Iko wapi CHADEMA jeuri ya Dr.Slaa iko wapi BAVICHA tukutu ya John Heche

DAH KWELI MASHINJI ANAKAZI

Mashinji hana kazi yeyote,tatizo mnapigana na nguvu msiyoiona.Haya hebu jiulizeni familia moja wanasheria 13,na mnategemea familia itawasupport,wamekwambia wala msihangaike nao mkutane Mahakamani.

Chama Cha Mauaji aka CCM miaka 55 ya uwepo wake duniani,miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika kila siku ni bora ya jana!Mlichoweza kufanikiwa ni Utekaji,Utesaji na Uuaji waraia wasio na hatia.
 
Dr Slaa atakumbukwa kama katibu mkuu aliyewahi kuongoza CHJADEMA kwa mafanikio mbali mbali chini ya katibu mkuu Dr Slaa tuliona CHADEMA ikipata mafanikio makubwa kwa kuongeza wabunge wengii na madiwani wengi na yote haya yalifanikiwa sababu katribu mkuu ndio mtendaji mkuu wa chama na injinii ya chama.

MAANDAMANO

Chini ya Dr Slaa tuliona tuliona akiongoza maandamano tofautii katika mikoa mbalimbali ya nchi sababu ya ujasil wake na kupigania anachokiiamini mfano tunaweza kuona maandamano yaliyofanyika jijini Mwanza 26 September 2014 Dr Slaa alikuwepo pale kuwapa nguvu vijana wake na kuhakikisha wanatiimiza lengo lao kwa mujibu wa sheria hakua muoga hata kidogo

Chini ya Dr Slaa tumeona maandamano yaliyofanyika Arusha 4 January 2011 kupinga uchaguzii wa Meya maandamano kama haya tunaona Dr Slaa alikua mstar wa mbele kama mtendaji mkuu kuhamasisha makamanda wake yeye kama kiongozi hakurudi nyuma na ujumbe uliwafikia watanzania wengi na katika yote haya hakuogopa mabomu wala vitisho vya polisi.

OPERATION
Chini ya uongozi wa Dr slaa tuliona CHADEMA ikija na operation mbalimbali ndani ya chama ambazo ziiliweza kuvutia wanachama wengi kujiunga na chama na pia kuelewa malengo na dhamira ya dhati ya chama opoeration kama Sangara,Chadema ni Msingi,m4C nk operation kama hizi zote zilianzishwa chini ya Dr slaa zlisaidia sana kusambaza chama mpaka vijijin hivyo chama kikawa na wafuasi wengi na kukubalika kwa wanachama hapa tunaona Dr Slaa alikua mbunifu na kiongozi anayebadilika kutokana na wakati.

NINI KIMETOKEA?
B
aada ya Dr Slaa kubwaga manyanga alipewa jukumu hiko zito Dr Mashinji ili kuongoza chama hapa alikuja na operation UKUTA operation hii hakufanikiwa maana ilikua na lengo la kupambana na u dikteta uchwara hapa mashinji alishindwa kuongfoza majemedali wake kupigania kile anachokiamin na hivyo operation hii ikafa kibudu na kifo cha mende na baada ya hilop hakuja na njia mbadalka wa kufikisha ujumbe kwa watanzania na watawala badala yake alisalim amri na kurudi ofisin kufanya paper work hata majemedari kama kina John John Mnyika wameamua kuwa kimya,kina kamanda Lema baada ya Kisongo wameamua kufanya siasa pozo sababu hawana back up ya kiongozi wao mkuu.
Hapa tunaona ile spirit ya maandamano hakuna tena wala operation hakuna tena tofauti na CHADEMA chini ya Dr Slaa na mfano mzuri ni pale Wafuasi wa CHADEMA waliopozuiwa kufanya maombi kwa ajiri Lissu uwanjani hakukuwa na vijana au wanachama wanaofikia hata 20 hii ni mbaya kwa mstakabali wa chama

