Ilani 2010-2015 chadema vs ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilani 2010-2015 chadema vs ccm

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Njowepo, Sep 3, 2010.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  ILANI YA CHADEMA 2010-15
  Ichi kibwagizo kama ni kweli JK hayuko serious “Hivi karibuni Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete, aliulizwa na waandishi wa habari wa
  Jijini Paris, Ufaransa kwamba “Nchi yako ina utajiri mkubwa wa maliasili, inakuwaje
  Watanzania ni masikini wa kutupwa hata mimi sijui sababu; ninajiuliza kila siku swali hilo lakini sijapata jibu!’’
  UFISADI NI NINI?
  Kwa msisitizo neon ufisadi limetumika sana wakimaanisha
  Tunapozungumzia Ufisadi tunazungumzia mfumo na muundo wa utawala ambao
  umetengeneza utamaduni wa kuishi kiujanja ujanja, matumizi mabaya ya madaraka na
  vyeo, ufujaji wa mali ya umma, wizi wa fedha za umma, utaratibu wa kubebana na ajira
  zinazotegemea kujuana, na mahusiano ya watawala na watawaliwa ambayo msingi wake
  ni woga, vitisho, na kujiona watu wanastahili zaidi kuliko wengine.
  ELIMU
  Takwimu cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, idadi ya wanafunzi wanaofaulu
  katika madaraja ya I, II na III kimeshuka kutoka asilimia 37.8 mwaka 2004 hadi asilimia
  17.8 tu mwaka 2009. Aidha, idadi ya wanafunzi wanaofeli kwa kupata Daraja la 0
  (Division 0) imeongezeka kutoka asilimia 8.5 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 27.49
  mwaka 2009
  MY TAKE:Ukienda ya CCM kwenye kipengele cha elimu wanaongelea kuongezeka kwa walimu,wanafunzi naona ni mwendo wa bora elimu na si elimu bora..
  KIBWAGIZO KINGINE
  Rais Kikwete, badala ya kuja na suluhu ya tatizo, anawalaumu
  watoto wanaopata mimba kwa kuwaambia kuwa wanapata mimba kwa sababu ya
  ‘kiherehere chao’ (Nipashe, Jumatatu, 07 Juni 2010).

  ON REASERCH
  Ili kuchochea ubunifu na kuviweka vyuo vyetu vikuu katika Nyanja za kimataifa,
  Serikali ya CHADEMA itaanzisha Baraza la Taifa la Utafiti (National Research
  Council)
  MY TAKE:Atleast itaamsha seriousness on R&D kama nchi bse maendeleo ya kweli huanzia kwa kufanya utafiti kabla ya kwenda step B.Ni kitu kizuli CCM wakaiga.
  VIFO VYA AKINA MAMA
  CCM iliahidi katika ilani ya uchaguzi wa mwaka 2005 kupunguza vifo vya akina mama
  kutoka vifo 278 katika akina mama 100,000 wanaojifungua hadi 132 kufikia mwaka
  2010. Hata hivyo, siyo tu kwamba wameshindwa kufikia malengo waliojiwekea, lakini
  pia, badala ya kupungua, vifo vya akina mama wajawazito vimeongezeka hadi kufikia
  292 kufikia mwaka 2009!
  CHADEMA itafanya nini?
  Katika kuimarisha huduma za afya zinazotolewa na sekta ya umma, Serikali ya
  CHADEMA itachukua hatua zifuatazo:
  • Katika mwaka wa kwanza wa serikali ya CHADEMA mpango wa ujenzi wa
  Hospitali ya Taifa ya Watoto (National Children Hospital)

  AJARI ZA BARABARANI
  Aidha, ajali za barabarani zimeendelea kuua watanzania wengi kila mwaka, na hakuna
  jitihada zinafanywa na serikali ya CCM katika kukabiliana nazo, zaidi ya kutoa salamu za
  rambirambi kila ajali hizo zinapotokea.
  MY TAKE:Tunarudi kwenye tatizo la msingi rushwa unasajiri gari yenye chasis ya scania 124 ya kubeba tani mpaka 40 kuwa ya kubeba abiriaIts merely lack of seriousness ya hao waosajili manake turudi nyuma aliajiliwaje?mshahara wake?allowances?mengi yanachangia.

