Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Gazeti maarufu nchini Marekani liitwalo Forbes, huwa halipendi kuwaheshimu matajiri wengi wa bara la Afrika. Sababu hasa ni ule uhusiano wa matajiri na wanasiasa wanaokuwa kwenye uongozi wa nchi. Mabilionea wa Afrika wengi wanazo mali ambazo kwa njia moja au nyingine zinao uhusiano na wao kupewa zaidi kipaumbele na wanasiasa (favoritism).
Malalamiko ya mwanasiasa mkongwe baada ya kutumia nguvu nyingi sana kiuchumi katika kutafuta uongozi, yananikumbusha ule mtazamo wa Forbes kuhusiana na matajiri wa kiafrika, ambao mara nyingi huwa na pato la kawaida ikiwa wakiwekewa mazingira magumu kwenye suala la wao kuwa karibu na uongozi wa kiserikali.
Urais unaposhindikana kwanini mtu asikubali kuwa mwanasiasa mkongwe mwenye ushawishi kwenye jamii?. Kwanini mwanasiasa awe ni yeye tu mwenye kuustahili urais, je haoni kama vile anakuwa anawadharau wale wengine ambao wamekubalika mbele ya wananchi?. Kwanini mtu uzeeke na uhasama moyoni eti kwa sababu ulichoota kukipata hujakipata?.
Sio wote wanaoandikiwa kuwa marais, ni jambo ambalo kama linafanikiwa unanyoosha mikono hewani na kumshukuru Mungu lakini likishindikana basi hakuna haja ya kukiona kama vile umedhulumiwa kitu ambacho ni haki yako ya kuzaliwa.
Forbes wapo sahihi kabisa kwa kutowapa vipaumbele mabilionea wa bara la Afrika. Wengi wao wanao utajiri usioweza kutenganishwa na umasikini pamoja kudhulumiwa kwa wanyonge wengi.
Hili suala la siasa kuununua uongozi na kuzalisha matajiri wenye kunuka uonevu linauhusu Tanzania pia na litaendelea kutuhusu kwa miaka mingi ijayo.