Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,335
- 72,799
Ni dhahiri kuna kosa la kikatiba ambalo tayari linaonekana kuwa limefanyika katika uteuzi wa nafasi 10 za Rais kuteua wabunge. Katiba iko wazi kuwa lazima Wanawake wasiwe chini ya Watano, na kwa sasa hata hizo nafasi zilizobaki wakipewa wanawake bado uwiano hauwezi kuwa hivyo tena.
Ili kulinda heshima ya mteuaji kwa kukosea kwake ni lazima mmoja wapo kati ya Prof Kabudi au Abdala Bulembo atangaze kutokubali uteuzi huo kuliko kusubiri jambo hilo kugonga ukuta Bungeni wakati wa kuapishwa. Yako mawazo kuwa hili jambo ambalo ni uvunjifu wa katiba linaweza kulazimishwa kufanyika, lakini hiyo itadhihirisha kuwa kumbe Katiba haiheshimiwi na hata lile wazo la Zitto kupeleka mashtaka Bungeni dhidi ya Rais ni ya msingi.
Jee kwa umuhimu wao wakiwa ndani ya Bunge, hawa wawili ni nani atangaze kutokubali uteuzi ili kumpa nafasi mwingine mwenye umuhimu? Nani KABUDI au BULEMBO out?