Ili kukuza uchumi, tunahitaji kuchora mstari baina ya wanasiasa na wataalamu

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Tanzania ni nchi tajiri ki rasilimali kuliko ncho zote za afrika mashariki lakini utajiri huu wa rasilimali hauko reflected katika maisha ya watu au kipato, Tatizo liko wapi?

tatizo kubwa la tanzania ni kutokuwepo mstari unaosema mwanzo na mwisho wa mwanasiasa ni huu na mwanzo na mwisho wa wataalamu ni huu.

wanasiasa wamekuwa wakifanya maamuzi yanayotakiwa kufanywa na wataalamu na katika kufanya hivyo ni sawa na wacheza mpira wanaokuwa uwanjani hawajui gali lao liko wapi na matokeo yake wakati mwingine wanabutua hata kuelekea gorini kwao.

ipo mifano iliyo wazi kuonyesha tofauti kubwa mfano baina ya kenya na tanzania nchi ambazo ukizingalia kimitaji ya rasilimali utashangaa jinsi gani kenya inaweza kuwa juu ya tanzania.

1. kwanza ni mfumo wa vitambulisho.
ni kwa jinsi gani nchi yetu haioni umuhimu wa vitambulisho hata kiuchumi? kenya wameweka mfumo wa vitambulisho vya taifa ambavyo wanaweza kudhibiti wageni. huwezi kuwa na uchumi unakua huna mfumo wa kudhibiti wageni na majirani zako wasiwe wanaingia kutafuta maisha. ukiwa na vitambulishop vya taifa huhitaji kutumia gharama kwa kila taasisi kuwa na ka mfumo kake kadogo ka kutambua wateja wake. ukiwa na vitambulisho vya taifa ni rahisi kudhibiti ukwepaji kodi, watumishi hewa, uhalifu na kila kitu. mwanasiasa ndiye anaweza kuhold vitambulisho vya taifa kwa miaka mingi kama kwetu na kufast track vitambulisho vya kura ili kubaini wapiga kura, kuhangaika kutumia gharama kubwa kukabiliana na changamoto moja moja kivyake badala ya kutumia gharama kidogo katika vitambulisho vya taifa.

2. kuna mtu mmoja alikuwa anadai uchumi wa tanzania uko juu ya uchumi wa kenya akidai tanzania kuna magari ya kifahari mengi kuliko kenya. hatujiulizi kwa nini kenya shilingi yao iko imara miaka mingi huku sisi shilingi yetu ikiporomoka? wao wanatumia wataalamu wanawaambia magari yanadrain uchumi wao kwa kuwa ni imports. wakaamua kuweka mifumo ambayo wakipiga mahesabu kwa mwaka ni wanatoa foreign currency kiasi gani katika sekita hiyo iko chini kulinganaisha na sisi tukidhani ni ufahari. wanasiasa wanafocus kutatua changamoto katika sekita hii kwa kuongeza barabara tu. yawezekana hii ni presha ya juu hivyo haitatuliwi kwa kuongeza mishipa ili damu ipite kwa urahisi bali kupunguza unene pengine kwa kupunguza vyakula vya mafuta. wataalamu wanaweza kuona lakini mwanasiasa anaona barabara tu kuwa ndio tatizo.

3.inashangaza kuona katika awamu ya nne serikali ilitoa ruzuku kwa mbole mavuno yakaongezeka. wakuu wa mikoa wakawa wanapiga marufuku kwa mikoa ya mpakani kama mbeya na rukwa kuuza chakula nje? kama wataalamu wangekuwa wametumika wangewashauri serikali kuwa kuuza chakula nje hata kama hakilipi kodi kina faida kubwa sana kwa taifa kuliko chakula kinachoozea kwa wakulima. kuzuia wakulima kuuza kunawakatisha tamaa hivyo huku unahamasisha kilimo kwa kutoa ruzuku huku unazui maendeleo kwa kuua masoko ya mazao ya kilimo.

kimsingi kwa tanzania tunabutua tu, kila taasisi inapanga mambo yake, kila mwanasiasa ni mtaalamu anafanya maamuzi yake. hii sio mipango hata kama tuna kaskeletoni kanaitwa mpango wa taifa na kila mmoja anaweka nyama yake.

tunahitaji kuweka mstari baina ya utaalamu na wanasiasa.

mstari huu ni wanasiasa kutambua kuwa wao kazi yao ni kuhamasisha na kusimamia mipango iliyokwisha pangwa na sio wao kuwapangia wataalamu.

