Ikulu kuingilia mgogoro wa Cuf

Ikulu kuingilia mgogoro wa Cuf

Na lipumba aombe sana huu mgogoro ndani ya CUF usiiishe kwa namna yoyote, aidha kwa kuwapatanisha au kwa kumfukuza Maalim Seif, maana ukiisha kazi yake na umuhim wake kwa wanaomtuma utakuwa umefikia ukomo na atakuwa sio agenda tena
 
Ahsante kwa taarifa mimi imenifanya nijaze mapengo yaliyokuwa yamebaki katika uchambuzi Wangu.
1. CCM hawafanyi siasa kwa sababu ni chama dola
2. Serikali hawafanyi tathmini ya athari ya mikakati yao.
3. Pamoja na gharama inayotumiwa, chama dola na dola yake wamejianika kuwa fedha na rasilimali zetu nchini zinatumika ndivyo sivyo.
4. Piga ua kupora haki hakumuwachi mtu salama.
5. Magu na wapuuzi wake wa CCM na vyombo vya usalama kwa sisi wengine mmethibitisha hofu yetu ya awali kuwa hamna uwezo wala dhamira ya uongozi wa taifa hata kwa katiba iliyopo.
6. Chama chenu kikiri tu mmefanya kosa kudhulumu haki za watanzania kuchagua viongozi wao kwa kuweka uongozi bandia.

Milijitahidi kupora madaraka, lakini kwa hii issue ya CUF kila siku mnajivua nguo. Na huo ndio udikteta wenyewe. Mbinu za kupambana na nyinyi zipo wazi ikiwa kwenye misingi ya HAKI SAWA na hususan haki ya Mungu.
 
Kwa ujumla watawala wanawajua vizuri Wazanzibar mwisho wake hautakuwa mzuri kwani walianza wao kuwabagua na kuwaona wenye Zanzibar yao hawana akili.
Sasa anavyozidi kuwabana ndo mwamko unazikuwa mkubwa kwa Wazanzibar halisi kwani wenyewe kwa wenyewe wanajuana hapo ndo install ulipo kwa wanaicheza hii Muvi.
Tahadhari ya mwalimu Nyerere Viongozi hawaifuati wameamua kuingia kibabe na majibu yake wanayo hao wanaotawaliwa sio hao wanaowapangia namna ya kuwatawala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sishangai kwani mwaka 2015 Mnyika wa CHADEMA alisema KIKWETE lazima aende' The Hague' na mapovu yakimtoka.
Mnaongea kilevi kilevi sana.Mutungi aende jela kwa lipi ?
Nakutakia maisha marefu sana mkuu , Francis mutungi atafungwa jela hata kama si kesho .
 
Kama kuna ambaye hajui, ukisikia kuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe inaandaliwa na dola yenyewe ndiyo hii sasa. Siku tu watu uvumilivu ukiwaishia, ndiyo itakuwa muda tayari. Hapo hakutakuwa na kamati ya ufundi, wala mikakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe pirika zote za lipumba ni kuona maalim hakabidhiwi haki yake zanzibar?
 
Kumbe pirika zote za lipumba ni kuona maalim hakabidhiwi haki yake zanzibar?
 
_Njama za kumvua uwanachama Maalim Seif zaiva_
_Ni baada ya kutishwa na ziara ya Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola_

Baada ya juma lililopita kupatikana habari za mkakati wa kambi ya Profesa Ibrahim Lipumba, anayetambuliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, kumfukuza katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa kuandaa mkutano mkuu ‘feki’ kwa kushirikiana na ofisi ya msajili huyo, taarifa za ndani zimezidi kuanika msingi wa mkakati huo na nani aliye nyuma ya jambo hilo.

Mzalendo.Net imebaini kuwa Maalim Seif anawindwa ‘kufukuzwa uanachama’ kinyume na sheria na taratibu ili kuinusuru Serikali ya Muungano wa Tanzania (SMT) na kibano cha kutengwa na jumuiya ya kimataifa kufuatia kutotekeleza sharti la kuirejesha Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) na makabidhiano ya ushindi kwa mshindi kufuatia uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015.

Awali, jumuiya ya kimataifa ilitegemea SMT ingeliingilia kati mgogoro wa uchaguzi uliotokana na hatua ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha, kufuta matokeo ya uchaguzi huo na kuitisha mwingine tarehe 20 Machi 2016, ambao ulisusiwa na CUF na kupingwa na jumuiya hizo ya kimataifa iliyotoa msimamo wake wazi wazi wa kutokubaliana na jambo hilo.

“Jambo hilo limeiweka Zanzibar katika hali mbaya kiuchumi, kidiplomasia na kisiasa. Matarajio kuwa Serikali ya Muungano ingeliingilia mgogoro huu, yalitokana na hotuba ya Rais John Pombe Magufuli katika uzinduzi wa Bunge (la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma) mwezi Novemba 2015,” kinasema chanzo chetu kilicho karibu na serikali zote mbili, ya Muungano na ya Zanzibar.

