Ili CCM ishinde 2015 ifanye hivi

Mkuu umenichosha kabisaaa, inakuwaje watu tumewaamini kwa miaka 50 wameshindwa kudeliver, kama nchi tunazidi kurudi kwenye ujima badala ya kuendelea. Elimu, Viwanda, kila kitu ni ziiiiiii. Bado tu unawapa ushauri waendelee kupata ridhaa yetu kutudidimiza kwa nguvu zaidi. Tunahitaji mabadiliko mkuu!
 
Ni kweli lakini wasi wasi wangu wakifuata ushauri wako wataiweka CDM katika hali ngumu 2015.
 
Watu wamechoka maeneno ya CCM ,,,watu wanataka action tu,Na chama cha ccm kimeshatamka kamwe hakitomaliza matatizo haya,ugumu wa maisha,umeme,maji safi,huduma ya afya,ajira,kikwete mwenyewe ndio mkuu wa chama hicho ametamka katika televison nini tutarajie ????????/

Chama cha ccm hakitaki challenge kutoka kwa wanachi wala kwa vyama vyengine vya siasa katika kujenga nchi vipi tutafika ? KWANI wao nio wameumbika peke yao ?

Hawa hawana lolote,cha kufanya CCM wabadili sera yao ya kikoloni ya kuwanyonya wananchi,wabadili katiba tena kuundwe taifu huru la tanganyika ili serikali hiio wananchi wawe na imani nayo kwa sababu zanzbar hawana imani na neno tanzania limekuja kiusanii hii peke yake ndio kero kubwa katika muungano na ndio chama kikajaa wasaniii ...

Sojenga hii nchi kuundwe taifa huru lirudishwe lile la tanganyika ,pia tuache tabia ya kurithishana uwongoziiii leo mtoto wa kikwete raisi,kesho mtoto wa mwinyi,kesho kutwa wa mkapa,haya ndio wanayopinga north africa.

Tujenge nchi basi tuwe tayari kushirikiana na wananchi na serikali ijali zaidi wananchi kuliko kujali viongozi kama wabunge na kuwapa posho kubwa na kuwapa bima za afya za ulaya wakati wananchi maisha magumu ajira hakuna,elimu duni bado mabanda ya mbuzi tunatumia,wanakaa chini watoto,vitabu hawana,umeme kila siku mgaooo,haya yote yataisha lini ?

Ulaya mbona yameisha jamani,,nusu karne ccm imeshindwaaa
 
Big up Bro.!
CCM wanahitaji ku-pay attention ili kuepuka msiba utakaowakumba. Baadhi ya viongozi wao wanajibu hoja kama kina mama wa uswahilini wanapashana. Usishangae K/Mkuu kusikika akisema maoni yako ni kelele za Chura ambazo hazimzui ng'ombe kunywa maji. Bora kutimiza wajibu wako kwa kuwashauri anyway.
Amini! wanasiasa walivyo wa ajabu, Muda huu hawasikii la mtu lakini watakaposhindwa kuchakachua 2015 watang'ang'ania madarakani na kutupeleka Kenya tuje kusuluhishwa na Museveni.
 
Sio siri Chama cha mapinduzi (ccm)kwa muda sasa hasa toka Nyerere aondoke duniani kimekua kikiteswa na mafisadi pamoja na ufisadi kiujumla.Zipo jitihada za hapa na pale zimefanyika ndani ya ccm hasa kwenye serikali hii iliyopo madarakani ambayo inamalizia muda wake wa awamu ya pili,mojawapo wapo ikiwa ni ile jitihada iliyoasisiwa na mwenyekiti wa chama hicho ikiienda na kauli mbiu mashuhuri ya chama "kujivua gamba" ufisadi.

Napongeza jitihada hiyo lakini ningependa chama kiende mbali kidogo kwa kufanya maamuzi magumu dhidi ya mafisadi papa kwa kuanzia ambao ndio wamekua wakikiyumbusha chama kwa kutumia mipesa michafu ya kifisadi na kujaribu kufifisha jitihada mbalimbali za chama kukisafisha na kujiondoa mikononi mwao.

