Ikoje hii

GY

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,279
126
serikali ya libya yajitokeza kusaidia athari za mafuriko kilosa


Kuwajengea Nyumba 200 Nyumba Waathirika
Na Jovina Bujulu, Maelezo.
Jamhuri ya watu wa Libya imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko ya Kilosa mkoani Morogoro. ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba 200 zenye thamani ya shilingi bilioni 1.5.

Akiongea na wanahabari katika uwanja wa ndege Dar es Salaam Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) Mheshimiwa Philip Marmo alisema msaada huo umekuja wakati muafaka kwani hali ya wahanga hao si ya kuridhisha

Aidha Waziri Marmo alizitaka nchi rafiki,Jumuiya za Kimataifa pamoja na Watanzania kwa ujumla kutoa misaada kwa hiari yao kwa kadri wanavyoguswa kwa wahanga wa mafuriko ya Kilosa.

“Uwezo wa Serikali ni mdogo na hauwezi kutosheleza kila kitu hivyo tunaomba Jumuiya mabalimbali za Kimataifa na Watanzania Kushirikiana katika kutoa misaada”.Alisema.

Pia alizitaka Kamati za maafa husika kutekeleza wajibu wao kwa kufikisha misaada hiyo kwa wahusika na alimhakikishia balozi wa Libya nchini Ahmed Abdusalaam Al Ashaab ambaye alikabidhi msaada huo kwa niaba ya nchi yake kuwa itawafikia walengwa na magari yataanza kupeleka misaada hiyo kesho.

Akikabidhi msaada huo balozi wa Libya nchini bwana Ahmed Abdulsalaam Al Ashaab alisema msaada huo umetolewa na jumuiya mbalimbali nchini humo kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Libya.

Vifaa vilivyotolewa ni magaro 1100, Blanketi 400, Mahema 1300, Mito 1200, Maboksi 500 ya madawa ikiwa ni pamoja na vifaa vya huduma ya kwanza.


source: Michuzi blogspot

© Michuzi | Saturday, January 16, 2010 | Permalink | Mtumie Rafik




Maoni Binafsi:

Kwa Tshs ambazo gadafi ametoa kujenga nyumba 200 za wahanga wa mafuriko, benki kuu ya tanzania imejenga nyumba moja tu ya gavana

ikoje hii wakulu!
 
Familia 200 hazijafikia hadhi ya mwandamizi(mheshimiwa) katika nchi za Africa. Labda ziongezeke kidogo zifikie kama 500 hivi.
 
Back
Top Bottom