huwezi kuamini kusikia tanzania tuna gesi, alafu kwa mwaka tunaingiza mafuta zaidi ya lita bilioni tatu. tumevumbua gesi tunasikia wanasiasa wakisimama kwenye majukwaa wakijigamba sisi kuondokana na umeme wa maji kwa kuanza kutumia gesi. kwa mwanasiasa haya ni maendeleo makubwa lakini je wataalamu wanakubali haya ni maendeleo?

kama wataalamu wangetumika kwanza kupanga tungebaini kuwa tunaweza kupata faida kupitia gesi yetu kwa kuanzia nyumbani kupunguza imports za mafuta. kwa nini tusianze mchakato wa kubadilisha magari yetu kutumia gesi. umeme wa maji kuuzalisha ni bei nafuu sana kulinganisha na gesi na kwa kuwa gesi ni biashara basi gesi itumike kwa emergency tu lakini lazima tuendelee kuzalisha umeme kwa maji.

kuchora mstari ni kwa kutumia wataalamu kuplan na wanasiasa wote wanaanza kuhamasisha mpango wa serikali uliopangwa. Sio kuwapa vichwa vya habari kila mmoja akajaze nyama zake bali kama ni kilimo wataalamu wanaandaa mpango wa kuendeleza kilimo ambapo wizara ya kilimo inaambiwa wajibu wake, wizara ya fedha inaambiwa wajiwa wake, halmashauri zinaambiwa wajibu wake, wakulima na kila mdau anajua wanatakiwa kufanya ni wakati gani.

kila anayesimama kwenye jukwaa anatekele mpango ule ule, kila aliyekaa ofisini anatekeleza mpango uleule, kila anayetoza ushuru anatekeleza mpango uleule, kila anauza pembejeo anatekeleza mpango uleule, anayetoa mikopo anatekeleza mpango uleule, anayelima anatekeleza mpango ule ule.

lakini kuwaachia hasa wanasiasa kila mtu akapanga yake, wale wanaoelekezwa nao kila mmoja anatekeleza yake. huyu anasimama kwenye jukwaa anaahidi ruzuku ya mbole huyu anasimama jukwaa lilelile anapiga marufuku masoko yaliyopo kama kuuza nje au kutengeneza vinywaji wakati anakoelekeza masoko halali anayoyataja hayapo kwa wakati huo na yeye hana mpango wowote. hii ni kutokuwa na mipango na kila mmoja anabutua anavyotaka hakuna timu inaweza kupata ushindi haswa kama kwenye mchezo kuna timu ziko makini sana.
 
wakati mwanasiasa anaona mawasiliano ya data, tv, michezo ya kujiliwaza kama vichecheo vinavyosababisha watu kuwa wavivu na kuacha kufanya kazi wataalamu wanaona uvivu si matokeo ya huduma fulani kwenye jamii.

wataalamu wanaona watu kushinda kwenye baa wakicheza pulu, kushinda wakichati, kushinda wakiangalia tv ni kutokana na ukosefu wa ajira. tatizo hili haliwezi kuondolewa kwa kufunga data, kufunga mabaa, kuzima tv bali tatizo hili litaondolewa kwa kutengeneza nafasi za ajira.

hakuna mwanadamu anayependa kushinda anacheza pulu huku nyumbani familia inamtegemea au akitoka hapo akaombe chakula. lakini kama cha kufanya hakipo kujiliwaza ndio jambo la busara.

ajira zinatengenezwa na mambo mwili makuu. kwanza ni shida za watu pili ni uwezo wa wenye shida hizo kutoa gharama kuhudumiwa. kama kimojawapo hakipo au vyote havipo basi ajira hakuna. hata nguvu ikitumika kuwalazimisha watu kutoa huduma au bidhaa ambazo ama watu hawazihitaji au wanazihitaji lakini uwezo wa kuzigharamikia haupo matokeo ni hasara kwa maana nguvu inayowekezwa haitarudi au hawatapata mahitaji yao.
 
Ndani ya taaluma kwenyewe pia tunahitaji kuchora mistari pia kama siasa zinazoongoza kila kila zinavyoingilia kufanya maamuzi hata yaliyotakiwa kufanyika kitaaluma, wanataaluma nao wanaiga mambo hayo hayo.

yawezekana kama wanavyosema baba mifano anayoitoa katika familia ndivyo watoto nao huenenda. yaani kwa kifupi tumechagua mifumo holela katika kila kitu.

jinsi unavyoona mitaa yetu imevurugika kimakazi ndivyo kila kitu katika jamii yetu kinavyoendeshwa holela.

uhelela huu ndio kikwazo namba moja katika maendeleo yetu.

hatuwezi kupata maendeleo kwa kusema wataalamu tu wataalamu wafanye kazi kwanza alafu ndio wanasiasa waje nyuma kuhamasisha na kusiamamia kama ndani ya wataalamu nako kutakuwa na mifumo holela.

