Ikulu kumjibu Lema...

Ikulu siku hizi haina maana maana kazi ya msemaji wa ikulu kama Salva hatakiwi kujibu kama anavyojibu kashfa mbalimbali zinazoiandama ofisi hiyo. Raisi hawezi kushutumiwa kwa lolote alafu salva anajibu kama alikuwepo. Kikwete alishutumiwa kuhongwa suti afadhali akanushe kwa alichose raisi anaongea maneno yake yeye. "Kumbuka Ikulu ni mahali patakatifu" uharamu wanaouleta hautawasaidia, tunajua hawawezi kukubali ila habari ndiyo hiyo.
 
Kweli hihi nchi inaongozwa kwa mipasho kashindwa kuongoza nchi, anapambana na Lema kweli wa Tanzania tumempata raisi
 
Jk na Salva wote walikua bado Arusha wamenipta maeneo ya KIA pale kama saa tisa hiv; sasa hao walouandaa huo waraka na kuutuma ni kina nani?
Kama Salva iweje autume tena si angempelekea tu akausome na aufanyie marekebisho?

Kama Great thinker usitake kutengeneza tu story ili utufurahishe umma basi kwa comments za kwenye vdole ungetupia hii kitu kwenye Chit chat au kwa wale wa gothip tungecomment kigothip"
 
Nadhani, uelewa mdogo
nao unachangia nchi sasa kuwa ya majungu na ushabiki usiyo na tija. Hivi
Salva anasakamwa kwa sababu ni msemaji wa Ikulu au kwa sababu yuko
katika nafasi ambayo wengi waliimezea mate na hawakuipata?

Naamini wewe ndie Salva mwenyewe hebu acha ujinga bwana watu wote sisi tungewezaje kuwa wasemaji wa ikulu!
Mtu hajui kazi hajui tu, umbwiga mwingine pembeni.
 
yani huko jikoni ikulu badala ya kupika mnasogoa kuhusu lema..kweli hamna kazi huko..
 
Nadhani, uelewa mdogo nao unachangia nchi sasa kuwa ya majungu na ushabiki usiyo na tija. Hivi Salva anasakamwa kwa sababu ni msemaji wa Ikulu au kwa sababu yuko katika nafasi ambayo wengi waliimezea mate na hawakuipata?


Pilipili usiyokula yakuwashiani?! wewe ni Salva au wakili wake! yaani this is typical excuse of the lazy; wengi wetu tunamkumbuka Salva enzi za Rai, Mtanzania na Dimba, akiwa na waandishi mahiri kama Jenerali, Bwire, Dr. Shoo, Johnson Mbwambo and the rest of the team iliyokuwa na Vison ya kizalendo kweli kweli, hawa watu walikuwa wanafuata nyayo na kumuenzi Muasisi wa taifa hili Mwl. Nyerere kweli kweli; tunamshangaa ni dhoruba gani ilimkuta mpaka akaamua kwenda kuwa SPIN DOCTOR wa utawala wenye maono tofauti kama mwanga na giza kulinganisha na yale tuliyokuwa tukimtabua nayo enzi za habari corporation; ndio maana great thinkers tunamfuatilia sana kwa karibu sio kumsakama lakini kuchambua maono na misimamo yake mipya akiwa SPIN DOCTOR wa serikali ya sasa compared to what he used to be na kuendelea kumuonyesha makosa yake kwa kadri inavyowezekana; a total let down.
 
Hivi kuna haja yoyote ya kumjibu Lema, yule si naye ni kama amechanganyikiwa? Nadhani inatokana na ukweli kwamba atakosa posho za vikao vya bunge ndiyo maana anaamua kutjipatia posho hizo kupitia majukwaa.

Miongoni mwa watu wanaotakiwa kuondoka great thinkers wee ni kwanza. Ni mvivu jufikiria kama cjui nini,in short you dont deserve dat title. You dont read books you cant increase your knowledge,you dont even know even about revolution, kukusaidia tu: wanaharakati wako hivyo, au nao huwajui?
 
haya Lema anatisha sana ndio maana anamfanya jk asilale hana rahana na uongozi ni kama Libya na Misri
 
.......nafikiri ziishie kuwa tetesi, kama Ikulu itajibu, kwa mtazamo wangu hiyo itakuwa hali ya chini sana,...
 
Sasa mkuu unayefanya kazi jikoni fanya mchakato unitumie namba yako nikupatie sumu ya panya uweke kwenye msosi wa mweshimiwa
 
Kama wanafikiri kwa kutumia jina la Mayor wa Darisalamu watamjibu Lema. Na ikitokea wakimjibu tu lazima Lema apasue kilichojiri kwenye kikao chao cha Oysterbei.

Wakinyamaza wamemuogopa, wakimjibu wanadhihirisha aibu ya kumnyang'anya ubunge.

Kweli Lema kawakamata kusini, kaskazini,mashariki, magharibi na centre.
 
Ikulu itasema jk hajawai kukaa wala kukutana na rais, na huo ni uchochezi na upotoshaji. Na lema atatakiwa kuomba msamaha kwa kumdhalilisha jk. Je::::je::je: lema atamuomba msamaha baba asha?
 
Hivi Ikulu wanaweza kujiingiza katika hali itakayotufanya wengine tushindwe kuwatofautisha na Lema kweli? sidhani, ngoja tusubiri tuone (Lema ni ni Chizi na a normal human being akianza kurushiana maneno na Chizi watu watashindwa kuwatofautisha yupi Chizi na yupi mzima)
 
Wataalam wa shria na katiba naomba msaada hapa:

Hivi rais (JK) akituhumiwa (na GL) kuingilia uhuru wa mamlaka nyingine ya dola (mahakama), tena tuhuma zikawekwa wazi kwa njia ya maandishi, Katiba na Sheria zinasemaje kuhusu uwezekano wa kufanyika uchunguzi wa wazi kuthibitisha kuwa tuhuma ni za kweli au za uongo?

Ni nani anapaswa kufanyia uchunguzi?

Ikionekana kuna kosa kisheria (mtuhumu au mtuhumiwa) ni adhabu gani inatolewa?
 
Mkuu wa mawasiliano na
habari ni mwandishi Salva Rweyemamu,wanaojua kazi ya RWEYEMAMU wakati
mtandao ukijiandaa kwenda Ikulu watakumbuka mchango wake mkubwa ulikuwa
kusifia kichwa cha nazi na kuchafua wagombea wazalendo kwa kadiri
ilivyowezekana.

Kwa ajili hiyo ukiangalia press release zote za Salva hutakosa maneno
aina ya majitaka au mipasho au dalili za ukosefu wa mamlaka ya
kimaadili.

Mliona utetezi dhidi ya suti tatu,au dhidi ya tuhuma za awali za Lema
dhidi ya Ikulu?
mkingoja jibu la msingi kwa Salva mtangoja sana....chambilecho
Mkapa!

zilikuwa suti tano sio tatu!
 
Back
Top Bottom