Ili tuendelee hatuhitaji watu, ardhi

Ili tuendelee hatuhitaji watu, ardhi

tubalayya

Member
Joined
Apr 16, 2010
Posts
69
Reaction score
105
....wala siasa safi. Tunahitaji uongozi bora pekee.
Fikra za kwamba ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi.... hazina mashiko hivi sasa. Kama kitu chochote katika dunia hii, huchakaa na kufa. Tatizo watu kwa hulka yao hupenda kung'ang'ania.

WATU: Hapa hayati Nyerere alikusudia nchi haina budi kuwa na idadi kubwa ya wananchi ili iendelee! Si kweli. Emirates, Qatar, Luxemboug, Taiwan....hazina hata asilimia 10 ya raia wa Tanzania, lakini, kama Qatar yenye wakazi 2.6 milioni ( laki tatu tu ndiyo Waqatari wazawa), pato lake la mwaka ni dola bilioni 370 ambapo kila mtu anafurahia kipato cha dola 77,000 kwa mwaka. Fananisha na Tanzania watu milioni 70+ pato la mwaka dola bilioni 77~80, na kila mtu 'anafurahia' tunda la dola 1,400 tu(wale wazipatao)!

Kuna atakayesema ' lakini Qatar wana mafuta na gesi'! Ingawaje siye tuna mali zaidi ya hizo. Lakini chukua Luxembourg yenye wakazi laki 7tu lakini mapato ni dola bilioni 138 kwa mwaka na raia wanafurahia kipato cha dola 120,000 kila mmoja kwa mwaka. Sasa, Luxembourg haina vyanzo vyovyote, wategemea viwanda kidogo vya chuma, chuma cha kununua, na utalii na mabenki! Hivi wingi wetu umetufaa nini hapa? Nikileta mahesabu ya Emirates, Taiwan, Malaysia, Singapore....zote hazina watu kama siye, wala rasilimali, lakini maendeleo yaliyotupita kwa miaka 100 ijayo....utalia!

ARDHI: Halkadhalika nchi hizo hazina ardhi yoyote. Infact, kwa wale waliofika Malta, hili ni jiwe moja tu lilikitwa baharini lakini wanakula, wanakunywa, .....kutushinda siye wenye ardhi. Nadhani hayati Nyerere alipotaja ardhi alikusudia sote tuwe wakulima ndiyo tutaendelea! Kama angetaka tuendelee kwa kilimo angeanza kama alivyofanya Capt. Traore aliyenunua matrekta 40,000 katika awamu ya kwanza, akawagawia wananchi. Kilimo cha jembe? Hata wakulima wenyewe wafa njaa!

SIASA SAFI: nope! Siasa yoyote yaweza kuendeleza nchi: safi, mbovu, inayonuka... nk. Nchi chungu nzima duniani zimeendelea kwa siasa tofauti kabisa:
Marekani, Uingereza: Ubeberu
Ujerumani, Utaliano: Ufashisti ( Hitler aliikuta Ujerumani 1923 baada ya vita vya Kwanza, ikiwa imefilisika, madeni, watu walala na njaa barabarani! Pesa yao ilikuwa zaidi ya Zimbabwe, Deutschemark milioni 2 kwa mkate mmoja! Ila kufikia mwaka 1933 yeye na chama chake cha Nazi waliweza kuirudisha hali na hadi kufikia mwaka 1939 Ujerumani ilikuwa na nguvu kuliko nchi zote za Ulaya!
CHINA, BELARUS, CUBA: Hizi ziliendelea kwa Ujamaa
IRAN: Hii imeendelea kwa mfumo wa Kiislamu.

Hii yaonesha wazi mfumo wowote wa siasa unaweza kuendeleza nchi. Deng Xiaoping 1904~97, baba wa maendeleo ya China alisema: 'Haijalishi kama paka ni mweusi au mweupe maadam hukamata panya'!
Sasa, kama watu, ardhi, siasa safi....si lazima kwa maendeleo, ni kipi basi?
UONGOZI BORA! Ndugu zangu hiki ndiyo kitu pekee kinachoitoa nchi kutoka kuchelewa, ujinga, maradhi, imani za kichawi na superstitions....kuelekea maendeleo.
Hebu tuelezee maendeleo ni nini hasa, maana kuna puguwani wanaoona SGR, barabara nne mjini ndiyo maendeleo, ingawaje hajui jioni atakula nini!

Maendeleo ni kuwa na taifa ambalo at least 80% ya wakazi wanamudu mahitaji yao ya lazima katika maisha, tena ya viwango. Wanakula milo mitatu balanced, watoto wao waenda shule kupata elimu bora, wanamudu matibabu ya kuaminika, na wana uhuru wa kutoa maoni yao bila ya kupotezwa.
Katika baadhi ya mahitaji haya, maendeleo yanamaanisha kufikia asilimia 100%. Kama elimu ya kiwango cha kumtengeneza mtu, kula milo mitatu.....ndiyo maana katika nchi zilizoendelea hakuna anayeshindwa kumpeleka mtoto Shule, hakuna anayekufa kwa utapia mlo nk. Hayo ndiyo maendelea.
Maendeleo pia ni kuwa na wananchi wenye elimu ya kujiamulia na kujitengenezea wenyewe zana na miundombinu wanayoihitajia kwa maendeleo.

Kufikia maendeleo haya ya kweli si rahisi. Yataka uongozi usiojipenda, focused, unaopenda watu, unaoathirika kwa hali zao, unaokosha wizi,rushwa, upendeleo, uzembe, ufujaji na unaojitoa muhanga.
Ndiyo maana wanakimbilia mambo rahisi rahisi tu na kuyapigia debe sanaaa na kujipiga kifua, kama kununua ndege, SGR... haya ni msaada tu wa kufikia maendeleo. Maendeleo hasa ni tunapoweza kutengeneza wenyewe!

Bila ya uongozi bora hakuna maendeleo!
 
Taifa linaloona wananchi wake hawapaswi kuwa matajiri; Kwanini awe tajiri bila kuwa wa kwetu( elites), basi hili taifa ni mfu.

Kwa Africa, uongozi ni kimbilio la kujineemesha. Sehemu wakimbiliao watu wabinafsi, wachoyo na wanafki. Kwa mantiki hiyo, kupata uongozi bora ni ndoto za mchana.

Sijui nataka kusema nini. Ila Africa ina safari ndefu sana.
Kuna makosa mengi sana yalifanyika kipindi vuguvugu la kujikomboa lilipoanza. Kila aliyekuwa kiongozi alitaka 'udon'.. kwa eneo lake. Mgawanyiko huu ulileta athari kubwa sana ambayo bila maamuzi magumu, tutakuwa wasindikizaji Daima.
 
Back
Top Bottom