Ilani ya CCM yadanganya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilani ya CCM yadanganya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 15, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0  Ilani ya CCM yadanganya

  Ilami ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2010 imesheheni takwimu zinazoikinzana, imegundulika.

  Katika ilani hiyo, ambayo anatumia mgombea Jakaya Mrisho Kikwete kuomba ridhaa ya kuendelea na urais, inaelezwa kuwa uchumi umekua kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005 hadi asilimia 6.7 mwaka huu.

  Lakini takwimu za serikali na washirika wake – Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zinaonyesha kuwa kiwango cha asilimia 6.7 kilifikiwa mwaka 2005 na siyo mwaka huu.

  Hata kiwango cha asilimia 4.5 ambacho inadaiwa ndicho utawala wa kikwete ulianza nacho mwaka 2005, hakipo, kwani tayari wakati huo, serikali iliyokuwa inamaliza ngwe yake ilikuwa tayari imefikia asilimia 6.7.

  Kwa hiyo, ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka huu ilipaswa kuonyesha utendaji wa serikali – kufaulu au kushindwa – kuanzia asilimia 6.7 kwenda juu au kurudi chini. Haifanyi hivyo.

  Ripoti ya WB ya mwaka 2007 kuhusu biashara na uchumi nchini ilisema, “…..uchumi wa Tanzania ulikuwqa ukikua kwa wastani wa asilimia tano hadi sita katika kipindi cha kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

  Basil Mramba, aliyekuwa waziri wa Fedha katika serikali ya Mkapa, aliuambia mkutano wa mwisho wa Bunge la bajeti (2005) mjini Dodoma, kwamba “uchumi wa Taifa umekua kwa asilimia 6.7.”

  Alisema, “mheshimiwa Spika, utawala wa Awamu ya Tatu umepata mafanikio makubwa ya kiuchumi. Kwa mfano, uchumi umekua kutoka asilimia 4.2 mwaka 1996 hadi asilimia 6.7 mwaka 2005.”

  Kwa mantiki hii, miaka mitano ya utawala wa Kikwete imekuwa ya makitaimu; bado uchumi uko palepale alipouacha rais mstaafu Benjamin Mkapa. Hii ina maana Kikwete ameshindwa kuinua uchumi wan chi……..

  Habri zaidi katika Mwanahalisi la leo.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Anajua fika mamilioni ya mambumbumbu anaotaka wamrudishe mjengoni hawajui chochote -- kitu cha uongo au cha kweli. Wao wamepumbazwa na sura tu!!!!!!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hawana hata aibu kucheza na tarakimu za uongo! Sijui hawa CCM uongo utawafikisha wapi! Mwaka huu watajibeba tu!!
   
 4. p

  pierre JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmmmmmmmmh.Hii kali,kumbe tumekuwa tukidanganywa miak yote?.Wanaona watz ni mazezeta wasiokuwa na kumbukumbu.Shame on CCM.Kwa nini lakini mdanganye ni ili iweje?Kwani mkiwa wakweli nani atawahukumu??Kweli huu ni usaniii wa hali ya juu,watu wenye akili zao wanazidi kushabikia huu ujinga wa kudanganya wananchi?Shame upon you wasomi mlioko CCM.
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,602
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  Ni kaw3aida yao hawa!!
  Ndiyo maana mambo ya msingi wanaenda kuongea na vizee vya dar badala ya kuongea na wahusika.
  wanajua fika hawana jipya wala la maana la kuongea na watu makini!
   
 6. b

  bwanashamba Senior Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiongozi kama una data nzuri kama izi yakubidi ujitnkeze na uzungumze kwa uwazi zaidi,unaweza ukawa msaada zaidi
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 10,644
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  hii ndiyo ccm iliyokwisha kuchakachuliwa na akina makamba
   
 8. D

  Dopas JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,150
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kikwete anadanywa katika mambo madogo tu ambayo hayahitaji kutumia nguvu nyingi ya kufikiri, itakuwa haya ya kuchambua kwa kina ukuaji wa uchumi wa Nchi! Japo hata katika hili hatumsamehe kwa sababu ana wataalamu wa sekta zote wanalipwa na kodi za wananchi maskini ambao inawabidi wakaze mikanda ili waweze kulipa kodi.

  Hata mzee wa kijijini ambaye hajasoma hata darasa moja hadanywi mara nyingi namna hii katika masuala yahusuyo familia yake na vitegemezi vyake. Nina mashaka na elimu ya JK, hivi kweli alifika Chuo Kikuu na kufuzu kwa kichwa chake au alibwewa bwebwa.

