Ikulu ya Magogoni vs Ikulu ya Chamwino

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,901
PONGEZI SANA KWA RAIS JOHN MAGUFULI KWA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU YA KUHAMISHIA IKULU DODOMA.

Na Fredrick Mmari
+255 717 220707

Ikumbukwe mwaka 1891 Ujerumani iliitangaza Dar es Salaam kuwa makao makuu ya utawala wake.

Baada ya vita vya kwanza vya dunia 1914 -1918, Mjerumani aliondolewa kwenye utawala wa Tanganyika na nchi ikaendeshwa na Muingereza.

Mwaka 1920, Uingereza ilianza ujenzi wa Ikulu yake eneo lile lile walipojenga Wajerumani na kumaliza ujenzi huo mwaka 1922, mwaka ambao Baba wa Taifa letu Mwl. J.K Nyerere alizaliwa.

Mwaka 1956, Mwingereza alijenga jengo lingine pembeni ya eneo la Ikulu hiyo.

AWAMU YA KWANZA. Ilipofika mwaka 1968-1969, Mwl. J.K Nyerere alijenga jengo lingine na kufanya Ikulu kuwa na majengo makubwa manne.

AWAMU YA PILI. Kuanzia utawala wa Mzee Mwinyi miaka ya 1990 ikulu hiyo ilizungushiwa ukuta.

AWAMU YA TATU. Utawala wa Mzee Mkapa kuanzia miaka ya 1995 akaja kujenga makazi ya Rais Ikulu hapo.

AWAMU YA NNE. Enzi za utawala wa Kikwete kuanzia miaka ya 2005, Ikulu palijengwa ukumbi wa mikutano ujulikanao kama Kikwete Hall.

Hiyo ni historia fupi ya Ikulu ya Dar es Salaam.

Wakati wa Mwl. J.K nyerere alipendekeza makao makuu ya nchi yatoke Dar es Salaam na yahamie Dodoma.

Mapendekezo hayo yalitolewa 1971/73 na kushirikisha mikoa yote ya Tanzania.

Ipo mikoa iliyokataa uamuzi wa kuhamishiwa makao makuu mkoani Dodoma na kati ya mikoa iliyokataa Pwani ni mmoja wapo.

Mwaka 1977 maamuzi ya kuhamishia makao makuu Dodoma yaliazimiwa rasmi.

Awamu zote hizo maamuzi ya kuhamishia makao makuu kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma yalikua yanafanyika kidogo kidogo ila AWAMU YA TANO ndio yamefanya kwa haraka zaidi.

Hakika ni ujasiri mkubwa na mgumu ambao unahitaji gharama sana.

Leo 30/5/2020, Rais John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma akishirikiana na mama Maria Nyerere kwa niaba ya Baba wa Taifa (Mwl. J.K Nyerere), Rais wastaafu wakiwemo, Mzee Alhasan Mwinyi, Benjamín Mkapa, na Jakaya Kikwete.

Pia Mheshimiwa Rais Magufuli aliambatana na viongozi mbalimbali wa serikali,bunge,mahakama,jeshi na vyama vya siasa kwenye kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Ikulu ya Dodoma ambapo ndani ya miezi mitano Ikulu itakua imekamilika.

Ikulu ya Dar es Salaam na barabara zake ina eneo la hekari 41 na ya Chamwino ina hekari 8473.

Tayari ikulu ya Chamwino imeshazungushiwa ukuta wenye urefu wa kilometa 27.

HAKIKA HIZI NI JITIHADA KUBWA SANA NA ZA KUPONGEZWA ZINAZOFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO CHINI YA RAIS JOHN MAGUFULI.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

MUNGU NAOMBA UMLINDE NA KUMUONGOZA VYEMA RAIS WETU JOHN MAGUFULI.
 
Point of correction, Ikulu iliungua wing moja wakati wa mabomu ya WWI. Alichofanya Muingereza ni ukarabati mkubwa na wing ile ili pesa jina la mtoto wa Mfalme Geoge.
 
PONGEZI SANA KWA RAIS JOHN MAGUFULI KWA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU YA KUHAMISHIA IKULU DODOMA.

Na Fredrick Mmari
+255 717 220707
Hili swali ni miaka ishirini sasa sijapata jibu lake.: ''Kuna faida gani ya kuhamisha makao makuu kutoka Dar kwenda Dodoma ukitiliana maana ni gharama kubwa?''
 
Huu uwongo haukubaliki
Dogo taratibu punguza muhemko tunatumia ID fake siku ukigundua mi ni katibu mkuu wa chama chako kichovu utakunywa sumu??

Wengi tuko kwrnye chama chenu kichovu kwa ajili ya maslahi tu lakini akili na mioyo yetu IPO chadema, nakuibia siri na tupo wengi
 
Huu uwongo haukubaliki
Dogo sisi wengine hatuna chakupoteza tulishapata hela na maisha mazuri long time, tunaipinga ccm na uhuni wao ili tuwe na marndeleo endelevu. tunapigania demokrasia ili kila MTU awe na maisha mazuri kama sisi, hatukaki nchi iendeshwe kisanii, punguza ushabiki was kijinga wakati ndugu zako huko bush wanataabikaika
 
Hizo pesa nashauri zingetumika kukupelekea shule ili angalau ujue kuandika vizuri. Wewe upo lile fungu la lumumba buku 4.
 
Back
Top Bottom