  On ECONOMY
  Kwa ufupi, uchumi wa Tanzania ni uchumi uliolala (sleeping economy). Maana yake ni
  kuwa kile ambacho tunakiona kama ni shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini ni
  kiduchu tu ya kile kinachowezekana kufanyika katika taifa letu. Lakini zaidi ni kuwa
  uchumi wetu ni uchumi wa bandia (artificial economy).

  Kutokana na ukweli kuwa serikali imekuwa ikitenga kiwango kikubwa sana
  cha fedha katika posho ni muhimu serikali mpya kubadilisha utaratibu huo ili
  hatimaye kuinua mishahara ya watumishi wa umma. Kwa mfano, serikali ya
  CCM katika mwaka 2008/2009 ilitenga zaidi ya shilingi bilioni 509 (zaidi ya
  nusu Trilioni) kwa ajili ya posho mbalimbali. Hii ni sawa na malipo ya mwaka
  mzima ya walimu zaidi ya 109,000!

  Malengo ya MKUKUTA I ilikuwa ni kupunguza tatizo la ajira kutoka asilimia 12.9
  mwaka 2000/2001 hadi kufika asilimia 6.9 ifikapo mwaka 2010. Hata hivyo, hali halisi ni
  kwamba tatizo la ajira limepungua kwa asilimia mbili tu kutoka asilimia 12.9 hadi
  asilimia 11 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2010.
  MY TAKE:We need to be like Asian tigers zilikuwa nchi masikini kwa sasa wako mbali tukianza kwa kuondoa unnecessary posho either kwa kupandisha mishahara au allowances
  ON PAYEE
  Tutapunguza kodi ya pato itokanayo na
  mshahara(PAYE) kutoka asilimia 14 ya sasa hadi asilimia 10.
  MY TAKE:Inaonekana uti wa mgongo wa TRA ni PAYEE kuipunguza na kutafuta altenative sources za kupanua wigo wa kodi ni jambo la haraka just through brainstorming twaweza pata other sources.Mfano kwenye madini.

  WAZEE
  Wazee wote wenye umri wa kuanzia miaka 65 watapatiwa kadi maalum za
  vitambulisho ili waweze kupata punguzo la bei katika huduma na bidhaa mbalimbali pote
  nchini. Baada ya kulitumikia taifa lao wazee wetu wanastahili kupunguziwa mzigo katika
  masuala ya fedha.
  MY TAKE:Lazima tuchukue hatua madhubuti juu ya suala la wazee bse wengi wao kama akina Mramba wanajirimbikiizia mali bse hawajui uzee wao utakuwaje.
  HITIMISHO
  . Ilani hii inawezekana kutekelezeka kwani imezingatia uwezo wa ndani wa nguvu kazi, akili, vipaji, na uwezo wa kuongoza wa Watanzania wenyewe.
  CHADEMA inaamini kabisa kuwa endapo uongozi thabiti wenye maono makubwa ya mabadiliko unashika madaraka nchini basi kazi ya ujenzi mpya wa taifa letu itaanza upya kwa namna na mtindo ambao utalibadilisha taifa letu kwa haraka zaidi kuelekea mafanikio ya kweli na ya kudumu.

  Hatuhitaji chama kile kile, chenye viongozi wale wale, wenye sera zile zile
  zilizoshindwa. Hatuwezi kuendelea kuongozwa na nadharia kuwa maendeleo ni “wingi
  wa vitu” kama ambavyo serikali imekuwa ikifanya