BAVICHA YA HECHE VS BAVICHA YA PATROBAS
Bavicha chini ya Heche tunaona ilivyokua moto moto na vijana waliokuwa machachali katika ujenzi wa hoja na kupigania chama kipindi cha era za bavicha ya Heche ndio walikuwepo vijana machachali akina David Kafulila,Juliana Shonza,Kashinje Masanja,Chagulani,Nyakarungu,Habib Mchange akina Manawa Bukwimba,Mtela mwampamba aina hii ya vijana ndani ya BAVICHA ya Heche ilikua tishio mpaka serkali ya CCM kuamua kununua baadhi ya vijana kwa ahadi ya pesa na uongozi sababu tu ya uwezo wao wa kujenga hoja na ushawishii katka jamii vijana kama kiina Shonza na Mtela walinunuliwa na CCM sababu ya utukutu wao wa kujenga hoja,kuhoji na kutikisa serikali Shonza sasa hv ni mbunge viti maalum na Mtela ni DAS
Ukitizama hapo juu aina ya BAVICHA ya Heche ukaja kuona BAVICHA ya Patrobas imeshindwa kabisa kutoa vijana ambao ni jeur na tukutu wanaoweza kujenga hoja na kuyumbisha serikali BAVICHA inafanya siasa pozo na zisizo na malengo mfano waliposema wanaenda kuzuia mkutano mkuu wa CCM Dodoma ambao Magufur alipewa uenyekiti hakuna impact yeyote iliyooneka kwa harakati zao hizo.

Tunamuombea AFYA NJEAMA mpiganaji Tundu Mungwai Antipasi Lissu huyu ni mpiganaji wa kweli na vijana wengi wanatamani kuwa kama yeyey lakini hawataweza sababu wamejawa na uoga,unafiki wanajazana kwenye comment JF lkn wakihitajika kusonga front kama alivyo Lissu hauta ona hata mmoja hapa ndio unapata taswira ya vijana halisi tulio nao katika chama

Pia hapo jana walitangaza maombi kwa ajiri ya Lissu na polisi wakazuia hatukuona kiongozi yeyote wa BAVICHA akiiwa uwanjani na hata vijana wakiwa uwanjani kuonyesha wana nia ya dhati katika lengo lao hilo la kufanya maombi hapa tunaona BAVICHA imekwama ki mkakati na hata vijana wengi wa BAVICHA wanapambana kwenye social media kama Jamii Forum kwa ID fake lakini kwenye ujenzi wa Chama na wanapohitajika kwa chama kujitokeza kama hapo jana hawaonekani wako busy kwenye mitandano ya kijamii wakificha sura zao nyuma ya vioo vya simu zao. Ujenzi na ukombozi wa NCHI hii unahitajika kujitokeza na kuonekana ukifanya vitu kwa vitendo na sio kwa ku comments na ku like vijana na wana CHADEMA badiliken

Tunahitaji CHADEMA jeuri kama ya Dr.Slaa na BAVICHA tukutu kama ya John Heche
Is he an asset or a liability yule jamaa??
 
Mashinji hana kazi yeyote,tatizo mnapigana na nguvu msiyoiona.Haya hebu jiulizeni familia moja wanasheria 13,na mnategemea familia itawasupport,wamekwambia wala msihangaike nao mkutane Mahakamani.

Chama Cha Mauaji aka CCM miaka 55 ya uwepo wake duniani,miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika kila siku ni bora ya jana!Mlichoweza kufanikiwa ni Utekaji,Utesaji na Uuaji waraia wasio na hatia.
haya uliyoongea yapo kwenye bandko langu mkuu?
 
Unalinganisha zama mbili tofauti, kati ya uongozi wa kidemokrasia na uongozi wa kifashisti.
 
haya uliyoongea yapo kwenye bandko langu mkuu?