Leo hii serikali ikitaka kufanya jambo inatumia gharama kubwa kuajiri wataalamu kufanya kazi hizo. hapa uholela unaibuka ndani ya wataalamu kwa kutumia makoti ya utaalamu kupata kazi lakini wakishapata uholela unabaki palepale na kukwamisha kazi hizo.

mfano kama ni utafiti unaohitaji kutumia wataalamu wengi basi wahusika hujaribu kubana matumizi kwa kutumia watu wachache ili walipe kidogo na kujilimbikizia faida na kupata utajiri wa haraka. wakati mwingine kwa kuwa kutumia wataalamu ni gharama basi hutumia watu wasio na ujuzi ili kuwalipa kidogo na matokeo yake ni kuapata kazi iliyotoka kwa wataalamu kwa jina lakini kazi yenyewe si ya kitaalamu.

mfano serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa katika miradi ya maendeleo, miradi inayohitaji utaalamu wa aina tofauti mbali na serikali kutumia gharama kubwa kugharamikia miradi hii lakini unakuta mtu mmoja au wawili wa taaluma moja ndio wanafanya kazi za kufanywa na watu wenye taaluma kama Tatu. matokeo yake ni ubabaishaji. mambo haya yanalitia taifa hasara kwa kutumia gharama kubwa lakini kupata miradi yenye quality mbovu. mambo haya yanawanufaisha watu wa kati kwa kuacumulate faida na kujipatia utajiri wa haraka. mambo haya yanaliathiri taifa kwa kuleta tatizo la ajira.

hivyo si tu kuweka mistari baina ya siasa na wataalamu bali kunahitajika kuweka mistari katika taaluma pia.

yaani tuondokane na mifumo holela katika kila kitu.
 
Nchi haiwezi ishi bila wanasiasa.Wanasiasa kazi yao ni coordination.Wanacoordinate wataalamu wote wa fani tofauti wafanye kazi towards a common goal.Sababu ukiachia kila mtaalamu mmoja afanye vyake nchi itaenda kama gari la mlevi.

Mwanasiasa ndiye kiunganishi cha wote.Wawe mainjinia wa barabara,madaktari,walimu.maprofesa,wanajeshi nk ndiye muweka mikakati ya namna gani hao wote wafanye kazi wafikie lengo moja.Ukiondoa wanasiasa ukabakiza wataalamu pekee nchi haitaenda
 
kama sisi wenyewe tunavyofanya kazi kwa uholela ndivyo masoko yetu yalivyo holela. hakuna udhibiti wa bidhaa kutoka nje bidhaa zinaingia kama hakuna mipaka.

hivi tunajua tatizo kubwa la vijana wetu kutokuzalisha ni ushindani ulioko sokoni ambao umeachwa holela bidhaa za nje zinashindana na bidhaa za ndani ? huwezi kukuza kitu chochote kama kitu kichanga hiki kinashindana na kitu kilichokomaa kugombania mahitaji.

bila shaka kitu kichanga kinahitaji kulindwa. ulinzi huu unahitaji umakini ili usikiharibie kichanga hiki kinachokua future yake. yaani usikifanye kilichokomaa useles ili kukuza kichanga kwani kichanga hiki kikishakomaa kitakuwa useless pia.

tunahitaji kulinda wazalishaji wa ndani dhidi ya masoko ya nje ili wazalishaji wetu wa ndani wakue lakini katika kuwalinda huku tunahitaji kutokuharibu biashara ya kimataifa kwa wazalishaji wetu wa ndani tunataka baadae nao wazalishe wakauze nje.

kama unavyoona viongozi ambao ni politicians wakifanya mambo holela ndivyo masoko yetu yalivyo holela.

tunahitaji kuweka mistari katika bidhaa na huduma. mistari hii pia haitakiwi kuwekwa kwa mifumo ya holela bali kitaalamu ili kulinda future ya wazalishaji wetu.
 
my point is kuendesha taifa ni kama mradi ambao uko very complex.

hakuna mradi unaoweza kufanikiwa bila mpango ulio makini.

tunaanzia wapi ni je ni wanasiasa kupanga na wataalamu kutekeleza au wataalamu kupanga na wanasiasa kutekeleza?

hicho ndicho kitendawili kikubwa.

