Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendeleza juhudi katikakuhakikisha Sekta ya Madini inachangia kikamilifu katika kukuza uchumi na ajira.Kutokana na juhudi hizo, mchango wa madini katika Pato la Taifa umeongezekakutoka asilimia 3.3 mwaka 2010 hadi asilimia 3.5 mwaka 2014. Kuimarika kwa sektahii kumetokana na kufanyika mambo yafuatayo:-(a) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limewezeshwa kumiliki hisa kwenyemigodi ya STAMIGOLD (100%), Buchreef (45%), Buhemba (100%), Kiwira(100%), Tanzaniteone (50%), Tulawaka (100%), NDCLiganga (20%),Mchuchuma (20%), Ngaka Coal Projects (30%) na Mgodi wa Almasi waMwadui (25%);(b) STAMICO imeanzisha Kampuni iitwayo Kyerwa Tin Company Limited (KTCL) ilikununua madini ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini hayo hukoKyerwa. Hadi kufikia Machi, 2015 jumla ya tani 71.3 zimenunuliwa kwagharama ya Shilingi 1,106,326,000. Aidha, tani 30 zimeuzwa kwa Dola zaMarekani 201,000;(c) STAMICO imefanikiwa kupata kandarasi nne (4) za uchorongaji na utafiti wamadini yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.35 ambapo jumla ya ajira mpya 78zimepatikana kutokana na upatikanaji wa mashine za kisasa za uchorongaji;27(d) Ofisi mbili za madini za Kanda zimeanzishwa; moja katika Kanda ya ZiwaNyasa inayohudumia Mikoa ya Njombe na Ruvuma; na nyingine kanda ya Ziwaambayo inahudumia Mikoa ya Mara na Simiyu ili kusimamia na kudhibitibiashara ya madini. Kuanzishwa kwa ofisi hizo mpya kumeongeza idadi ya ofisiza Kanda kufikia kumi (10) na hivyo kuongeza ufanisi kwa wadau wa sekta hii;na(e) Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) umeendelea kuwezeshwa kwa kupatiwafedha na vitendea kazi ili kuimarisha utendaji kazi wake. Katika kipindi hichoWakala wa Jiolojia amepata mafanikio yafuatayo:-(i) Mfumo wa utunzaji, uchakataji, na usambazaji/uuzaji wa takwimu nataarifa za upatikanaji madini ili kuvutia uwekezaji umeboreshwa;(ii) GST imejiunga na COSOTA ili kusajili machapisho yake na kupewa hakimiliki (Copyright);(iii) GST imejenga maabara ya kisasa ya kuchunguza miamba na madinibaada ya kununua vifaa muhimu na vya kisasa; na(iv) GST imefanikiwa kufanya ugani na uchoraji wa ramani za upatikanaji wamadini (geological and mineral occurrence mapping) kwa asilimia 92 yaardhi kavu ya Tanzania Bara.(f) Idadi ya leseni za madini imeongezeka hadi kufikia 37,261 mwaka 2015ambapo leseni za uchimbaji mkubwa ni 15; uchimbaji wa kati ni 380; uchimbajimdogo ni 33,131; na leseni za utafutaji madini ni 3,735. Watanzaniawanamiliki asilimia 70 ya leseni hizo, wageni asilimia 25 na asilimia 5 ya lesenihizo zinamilikiwa kwa ubia kati ya Watanzania na Wageni;(g) Wachimbaji wadogo wametengewa maeneo 25 yenye ukubwa wa kilometa zamraba 2,407 na jumla ya leseni 8,800 zimetolewa kwenye maeneo hayo;(h) Wachimbaji wadogo 10,000 wamepatiwa mafunzo ya huduma za ugani(extension services) katika nyanja za kutambua umbile na tabia ya mashapo,masuala ya utunzaji wa mazingira, utambuzi wa madini na uboreshaji wauchenjuaji madini;(i) Jumla ya Shilingi milioni 909.5 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo kamaruzuku;28(j) Mpango wa utunzaji mazingira katika maeneo ya uchimbaji wa madini (ModernEnvironmental Protection Plan) umeanzishwa na umewahamasisha wachimbajiwadogo kutunza mazingira na kuepuka kuchafua vyanzo vya maji;(k) Mikataba ya madini imepitiwa kwa lengo la kulinda maslahi ya nchi ambapobaadhi ya vipengele vimefanyiwa marekebisho ili mrahaba ulipwe kwa kiwangocha asilimia 4 ya mauzo ghafi ya dhahabu (gross value) badala ya asilimia 3 yamauzo halisi ya dhahabu (Net Back Value) iliyokuwa ikilipwa na wawekezajihapo awali;(l) Migodi ya Bulyanhulu, North Mara, Buzwagi na Geita imeanza kulipa ushuru wahuduma (service levy) kwa Halmashauri husika kwa kiwango cha asilimia 0.3ya mapato ghafi ya migodi hiyo badala