Itakumbukwa kuwa kwenye hotuba hiyo iliyoshuhudia Dk. Ali Mohamed Shein akizomewa na wabunge wa upinzani, Rais Magufuli aliahidi kufanya kila awezalo kulimaliza suala la Zanzibar kwa kushirikiana na pande zote husika.

Hata hivyo, mara baada ya kutulia Ikulu ya Magogoni, inaonekana Rais Magufuli alipata ushawishi wa kuachana kabisa na suluhu ya Zanzibar na badala yake akaelekeza nguvu zake kukinusuru chama chake cha Mapinduzi (CCM) na aibu hiyo na hali hiyo kwa serikali yake kuandaa mpango wa kukihujumu chama cha CUF kupitia msajili wa vyama vya siasa.

Kwa pamoja, Ikulu na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa walimshawishi na hatimaye kumrejesha Lipumba katika nafasi ya uongozi wa CUF aliyokuwa amejiuzulu tangu tarehe 5 Agosti 2015, miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015.

“Ilikuwa rahisi kumshawishi Lipumba kushiriki mpango huo, kwani alikuwa ameshakubali pale mara ya mwanzo kushawishiwa ajiuzulu pamoja na Dk. Wilbroad Slaa (aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA) ili kuwasambaratisha UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi unaoundwa na CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi na NLD),” kinasema chanzo chengine.

UKAWA itaingia kwenye vitabu vya historia ya chaguzi za vyama vingi nchini Tanzania kwa kufanikiwa kwa mara ya kwanza kuitikisa na kuipa CCM wakati mgumu katika uchaguzi mkuu kwa pande zote mbili za Muungano (Bara na Zanzibar).

Chanzo hicho kinasema kuwa baada ya CUF “kuchukua hatua kadhaa za kujihami na hususani uamuzi wa kukimbilia mahakamani na kufungua kesi zenye mashiko”, sasa Serikali ya Muungano chini ya uongozi wa Rais Magufuli imeamua kutumia gharama na kila aina na nguvu kumsaidia Lipumba kufanikisha jambo hilo.

Katika siku za hivi karibuni, nguvu ya dola imejidhihirisha waziwazi kwenye mgogoro wa CUF baada ya taasisi nne za dola kuonekana kwa wakati mmoja zikijiingiza kichwa kichwa – Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA), Bunge la Jamuhuri ya Muungano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) – katika mpago wa waziwazi kusajili wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini ya CUF kinyume cha sheria, kufukuza wabunge wanane wa viti maalum na kuteua wengine wapya katika utaratibu wa kasi kubwa mno.

“Tatizo kwao ni kuwa CUF inafunguwa dhidi ya kila hatua wanayoona inawaelemea, ikiwemo moja ya jinai inayohusu contempt of court proceedings (kwa kughushi nyaraka ili kuishawishi mahakama isitende haki) dhidi ya Jaji Mutungi kama msajili wa vyama vya siasa, Emmy Hudson kama kaimu kabidhi na wasii mkuu wa RITA na Thomas Malima, ambaye ni mkurugenzi wa fedha wa Lipumba,” anasema mwanasheria mmoja wa ngazi za juu katika Chama cha Mawakili cha Tanganyika (TLS).

Mtandao huu wa Mzalendo.Net umefahamishwa kuwa mara tu baada ya CUF kuamua rasmi kuwekeza nguvu zake mahakamani kinyume na ilivyotazamiwa na ilivyozoeleka huko nyuma, ambapo chama hicho hakikuwa kikiamini uwezo na uadilifu wa mahakama, Ikulu iliamuru kufanyika kwa utafiti na timu ya wanasheria kutoka Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msajili wa Vyama vya Siasa kujuwa nafasi ya ushindi kwa serikali kwenye kesi hizo.

“Ukweli ni kuwa wanasheria waliwaeleza wazi wakubwa wao kuwa katika mashauri yote yaliyofunguliwa mahakamani, basi msajili hawezi kunusurika kama kesi zitaendeshwa kiadilifu. Ndipo ikaamuliwa kuwaomba majaji wanaoendesha mashauri ya CUF kusaidia kumnusuru Jaji Mutungi na kuiokoa serikali kutokana na aibu hii kubwa,” anasema mwanasheria mwengine ambaye yupo kwenye idara moja muhimu serikalini.

Chanzo chetu chengine kinasema kuwa kazi hiyo alipewa Jaji Mfawidhi Mama Mutungi (mkewe Jaji Francis Mutungi), lakini majaji wanaonekana kusutwa na nafsi zao kutenda dhambi hiyo kwa jambo lililo wazi na lenye maslahi na watu wengi.

Matokeo yake, chanzo chetu kinasema, majaji waliishauri Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itafute mawakili wazuri wanaoweza kuweka mapingamizi kupitia hoja za awali ili mashauri yaondolewe katika hatua za awali, kwani yakisikilizwa kama yalivyo, hakuna uwezekano wowote wa kutokipa chama cha CUF ushindi katika takribani mashauri yote kilichofunguwa.

Mzalendo.Net ina taarifa kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliwasiliana na Ikulu juu ya jambo hilo na ndipo ikulu ikatoa maelekezo kwa Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma kuhakikisha kuwa kesi zote zinatengenezewa mazingira ya kufutwa kupitia mapingamizi katika hoja za awali.

