Anatakiwa ajenge mazingira mazuri ya kidemokrasia nchini na ndani ya chama chake kwasababu mambo yameshabadilika...hata mwalimu naye alikuwa kwenye misuko suko mithili ya hii hivyo ulinzi wake na yeye mwenyewe alikuwa very cautios,na kipindi hicho ilikuwa wakati wa chama kimoja...Sasa yeye hajiulizi?
Kwanza hata wakati wa mwalimu kulikuwa na mafisadi na ufisadi ulikuwepo,lakini siri hazikufichuliwa kama ilivyo sasa kwasababu kulikuwa hakuna sababu za kisiasa kufanya hivyo,na pia zilikuwa ni siri za Taifa na kuzifichua ni kama uhaini...wakati huu kuna kila sababu za kisiasa za kufanya hivyo lakini mazingira hayaruhusu,bado mazingira ni kama ya chama kimoja kwa kiasi kikubwa na asipobadilisha mazingira lazima atakuwa hatarini zaidi....Na kama hataki kubadili mazingira basi ajiuzulu wengine wafanye hivyo,kipindi hiki si kama zamani....Mwalimu alianza lakini wengine badala ya kuendeleza kadri muda unavyozidi kwenda,wao wanarudi kinyume nyume na kufanya yale ambayo hata mwalimu mwenyewe hakuthubutu kuyafanya....Haya yanayomtokea sidhani kama ni mambo ya kawaida,kuna unrest ya hali ya juu ndani kwa ndani,na kama hawezi kufanya mabadiliko ya kweli ni bora ajing'atukie zake tu kama mwalimu ambaye aliruhusu vyma vingi kimachale machale na kuruhusu vyama vingi licha ya kutokutaka kufanya hivyo under his watch, kuliko kuendesha nchi kwenye mazingira kama haya ambapo wengi tunaona kama nchi imeshauzwa na wao hata hawajali....Pia asiwazuie wenzake kugombea eti ili amalize awamu ya pili,isue si mtu kumaliza awamu,issue hapa ni unawafanyia nini wananchi na unalifanyia nini Taifa?!
Waliyoyafanya mtandao mwaka 2005,hawawezi kuyafanya this 2010 halafu eti nchi ikaendelea kuwa na amani,asome alama za nyakati na abadilike accordingly,akicheza smart card atafanya hivyo,wananchi wana taarifa zaidi nyakati hizi kuhusu ufisadi na wanataka mabadilko lakini mazingira hayaruhusu,kama kuna wanamtandao ndani ya chama,basi pia kuna wazalendo ambao nao hivi majuzi tu wamenyimwa haki yao kuhusiana na ccj?!badilika Mh Rais acha kubandika pamba masikioni,mengi mabaya yenye mtiririko kama huu tumeona yanatokea...akiwa king'ang'anizi mi simo.