Iko wapi historia ya bendi zetu?

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Posts
244
Reaction score
166
Wana JF,

Nataka kuandika kitabu kuhusiana na Bendi za muziki za zamani kidogo. Kitabu chenyewe kitakuwa na mkusanyiko wa historia fupi ya Bendi hizo, wanamuziki wake, Makao makuu yao, Nyimbo zao zilizotamba wakati huo, tunzo mbalimbali walizowahi kushinda, na pendine kujua wanamuziki hao wako wapi na wanafanya nini.

Pengine pia ningependa kujumuisha na mafanikio waliyo nayo au wanayoyapata kutokana na kazi zao.

Ninataka kuandika kuhusiana na Bendi hizi zifuatazo:

Matimila Band
OSS Safari Sound
Juwata Jazz ya wakati ule
Tancut Almasi
Uda Jazz- wana Bayankata
DDC Mlimani Park ya wakati ule wa DDC Kariakoo au CCM kata ya 14
Sambulumaa
Maquis
Washirika Watunjatanjata
Bantu Group
M K Group

Na nyinginezo…..

Je, ni wapi ninapoweza kupata kumbukumbu za bendi hizi, na labda uwezekano wa kupata namba za simu za kila mwanamuziki mmoja mmoja ili niweze kufanya miadi ya kukutana nao na kufanya mazungumzo nao.

Nimegundua kwamba historia ya Bendi hizi za muziki inaweza kutoweka na hivyo vizazi vijavyo vikakosa kufahamu historia ya muziki wetu na Bendi zetu za Muziki.

Naomba ushirikiano wenu.

Angalizo: Hili ni wazo langu binafsi na sijafadhiliwa na mradi wowote.
 
Nenda Redio Tanzania, wana kila kitu juu ya hizo Bendi.
 
yeah RTD kwa sasa TBC1 wana archive kubwa sana ya hizi nyimbo!! hapo utapata kila kitu!

Niliwahi kwenda pale TBC 1 lakini walinzi hawakunipa ushirikiano, nashukuru kwa blog ya Kitime nadhani huyu atakuwa na mchango mkubwa wa huu mradi wangu.

kama kuna mwenye mchango zaidi naomba asisiste kunipa kwani lengo langu ni kutaka kuweka kumbukizi za hawa jamaa.......

Pamoja tuijenge nchi yetu......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…