ni nafasi ya 8, na huku tukiwa na Game reserves nyingi na nzuri kama Selous,na zaidi Mt. Kilimanjaro mlima mrefu kuliko yote Afrika.

Tanzania inayojivunia amani ilikuwa nyuma kwa kuingiza idadi ndogo ya wageni kuliko Kenya yenye ugaidi wa mara kwa mara na rasilimali chache.

MASWALI LA MSINGI:

-Tuko wapi mpaka tufanyiwe hivi na Wakenya?

-Sisi Hatuwezi kufanya Good Advertisements kwenye nchi zingine?

-Kwanini hili tatizo linajirudia? Mawaziri wanafanya nini?
 
Back
Top Bottom