  CCM 2005-10
  ITEM 45 G-kukamilisha ujenzi wa uwanja wa Songwe-MPAKA SASA UWANJA HAUJAKAMILIKA LABDA MWAKANI.
  ITEM 125 B Kuweka lami Iringa-dodoma-arusha-NIJUAVYO IRINGA-DODOMA MPAKA SASA HAMNA RAMI.
  MY TAKE:Haina yaliyomo wala hitimisho very unprofessional.Hakuna kinachoinadi kama ya CCM ie haina nembo ya chama/bendela.  CCM 2010-15
  13 F-VMchango wa Sekta ya Madini kwenye pato la Taifa umeongezeka
  kutoka asilimia 2.4 mwaka 2005 hadi asilimia 2.6 mwaka 2008.
  MY TAKE:Wakati katika masuala ya elimu wametoa takwimu mpaka za 2010 juu ya kuongezeka kwa mikopo kwa wanafunzi mpaka 243bilion toka 56 billioni madini zimeishia 2008 unaweza kuta pato kwa 2009 lilishuka ivyo ni aibu kuliweka.
  Alafu ongezeko la 0.2 nalo ni la kujivunia wakati kila kukicha tones and tones zaenda nje
  VII-Ajira katika uchimbaji mkubwa imeongezeka kutoka wafanyakazi
  7,000 mpaka 13,000.
  COMMENTS-Wangeweka na duration ya huko kuongezeka mfano toka 2008 to 2009 kwa nini hawakuwa specific kuna kitu apo kinakwepwa.
  15 B & C inaongelea elimu ya msingi na secondary wanaongelea idadi ya wanafunzi kiwango cha ufauru hawakiongelei bse in real fact kimeshuka asilimia 37.8 mwaka 2004 hadi asilimia17.8 tu mwaka 2009 KWA KIDATO CHA 1-IV
  33 Kilimo hawaongelei namna ambapo tutawakwamu wakulima wa matunda TANGA kwa kuanzisha viwanda vya usindikaji ili matunda yasiishie kuoza tuu.
  Inaongelea kuboresha kilimo cha umwagiliaji bila kuonyesha mikakati ya kufika uko
  34-D-Kujenga na kukarabati mabwawa ya kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua na
  mito kwa ajili ya umwagiliaji;
  34-F- Kutoa msukumo mpya katika uanzishwaji wa kituo cha mafunzo na
  shughuli za utafiti wa umwagiliaji na matumizi bora ya maji.
  35 SEKTA YA MIFUGO-Serikali iandae programu kabambe ya kuendeleza sekta ya mifugo na
  ufugaji.
  47-A- Kujenga Chuo Cha Utalii ili kuimarisha mafunzo ya hoteli na utalii kwa
  lengo la kuongeza wingi na ubora wa watumishi wa huduma hizo.
  MY TAKE
  Item 34 na 35 are Too general inawezekana ikawa makusudi bse wakiwa specific ni rahisi kuwaana next time kuwa hiki hamjatekeleza.

  63 WANAONGELEA HEP NA COAL ILA WA URANIUM HAUTAJWI WHY?
  67-J-Kupunguza Msongamano wa Magari katika Jiji la Dar es Salaam kwa
  kufanya yafuatayo:
  (i) Kujenga barabara za juu (fly overs) kwenye makutano ya barabara
  maeneo ya Ubungo na TAZARA.
  MY TAKE;Flyover pale magomeni nayo ni muhimu.Vile vile kuitanua morogoro road kuanzia ubungo mpaka angalau kibaha ili kuondoa msongamano
  GENERAL COMMENTS
  i. MISINGI YA UANDISHI HAIJAZINGATIWA KAMA YA CCM IKIWA HAINA YALIYOMO WALA HITIMISHO VITU AMBAVYO ARE SO BASIC KATKA UANDISHI
  ii. ILANI YA CHADEMA IS VERY SPECIFIC BUT CCM TOO GENERAL ILI ISIJE WAFUNGA
  iii. CHADEMA TALKS MORE OF BARA WHILE CCM TALKS OF BARA NA VISIWANI
  iv. KAMA MZALENDO WA NCHI CHAMA CHOCHOTE KIKICHUKUA NCHI PITIA ZURI TOKA KWA ILANI YA MWENZIO BSE LENGO NI KUJENGA NCHI YETU YA TANZANIA.KUMBUKA ILANI NI MAWAZO YA WATANZANIA
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Upande wa wafanyakazi anaongelea pia Scala Model ni system inayotumiwa na nchi nyingi na makampuni makubwa mengi.
  Mshahara unaongezwa kutokana na inflation rate prevailing at that time
   
Loading...