Huntsman
JF-Expert Member
- Oct 11, 2012
- 646
- 608
Nimeanzisha uzi huu uwe uzi kinzani wa mwana CCM kindakindaki ndugu Lizaboni hoja yake haikuwa na mashiko hivyo sitajibu lolote kwa sababu ni hoja Mufilisi. Katika hoja yake amesema Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye msimamo.
Mimi ninapinga jambo kwa kumkumbusha maneno ya muasisi wa Chama chake Mwalimu J.K. Nyerere aliyepata kusema kuwa ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne:
1. Watu
2.Ardhi
3.Siasa Safi
4.Uongozi Bora.
Hapa kwetu Tanzani vitu viwili yaani namba 1 na 2 tunavyo tumekosa vingine viwili tangu enzi ya Awamu ya pili yaani namba 3 na 4. Tukipata vyote hivyo hakika tutaendelea. Siasa inayoamua mustakabali wetu ikiwa safi hata mustakabali wetu utakuwa safi. Uongozi ukiwa bora na usipogeuka UTAWALA hakika sisi wananchi tutaona kule tunakoongozwa sio kubaya tofauti na ilivyozoeleka tangu awamu ya pili na inavyozidi kuwa mbaya. Sasa ni kama vile hakuna uongozi bali utawala au Himaya ya mtu binafsi
Pia ndugu Lizaboni kazi ya Rais sio kujenga fly overs kama ulivuosema au kujenga madaraja. Kazi yake ni kubwa hasa kuhakikisha namba hizo mbili yaani 3 na 4 zinakwenda vyema vinginevyo tutazidi kudidimia na misimamo isiyokuwa na Tija kwa Taifa.
Alamsik.
Cc: Lizaboni