Nashauri CCM kwa mfano Kinaweza kabisa kubadili kanuni za chama na pia kwa kutumia political power na ushawishi kilionao kwa serikali kuweka katika tume ya taifa ya uchaguzi kuwa mtu yeyote narudia tena yeyote aliyewahi kujiuzulu madaraka yake kwa kashfa ya ufisadi hata kama ilikua tuhuma tu lakini ikapelekea kujiuzulu kwake haruhusiwi kugombea uongozi mpaka ipite miaka 15 let say tangu kujiuzulu kwake.Hapo wakifanya hivyo nadhani yatakua yametimia wala kina Nape hawatakua tena na kazi kubwa ya kubishana na Jackton Manyerere,Absalom kibanda,said kubenea,Muhingo Rweyemamu wala Deo Balile kuhusu tafsiri sahihi ya "kujivua gamba".

Nawasilisha.
 
Lowassaphobia ni ugonjwa hatari sana!Sasa kweli nimeamini hakuna kama Lowassa ktk siasa za nchi hii kwa sasa. Yaani unataka CCM iishawishi NEC ibadili kanuni zake ili kumdhibiti Lowassa! Kila siku huwa nakuambia CCM hamumuwezi Lowassa kwa lolote naona sasa umeikubali hoja yangu. Lowassa ndiye rais ajaye wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mzanzibar kamwe hawezi kuwa rais wetu huku Bara.
 
JK and NAPE are birds who hates faeces but feeds on maggots!
 

Mbona unaweweseka kijana,mimi nimetupa jiwe gizani ....!
 
Nani atamdhibiti nani wakati wote ni waovu!

Uchaguz mkuu ujao sisiyem wasishiriki ktk uchaguzi mkuu ujao ktk ngazi zote ili wajipange! Mafisadi watajiondoa automatic kwani wataona hakuna DILI!
 
Mbona unaweweseka kijana,mimi nimetupa jiwe gizani ....!
Sasa mbona wewe ni wa kwanza kupiga kelele! Jiwe la Lowassa limekupata nini? Kwa sababu Lowassa hata bado hajatangaza nia ya kugombea urais wewe na CCM yako tayari mmeanza kuweweseka.
 
Sasa mbona wewe ni wa kwanza kupiga kelele! Jiwe la Lowassa limekupata nini? Kwa sababu Lowassa hata bado hajatangaza nia ya kugombea urais wewe na CCM yako tayari mmeanza kuweweseka.

mzee una tatizo la kupenda kuchangia mijadala bila kusoma kwanza hasa unapokua japo unahisi tu kwamba lowassa anaumizwa na mjadala husika,hebu soma sawasawa thread ni wapo huyo lowassa wako katajwa?

N a pili ni wapi "urais" umetajwa???

Au kwako wewe uongozi ni urais tu na ufisadi ni lowassa tu?

si ni wewe ndio ambae kila siku umekua ukidai lowasa atakua rais wakati mimi sijawahi kumsikia akitamka kugombea,tukuulize wewe nani amekwambia lowassa atachukua fomu za kugombea?

Kama hujatumwa na mtu kuja kuzua hiyo taarifa je lowassa anaweza kuwa rais tu bila hata kugombea huo urais?
 
Vice versa is true! Daima nyani huwa haoni kundule.
 
Vice versa is true! Daima nyani huwa haoni kundule.

acha maneno ya kwenye khanga lete hoja zenye ushahidi wapi katajwa huyo lowassa wako?au uongozi kwako ni urais tu?

au ufisadi maana yake ni lowassa hapa tanzania?

na kwanini unamtangazia lowassa kugombea urais kwanini asitangaze mwenyewe?anaogopa nini au ni kweli yuko mahututi hivyo familia yake imekuteua wewe kuwa msemaji wake ?
 
Mbona unakikimbia kivuli chako?
 
Mbona unakikimbia kivuli chako?
Leo huna hoja nimekushika pabaya,unapenda sana kumuongelea lowassa tatizo,hata asipotajwa unamchomeka ili uonekane unafanya sana kazi kuliko wapambe wake wengine au?
 
Leo huna hoja nimekushika pabaya,unapenda sana kumuongelea lowassa tatizo,hata asipotajwa unamchomeka ili uonekane unafanya sana kazi kuliko wapambe wake wengine au?
Nipe break fupi, nitarejea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…