  Lakini inawezekana hili la ukuaji wa uchumi amegeuza namba hizo makusudi ili asiabike. Kama ukuuji wa uchumi 2005 aliukuta 6.7, na kaurudisha hadi 4, atajiteteaje? Tuna bahati mbaya sana kuwa na kiongozi wa ngazi ya juu wa namna yake. Kwa vyovyote wajanja walimsoma ndo maana rasilimali za nchi zinaibwa mchana kweupe.

  Mwaka huu inafaa kuondokana na mzigo wa viongozi wasio na 'akili', ambao wanaweza kutuletea matatizo makubwa sio kwa vile wanataka bali kwa vile ni wajinga na hudanganyika kirahisi. JK, simtukani, ila ni mjinga. Mtu mzima mwenye akili zako huwezi kudanganywa mara nyingi namna hii kama sio mjinga.

  Kwa kwakeli wanaJF, tusaidiane kuwahamasisha watanzania ili waelewe hatari kubwa inayoinyemelea nchi yetu ikiwa tutaendelea kuufumbia Macho ujinga wa viongozi wetu unaoendelea kuifilisi nchi.

  Itakuwa baraka kwa nchi yetu ikiwa baada ya 31.10 JK ataitwa rais mstaafishwa kwa 'kura' za wananchi wa awamu ya Nne.

  Kura zote za Rais kwa Dr. W. P. Slaa, na wagombea wa Chadema kwa Ubunge na Udiwani.
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Nimemsikia sasa hivi Katika Channel 10 yule Msomali Muuza nyara za nchi akimtetea Bi Salma kuhusu matumizi ya serikali -- kwamba eti serikali inalipa gharama ya ndege etc. Kwa nini asikodishe ATCL, Precision na nyingine ili kutuondolea utata woote huu? halafu akaja na takwimu kuonyesha serikali imeongeza usambazaji wa mbolea maradufu. Inahusu nini hapa? halafu tutajuaje kama hizo tarakimu zake siyo za uwongo kama vile zile katika ilani ya CCM ambayo huyo Muuza nyaara alishiriki kuitengeneza?
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,584
  Likes Received: 5,805
  Trophy Points: 280
  Serikali iliyokuwa inamalizia ngwe yake tayari ilikuwa imefikia asilimia 6.7 ya nini ? Hata ukisema ya uchumi mzima, uchumi mzima ulikuwa na ukubwa gani? Umepimwa kwa mwaka mmoja au miaka mitano? Asilimia ni fraction, unaposema asilimia ni lazima useme asilimia ya nini, ukuaji huu wa uchumi ungekuja kwa actual figures, kwamba uchumi umekua kwa dola kadhaa mwaka fulani, ambazo dola hizo ukizilinganisha kama sehemu ya uchumi ni asilimia 6.7 tungeelewa vizuri zaidi.

  Unaweza kujisifu uchumi umekua kwa asilimia 50, kumbe umekuza uchumi kwa kuuza bazoka 200, na kuongeza mapato kutoka shilingi mia moja mpaka mia moja na hamsini. Ukiangalia katika asilimia unaona kweli tumepandisha uchumi, asilimia 50 ni nusu nzima, lakini ukiuliza nusu ya nini, na kuambiwa nusu ya shilingi mia moja, unazimia mwenyewe.

  Hizi habari za asilimia zita confuse watu tu, wekeni asilimia halafu wekeni na actual growth in USD.
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,623
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ningekuwa mwalimu wako wa HISABATI ningekuchapa viboko 12.

  Naomba nitajaribu kukupeleka shule... Mfano huu hapa ili uelewe... kama uko ok kichwani.

  Mwaka uchumi ukuaji
  1995: x 5% of x
  1996: y=x +(5% of x) 4.5% of y
  1997: z= x+y 4% of z
  Sasa ndugu yangu... ukiangalia hiyo hesabu habo... unaweza kusema uchumi wa 1997 umepungua kukua but in reality inawezekana ikawa sio... inawezekana ndio umekuwa zaidi.

  Mwisho: Jiulize Kenya uchumi wa marekani unakuwa sio zaidi ya 4% in fact nadhani ni hata 3% does it mean haukui... sio kwenye 10% ya uchumi wa bongo can not be compared with 1% ya uchumi wa Marekani.
  Nawasilisha.
   
Loading...