Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,440
- 1,029
Jamaa watatu walienda guest.Walipouliza bei ya chumba,waliambiwa ni sh.30000 kwa chumba kimoja.Wakaamua kuchanga kila mmoja sh.10000 wakamkabidhi mmiliki wa guest.Mmiliki wa guest alipofika ndani akagundua bei si 30000 bali ni 25000,akatoa buku tano akampa mhudumu awarudishie wale jamaa.Mhudumu akutaka shida,akatia buku 2 mfukoni na ile elfu tatu akawapa wagawane buku buku.Kwa hiyo kila mmoja akawa amelipa elfu 9 yaani elfu 27 kwa wote watatu.Ukijumlisha na ile elfu 2 aloficha mhudumu ni sh elfu 29.Swali.je shilingi elfu moja imeenda wapi?