hatua ya kwanza inaweza kuanzia kwa wanasiasa kwa kutoa wapi wanataka kwenda.

watalamu wanaweka mawazo hayo into action plan na huo ndio mpango wa kazi.

then wataalamu wakisha panga inarudi kwa wanasiasa kuhasimasisha utekelezaji na kusimamia utekelezaji na wataalamu wanarudi tena chini ya wanasiasa kutekeleza.

mfano unataka kuondoa umasikini kwa wafugaji. hii ni ajenda inayoweza kujengwa na mwanasiasa then wataalamu watakaa chini wataona wafugaji wana bidhaa kama maziwa, nyama, ngozi mbole.

ili kuondoa umasikini watalamu watatafuta jinsi gani unaweza kuwapatia watu hawa masoko ya bidhaa zao. wanaweza kuona mfano soko la ndani limejaa maziwa yalifungashwa yanayotoka nje watajiuliza ni kwa nini maziwa hayafungashwi ndani?

hawaishii hapo watajaribu kuangalia ikiwa leo hii mtu anafungasha maziwa je bei yake itakuwaje kulinganisha na maziwa ya nje? bei tu watangalia je wapandishe bei ya maziwa ya nje au wapunguze bei ya maziwa ya ndani ni kipi kitafnya biashara hii ya maziwa kutokufa ikaendelea na ikwa na tija kwa taifa kwa maana ya sio tu kuwapatia soko hawa bali pia kwa kupatikana fedha ya kuwapatia huduma nyingine kupitia kodi.

je kuna vikwazo gani katika uzalishaji? miundombinu, utaalamu, mitaji nakadhalika.

utakuta hapa zinahusika wizara nyingi na kila wizara inahitaji kuweka mchango wake kwa wakati sahihi.

bila kuandaa mkakati wa kazi hiyo kwa kutumia wataalamu unakuta kila mmoja anafanya jambo lake kwa wakati wake. wa miundo mbinu akiliona kaweka miundo mbinu basi wa kutoa mikopo wala hana habari anahangaika na mambo mengine kwani kwake yeye kutoa mikopo huku akiangalia hataonekana kama amefanya kazi hivyo na yeye anavipa kipaumbele vitu ambavyo kwake vitaonekana.

mwisho wa siku hakuna mpango unaokuwa umekamilika ili kutekelezwa mpaka mwisho bali huyu anashika hiki wenzake wako katika mambo mengine na yeye akihamia katika mambo mengine wameenda kwingine. huko ndiko kutokuwa na mipango.

mipango ni kusema tunafnya moja mbili tatu kwa kuangali hizo tatu ndizo zenye tija kwa wakati huo na kila mmoja ana play role yake.

kila mmoja anapimwa kwa kuangalia ametimizaje role yake katika yale tulitompangia.

mipango hii haiwezi kupangwa majukwaani na wanasiasa na ndio maana nasema wanatakiwa kusimamia plans za wataalamu.

wao wakiona jambo moja walibeba hilohilo tu mfano kama wafugaji ni masikini ama aliyeko kwenye kilimo atadhani wanakuwa masikini kwa kuwa hawalimi na kuanza mpango wa kuwalimisha. au aliyeko kwenye mifugo atadhani wakiongeza mifugo watatajirika na kuanza kuwahamasisha kupunguza au wa mazingira atasema mifugo ni mingi na ipunguzwe si kwa kuandaa mpango wa kibiashara bali anaandaa mpango wa hasara.

hawa wakae chini wawasikilize wataalamu wawaambie wewe utaanza kwa kufanya hili, yule atafanya lile, kukishafanyika haya kutatokea demand ya kitu fulani na hapa watahusika fulani na fulani kufanya haya na haya, haya yakishafanyika kutatoke haya na yatakabiliwa hivi.

hivyo kusema tuwaache wanasiasa wafanye wanavyotaka ni kuukumbatia umasikini

.
Nchi haiwezi ishi bila wanasiasa.Wanasiasa kazi yao ni coordination.Wanacoordinate wataalamu wote wa fani tofauti wafanye kazi towards a common goal.Sababu ukiachia kila mtaalamu mmoja afanye vyake nchi itaenda kama gari la mlevi.

Mwanasiasa ndiye kiunganishi cha wote.Wawe mainjinia wa barabara,madaktari,walimu.maprofesa,wanajeshi nk ndiye muweka mikakati ya namna gani hao wote wafanye kazi wafikie lengo moja.Ukiondoa wanasiasa ukabakiza wataalamu pekee nchi haitaenda
 
Back
Top Bottom