Naye, Kaimu Jaji Mkuu Juma kwa kutambuua kuwa hajathibitishwa na hivyo anaweza ‘kutumbuliwa’ wakati wowote, amelichukulia jambo hilo kuwa ni fursa na analifanya kwa kasi na usimamizi wa karibu sana.

Chanzo chetu kinatueleza kuwa Ijumaa ya tarehe 18 Agoti 2017, Kaimu Jaji Mkuu Juma alifika katika ofisi ya Jaji Kiongozi na kisha akakutana na Jaji Wilfred Dyansobera katika kile kilichosemekana ni kumkabidhi hukumu aliyoiandaa ya amri ya kuondoa zuio la ruzuku ya CUF kwa Lipumba siku ya Jumanne tarehe 22 Agosti 2017.

Aidha kila shauri limeundiwa kamati maalum inayofuatilia, ambazo hukutana kila siku na kufanya tathmini kisha kutoa mrejesho moja kwa moja Ikulu ili kuiwezesha Ikulu kuelekeza ifaavyo.

Kasi ya maelekezo ya Ikulu imeongezeka kufuatia ziara ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland, kufuatilia mchakato wa utekelezaji wa utatuzi wa mgogoro wa uchaguzi Zanzibar. Serikali zote mbili – ya SMT na ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) – zinaamini kuwa endapo Maalim Seif akifukuzwa chama, watapata utetezi kuwa hawawezi kumkabidhi serikali kwa kuwa hatokani na chama cha siasa.

“Aidha mahakama imeelekezwa kutopokea mashauri mengine mapya kutoka CUF kwa hoja kwamba kwanza inayashughulikia na kumaliza haya yaliyopo,” kinasema chanzo hicho.

Maelekezo hayo yalijaribiwa kutekelezwa na Msajili wa Mahakama pale CUF ilipotaka kufungua shauri jipya kuhusiana na wizi wa ruzuku baada ya lile la awali (Na.21/2017) kuondolewa kwa pingamizi la Jaji Wilfred Dyansibera.

“Awali Jaji Dyansobera alipangua hoja za pingamizi zote zilizowasilishwa, lakini katika hali yenye utata aliibuka na kile alichosema ni kwa maoni yake shauri lilipaswa kuletwa kwa kifungu cha 2(3) cha Judicature and Application of Laws Act, ambacho kwa wanaofahamu sheria wanafahamu kuwa hakisemi chochote kuhusu judicial review, mandamus and prohibition or prerogative orders (mapitio ya kimahakama),” kinafafanuwa chanzo chetu.

Uamuzi huo ambao taarifa za uhakika zinasema alipewa ausome na kuliondoa shauri ulikuwa katika karatasi iliyoandikwa kwa mkono tofauti na ile ya uchambuzi iliyokuwa imechapwa kwa kompyuta ambayo ndiyo alikusudia kutolea maamuzi. Jambo hilo liliwashangaza wengi kwa sababu miongoni mwa majaji wanaoaminika katika kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusu haki za binadamu, utawala bora, utawala wa sheria na demokrasia ni Jaji Salvatory Bongole, Jaji Fauz Abdallah Twaibu na yeye Jaji Dyansobera. Uamuzi wake ulionyesha wazi kuwa kuna mazingira yanayoshinikiza na kuondoa uhuru wa utendaji kazi wa Jaji Dyansobera.

Hata hivyo, baadaye Msajili wa Mahakama Kuu alilipokea shauri hilo pamoja na lile lililofunguliwa na wabunge wa CUF, ila taarifa za uhakika zinasema ameelekezwa asiyapangie jaji miongoni mwa waliopo sasa mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, na badala yake panaangaliwa uwezekano wa kumleta jaji kutoka mikoani mahsusi kwa ajili hiyo.

Hatua hiyo inatokana na Ikulu kuona kuwa huenda majaji waliopo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wameshikwa kigugumizi na kuchoshwa na udhalimu unaoendelea dhidi ya CUF na uvunjwaji wa sheria na haki.

Taarifa zaidi zinasema baadhi ya mawakili wanaosimamia mashauri ya CUF wametishwa kuwa watavuliwa uwakili iwapo wataendelea kusimamia mashauri hayo. Chanzo cha habari hizo kinasema baadhi ya mawakili hao wameanza kuchukua hatua za kujihami kwa kujiondoa katika mashauri mapya yanayowasilishwa mahakamani hapo.

Mtoa taarifa wetu aliye mahakama kuu anasema jambo hilo ni rahisi kufanyika kwa sababu utaratibu ni kutengeneza malalamiko tu na kuyawasilisha kwa Jaji Kiongozi ambaye anawezesha mchakato huo katika muda mfupi sana.
 
The good thing ni kuwa muda wa kutumika wa Lipumba utaisha na maccm yalivyo yakishakutumia yanakutupa na kukupotezea kama condom iliyotumika awaulize watangulizi wake watamwambia
 
Back
Top Bottom