ya Dola za Kimarekani 200,000zilizokuwa zinalipwa kwa mwaka;(m) Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) imeanzisha madawati yaukaguzi kwenye viwanja vya ndege vya Kimataifa ili kudhibiti vitendo vyautoroshaji wa madini nje ya nchi, hatua iliyowezesha kukamatwa madini yenyethamani ya Shilingi bilioni 15; na(n) Kamati Maalumu ya Kitaifa (National Local Content Committee) imeundwa ilikusimamia mikakati iliyowekwa na wadau kuhakikisha kuwa Makapuni yaMadini yanaongeza kiwango cha manunuzi ya bidhaa na huduma hapa nchinikwa lengo la kuongeza ajira na soko la bidhaa za ndani.35. Katika kipindi cha 2015 hadi 2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekezaSerikali yake kutekeleza mambo yafuatayo ili kuendelea kukuza Sekta yaMadini na kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa:-(a) Kuweka na kusimamia mfumo thabiti wa kukagua shughuli za migodi,kukusanya takwimu za madini na kufuatilia maduhuli yatokanayo na madinikwa malengo mapana ya kuongeza mapato ya Serikali;(b) Kuweka na kutekeleza mikakati madhubuti ya kuvutia mitaji ya uwekezajikatika Sekta ya Madini, hususan kwenye madini adimu (Rare EarthElements - REE);(c) Kuhamasisha uzalishaji na masoko ya madini ya viwandani;29(d) Kuweka miundombinu muhimu (umeme, simu, maji, barabara) kupitiaushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi (PPP) kwenye maeneo yenyeuwezekano wa kuanzishwa kwa migodi mikubwa mipya;(e) Kuboresha mfumo wa utoaji na usimamizi wa leseni za madini, naupatikanaji wa taarifa muhimu kwa wadau kuhusu Sekta ya Madini;(f) Kuimarisha udhibiti na usimamizi wa upatikanaji, utunzaji, usafirishaji namatumizi ya baruti katika shughuli za migodi;(g) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili liwezekushiriki kikamilifu kwenye shughuli za utafutaji, uchimbaji na utoajihuduma katika Sekta ya Madini kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote;(h) Kuendelea kuujengea uwezo wa kifedha na rasilimali watu Wakala waJiolojia Tanzania ili uweze kufikia kiwango bora zaidi katika ukusanyaji watakwimu na taarifa muhimu za kijiolojia na kijiofizikia zitakazosaidia katikakuchochea kasi ya utafutaji na upatikanaji wa mashapo ya madini hapanchini yanayoweza kuchimbwa kwa faida;(i) Kuendelea kuujengea uwezo Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania naOfisi za Madini Mikoani ili zijiimarishe katika kukagua na kusimamia shughuliza uzalishaji na biashara ya madini nchini, na hivyo kuongeza manufaayatokanayo na Sekta ya Madini kwenye uchumi;(j) Kusimamia na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za uongezaji thamanimadini ili kukuza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa;(k) Kubuni na kutekeleza mikakati mahsusi itakayowezesha kupunguza aukukomesha kabisa vitendo vya utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi nabiashara haramu ya madini nchini;(l) Kuweka na kutekeleza mikakati maalumu itakayowezesha soko la Tanzanitehapa nchini kuimarika zaidi na hivyo kuongeza manufaa yatokanayo namadini hayo yanayopatikana Tanzania pekee;(m) Kuwawezesha wachimbaji wadogo kujiajiri kupitia sekta hii kwa kufanyayafuatayo:-30(i) Kuwatambua, kuwarasimisha na kuwapatia maeneo ya uchimbajimadini;(ii) Kuwapatia ruzuku, mafunzo, teknolojia na maarifa ya kisasa kwa ajiliya kuendeleza shughuli za uchimbaji;(iii) Serikali kupitia STAMICO kwa kushirikiana na wachimbaji wakubwakuwawezesha kupata mikopo na masoko; na(iv) Kuendelea kuongeza na kuwekeza mtaji wa Benki ya Rasilimali (TIB)ili iweze kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo.(n) Kuendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi katika masuala ya usalama,utunzaji wa mazingira na afya migodini; na(o) Kuhakikisha migodi yote mikubwa nchini inaendelea inanunua huduma nabidhaa kutoka hapa nchini kwa kiwango cha kuridhisha kwa kadri yaupatikanaji wake.