wengi wetu tunalia bunge kugawanyika kwa makundi ya kivyama na kuweka maslahi ama yao mbele au vyama vyao mbele na kuacha jukumu la msingi la kusimamia na kushauri serikali.
mimi naamini tukiacha kuonyesha bunge live tutaondoa mbwembwe za wabunge bungeni ambazo nyingi huwa si za kusimamia serikali bali huwa ni za kujiimarisha mbunge mwenyewe au chama chake.
ili bunge liwe kitu kimoja ingefaa tupate taarifa ya jumla kama ilivyokuwa sakata la lugumi ambapo tulikuwa tunasikia kamati ya bunge na jeshi la polisi.
bunge linatakiwa liwe na msimamo mmoja katika mambo ya kitaifa.
tukisikia bunge limepongeza serikali kwa hatua mbali mbali inazozichukua kurekebisha hali fulani na kushauri njia ya kufanya mambo hayo yawe endelevu tunajua wabunge wetu wanafanya kazi.
tukisikia kwa ujumla wao wabunge wameibana serikali kuwa hapa inachokifanya inawaonea wananchi tunawahukumu kwa ujumla wao.
kupata kura tena kutategemea pia juhudi zake binafsi katika jimbo si katika kutoa misaada binafsi bali kuisimamia serikali katika ngazi ya jimbo na kuwa karibu na wananchi wakati wote.
sote tumekuwa tukilia bunge letu kuwa kitu kimoja, lakini hatutambui kuwa moja ya jambo linaloligawanya bunge ni kuruhusu wabunge hawa kufanya kampeni kwa wapiga kura wao kutumia mijadala ya bunge.
nadhani tusipoonyesha bunge live tunawalazimisha wabunge wote wajaribu kulifanya bunge liwe na matokeo yenye sura ambayo wananchi wanapenda lakini matokeo haya ni lazima yawe na tija kwa taifa.
ipo miradi mingi ni kwa ajili ya maendeleo ya taifa lakini katika kutekeleza miradi hiyo wapo wananchi ambao wanaweza kuathirika na wabunge hawa wakati mwingine wamekuwa wakipinga maendeleo ya nchi kwa kutetea wapiga kura wao ili kulinda kura zao.
wakati mwingine wamekuwa wachonganishi, mtu anaenda na swali la kuchonganisha maana mfano yawezekana ili kuweka ustaarabu katika miji wanaweza kusema pikipiki, ice ndogo haziendi katikati ya mji. mbunge anaelewa hilo lakini kwa chokochoko za kisiasa anaenda kumuuliza waziri live ni lini boda boda wataruhusiwa kufika katikati ya mji.
hapa inakuwa ni hoja ya mpango wa maendeleo lakini kwa kujua akisema hawaruhusiwi kuingia mjini basi hawa wanaendelea kuwa nyuma yangu na wakati mwingine wapanga mipango nao wanakuwa wadhifu mbele ya kupoteza kura anaamua kuweka uholela na kukiuka mipango ya maendeleo kwa kuruhusu kuingia mijini hovyo. wataalamu waliokaa na kuandaa mipango ya maendeleo wanabaki wakishangaa na kudai wanasiasa wanavuruga lakini hawajui tunawapa wakati mgumu wa kufanya maamuzi kwa kuchagua baina ya kura na mipango ya wataalamu wakati wataalamu wenyewe hawana kura za kutosha kuendelea kuwalinda. kwa bahati mbaya mipango yao jamii huwa haioni faida zake mpaka imetekelezwa na kuonyesha matunda ndio jamii huja kujua kumbe fulani alitusaidia wakati huo wapiga kura walisha maliza kazi yao mda mrefu.
kuonyesha bunge live tunafanya wagawa perembe kuonekana wazuri mbele ya wapiga kura kuliko watu wanofuata utaalamu kwa kuwaambia wananchi wafunge mikanda leo kwa kunywa maji tu ili kesho waishi kama wafalme.
hatuwezi kupata maendeleo kwa kuruhusu mgongano wa maslahi katika kujadili kwa mantiki ya kuisimamia serikali na kuishauri tukategemea tija.
waulizane huko kama mhusika alikuwa hajui apewe maelezo na wataalamu aelewe huko na mipango ya maendeleo haivurugwi na siasa.
yawezekana wapo wanaongalia live kama njia ya kufanya wabunge kuwajibika lakini kiukweli tunaingiza ushabiki ambao tunapoteza zaidi kuliko faida kwa kuonyesha live.
rahi yangu ni wabunge tuwahukumu kwa matokeo ya mijadala ya bunge. wao wanatakiwa kusimamia serikali, hivyo wao kwa umoja wao kuonekana wanaisimamia serikali ndio bunge letu kuonekana linawajibika na sio kuruhusu sisi kugawanyika katika makundi tukishangilia bunge huku ni sawa na timu ambayo kila mchezaji akipata mpira hatoi pasi kwa wengine anapiga chenga nyingi ili mashabiki wamshangilie lakini kukosekana kwa timu nzima kucheza kitimu timu inafungwa.
kama tukijigeuza kushabikia matokeo ya timu nzima, unakuwa unawalazimisha wachezaji wote kushirikiana kutafuta matokeo mazuri kwa timu maana hayo ndiyo yanawapa sifa kila mmoja wao.
na hapa tutambue majukumu ya mbunge ni yapi ili wale walioko katika chama tawala wasije kujishikiza katika mambo ambayo serikali inatenda.
serikali ina majukumu yake na bunge lina majukumu yake.
wananchi waelimishwe jinsi ya kutambua wajibu wa mbunge na kama anatekeleza na wajibu wa serikali na kama anatekeleza ili ikifiika uchaguzi sio wote waliokuwa wamelala na waliokuwa wanafanya kazi kwa maana ya bunge na serikali wanakuja eti chama chetu kimefanya vizuri au kipe kura chama chetu.
kwa wabunge tuwapime kwa matokeo ya jumla ya bunge na kila mbunge katika jimbo lake wampime kwa kutimiza wajibu wake.
tusiwaruhusu wabunge hawa waendeleze tabia zao za kutoka kwenye biashara zao wanaenda bungeni na wanatumia mijadala ya bunge kuonekana wanatekeleza majukumu yao kwenye majimbo. wanatafuta safari za kwenda kutembelea kwao mara moja kwa kutafuta misaada binafsi? hivi wakati haupo jimboni mwananchi ambaye serikali inamuonea kwa kumkadiria kodi kubwa na hakubaliani nayo aende kwa nani? barabara iliyojengwa katika jimbo nani anafuatilia serikali kama wanawajibika? kama watoto hawana walimu mashuleni au walimu hawafundishi hivi wazazi hawa wamuone nani ili akalifuatilie hili kwa afisa elimu wa sehemu husika? hivi wananchi hawa wanapokwenda hospitali wakakalishwa kwenye mabenchi kama una ndugu yako huko ndio anakushika mkono unapita kupata huduma hivi haya mpaka mbunge akalalamike bungeni au haya ni mambo ya mbunge huyu kufuatilia katika jimbo kwa kuwaona viongozi wa serikali ngazi hiyo ili wafuatilie na wakishindwa ndio anakwenda bungeni kulalamika kwa ngazi taifa ili ilete msukumo kutoka juu.