Ili kuleta nidhamu na uwajibikaji, Serikali ipeleke vijana jeshini miezi 12 then waingie chuo kikuu

Midumare Ngatuni Iwato

JF-Expert Member
Jul 13, 2016
1,653
2,042
Ili kuleta nidhamu,utii,adabu na uwajibikaji kwa vijana kuwa wazalendo katika Taifa lao la Tanzania napendekeza jambo hili muhimu lifanyike na maendeleo yatakuja kwa kasi sana.

Serikali Mwaka huu wa 2017 mpka 2018 ipige marufuku au kusitisha masomo ya Elimu ya juu kwa vijana wote iwe amri halali na ya kisheria lazima kwenda Jeshini miezi kumi na mbili then ndio Chuo kikuu.

Kwa wale ambao watakaokimbilia nje ya nchi kusoma atakaporudi tu lazima kwenda jeshini miezi 12.

Itengeneze utaratibu kwa watumishi wote wa umma na binafsi walio chini ya miaka 45 wapangiwe na waajiri wao ndani ya miaka mitano wawe wamekwenda wote angalau miezi mitatu, ambaye atagoma kwenda ndio mwisho Wa ajira.

Matokeo yake nikuzalisha kizazi ambacho kitakuwa Tiifu kwa nchi kwa ujumla watu kutoipinga serekali halali na hata kwa kiasi kikubwa kupunguza rushwa.

Uwajibaki kazi kuwa katika hali zuri sana nawakaribisha wale wapenda maendeleo ya vitendo kutoa mawazo yakujenga Taifa letu na sio watu wa kulalamika kila jambo kwao ni baya linalofanywa na Serikali yoyote ile.

Matusi na kashfa ni dalili za kutoelimika na unakosa nidhamu na heshima kwa kutoitendea vema katiba na haki ya Uhuru Wa mwenzako.

Karibuni watanzania wote.
 
Hebu niambie kati ya wote waliokumbwa na kashfa ya ufisadi nani hajapitia JKT na wengine wamepitia mpaka JW, kama wapo ni wachache sana
 
Mabadiliko yanaitajika tujenge hoja nasio kuhukumu naombeni mawazo mema yakuwafanya wananchi hasa vijana kuwa na nidhamu.heshima.utii.nasio kuangalia wapi tulipoanguka Bali nini kilichotuangusha
 
si juzi hawa form six waliokosa vyuo waliombwa kwenda jeshi na "green vest" kwamba serikali haina pesa....
ukisema wakae miezi 12 itakuaje?
 
Hivi ni nani yule alipiga ela za mradi uliofagiliwa sana wa POWER TILLER
 
KItu kigumu zaidi katika kufanya mabadiliko sahihi ni namna ya kujibadilisha kwanza wewe mwenyewe,
Uzalendo uanzie kwanza kwa hawa wanaooongoza nchi hii, na vijana wakiona kuwa viongozi ni wazalendo sina shaka hata watapoanza kuhubiri uzalendo kwa wengine wataeleweka.

Sasa we wataka raia kuwa wazalendo wakati watawala wenyewe ni madhalimu hawatendi haki, hawana utu hapo unategemea nani afurahie huu upuuzi?
 
Back
Top Bottom