Ikulu: Mashangingi sasa basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu: Mashangingi sasa basi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  FRIDAY, JUNE 22, 2012

  Boniface Meena na Fidelis Butahe

  OFISI ya Rais, Ikulu imesema Serikali itaanza kuwakopesha viongozi wake wa ngazi mbalimbali magari madogo ya gharama nafuu ili waachane na mashangingi yanayotumika sasa.  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliliambia gazeti hili kuwa mpango huo unaotarajiwa kuanza Julai mwaka huu, una lengo la kupunguza matumizi ya Serikali kwa kuondokana na magari makubwa yenye gharama kubwa za uendeshaji.


  Balozi Sefue alisema mpango huo unaanza katika mwaka huu wa fedha ambapo yatachambuliwa magari yanayofaa na yatapendekezwa yatumike katika shughuli gani.


  Alipoulizwa kama mabadiliko hayo yatawagusa mawaziri na majaji, Balozi Sefue alisita kulijibu hilo na badala yake alisema kuwa bado suala hilo lipo katika mjadala.


  "Hili jambo bado linajadiliwa, haya yote yatafanyika katika mwaka huu wa fedha," alisema Balozi Sefue. Mwaka wa fedha unaaza Julai mosi mwaka huu.


  Akifafanua zaidi alisema, "Kwanza tutatizama gari husika linatumia mafuta kwa kiwango gani, pia tutatizama hata gharama nyingine kama ufundi," alisema Balozi Sefue.


  Alisema kuwa utaratibu huo ukianza viongozi wanaotumia magari ya Serikali wataanza kukopeshwa magari hayo na kupewa posho kwa ajili ya kuweka mafuta.


  "Ni kipaumbele cha Serikali kuangalia hilo mwaka huu na hata katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13 imeelezwa wazi, lengo ni kupunguza gharama za uendeshaji," alisema Sefue.


  Aliongeza, "Badala ya kumpa mtu gari tunamkopesha halafu tunakuwa tunampa mafuta ili kupunguza matumizi Serikalini."


  Alisema katika uchambuzi huo wataangalia ni kiongozi gani atahitaji gari la Serikali na yupi atatakiwa kukopeshwa na kwamba hali hiyo itafuatana na kazi za mtumishi husika.


  "Tunaangalia hili la magari, lengo ni kuwa na magari ya aina fulani lakini si ya kifahari na tutawakopesha watumishi," alisema Sefue.


  Alisema kuwa katika uchambuzi huo pia watazingatia ubora wa gari husika ikiwa ni pamoja na kustahimili kusafiri masafa marefu, kulingana na majukumu ya mtumishi.


  "Yapo mambo ambayo Serikali imeyapanga na lazima yatekelezwe," alisema Sefue.


  Alipoulizwa kama mpango huo ni utekelezwaji wa mpango uliotolewa na Wizara ya Ujenzi mwaka 2004 wa kubana matumizi ya magari ya Serikali alisema hilo linaweza kutolewa ufafanuzi na Wizara ya Ujenzi yenyewe.


  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Herbert Mrango alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa mpango huo alisema hawezi kuzungumzia mambo ya Serikali kwenye simu.


  Wakati Balozi Sefue akisema hayo tayari kuna baadhi ya viongozi Serikalini wameshajikopesha magari hayo akiwemo Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu.


  Suala la Ndulu kujikopesha gari lilielezwa hivi karibuni na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe alipokuwa akisoma bajeti mbadala ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.


  Zitto alisema Serikali inatakiwa kupunguza mzigo wa matumizi ya magari ya Serikali kwa kupiga mnada baadhi ya ‘mashangingi' na kuweka mfumo wa kukopesha magari kwa watumishi wote wa umma wanaostahili magari kama alivyofanya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.


  Balozi Sefue alipoulizwa kuhusu suala la Ndulu kujikopesha gari alisema hajuI bali huo unaweza ukawa ni utaratibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT ndiyo ambayo inaweza ikawa imepitisha hilo.

  "Kwa maana ya framework hakuna kinachomzuia kufanya hivyo," alisema.  Katika mkutano wa 7 wa Bunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo alieleza kuwa kumekuwa na matumizi yasiyo ya lazima katika uendeshaji na ukarabati wa magari hayo na hadi Juni 30, 2010 Serikali ilikuwa inamiliki magari yenye thamani ya Sh5 trilioni.


  Alisema mwendelezo wa ununuzi wa magari unaofanywa na Serikali unaongeza gharama za uendeshaji na kusisitiza kwamba matumizi hayo si ya lazima kwa Serikali yenye uchumi mdogo uliozidiwa na madeni.


  Chanzo: Mwananchi
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Bravo... Wakati Umefika sasa lakini Wasiwasi wangu ni hao Maofisa hawatanunua Mashangingi Mlango wa Nyuma

  Kama Mchezo wa kawaida? Na Vipi IKULU? Wana BMW, BENZ na RANGE ROVERS (LAND ROVERS) Lini Rais ataamua

  Gari la Rais kutumia iwe Model Moja tu kama Maraisi waliomtangulia? kwasababu yeye ana fleet of different brands

  inaigharimu serikali mara dufu.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii Thread ilikuwepo asubuhi
   
 4. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  CHADEMA wanaendesha nchi... kitaeleweka tu
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hayo ni mazungumzo baada ya habari hakuna jibya hapo jumba bovu unapaka rangi ionekana mpya.... wameshachelewa watafute jingine
   
 6. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,384
  Likes Received: 6,563
  Trophy Points: 280
  rAV 4 ZINAWATOSHA hao mabwege vitambi
   
 7. D

  Danniair JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuwaheshimu walioanzisha web hii. Na si kutoa lugha zisizofaa kwa viongozi wetu, baba na mama zetu.
   
 8. D

  Danniair JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Elewa kuwa mkosoaji ni mpinzani. Kama hawafanyi hivyo tutawashangaa. Pia sidhani kama gavana ni mwana CDM, kwani ndiye amekuwa mtu wa mfano.
   
 9. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #9
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu,
  Nahisi kama mimi ndio sielewi maana ya Breaking News!
   
Loading...