Utajaza,ninachojua ni kwamba Chama Cha Mauaji miaka 55 ya Uhuru mlichoweza kufanikiwa ni Mauaji ya RAIA,Utekaji na Utesaji wa raia wasio na hati.Sasa kama pilipili imekuwasha kanywe maji
 
Utajaza,ninachojua ni kwamba Chama Cha Mauaji miaka 55 ya Uhuru mlichoweza kufanikiwa ni Mauaji ya RAIA,Utekaji na Utesaji wa raia wasio na hati.Sasa kama pilipili imekuwasha kanywe maji
sasa yana fall katika mada ipi ya bavicha au chadema ya mashinji na slaa?
 
sasa yana fall katika mada ipi ya bavicha au chadema ya mashinji na slaa?

Ndiyo mjue hata Dr.Slaa hakuwa na lolote la maana zaidi ya kusbiria kufika bei.Pole sana sana.

Kamwambie Mwenyekiti wako wa Chama Cha Mauaji,wengi wetu tunasema hivi Chama Cha Mauaji miaka 55 mlichoweza kufanikiwa ni:
1.Mauaji ya RAIA wasio na hati
2.Utekaji wa RAIA wasio na hatia.
3.Utesaji & UKATILI kwa RAIA wasio na hati.
4.Upigaji wa Mabomu kwa RAIA wasio na hatia.
5.UFISADI
6.RUSHWA
7.UJANGILI

Njoo tena ndugu.

SMG
yanini njoo tubishane kwa HOJA
 
Tangu bundi lowasa atue chadema basi chadema imegeuka imekuwa haitetei tena maslahi ya wengi
 
Ndiyo mjue hata Dr.Slaa hakuwa na lolote la maana zaidi ya kusbiria kufika bei.Pole sana sana.

Kamwambie Mwenyekiti wako wa Chama Cha Mauaji,wengi wetu tunasema hivi Chama Cha Mauaji miaka 55 mlichoweza kufanikiwa ni:
1.Mauaji ya RAIA wasio na hati
2.Utekaji wa RAIA wasio na hatia.
3.Utesaji & UKATILI kwa RAIA wasio na hati.
4.Upigaji wa Mabomu kwa RAIA wasio na hatia.
5.UFISADI
6.RUSHWA
7.UJANGILI

Njoo tena ndugu.

SMG
yanini njoo tubishane kwa HOJA
angekua hajafanya lolote leo kusingekua na wabunge 116 wa ukawa bungeni
 
angekua hajafanya lolote leo kusingekua na wabunge 116 wa ukawa bungeni

Amefanya nini alichofanya kupokea pesa za CCM??Hivi huyo Dr.Slaa amekuwa mzuri baada ya kufanikiwa kulaghaiwa na Chama Cha Mauaji??

Mnatia hata huruma,dhambi ya kutoa UHAI wa mtu haitawaacha salama hata kidogo,mpaka vizazi 25 vya koo zenu zitaikumba adhabu hiyo
 
Kapokea pesa ya CCM shilingi ngapi?
 
Amefanya nini alichofanya kupokea pesa za CCM??Hivi huyo Dr.Slaa amekuwa mzuri baada ya kufanikiwa kulaghaiwa na Chama Cha Mauaji??

Mnatia hata huruma,dhambi ya kutoa UHAI wa mtu haitawaacha salama hata kidogo,mpaka vizazi 25 vya koo zenu zitaikumba adhabu hiyo
Hata ikiwa hivyo, bado hujajibu hoja. Chadema ya Dr. Slaa Na chadema ya Dr. Mashinji ziko sawa? Bavicha ya Heche Na bavicha ya Patrobas ziko sawa?
 
Hata ikiwa hivyo, bado hujajibu hoja. Chadema ya Dr. Slaa Na chadema ya Dr. Mashinji ziko sawa? Bavicha ya Heche Na bavicha ya Patrobas ziko sawa?
Mkuu hawawez kujibu wataleta mambo ya viwanda sjui bombadier utafikili ndo hoja iliyopo mezan
 
angekua hajafanya lolote leo kusingekua na wabunge 116 wa ukawa bungeni

Jibu hayo juu.Alimfanyia kampeni Mubunge yupi??Katika watu wanaodharauliwa na dunia leo ni huyo jamaa yenu Dr.Slaa naye akafie mbali hana tofauti na washika SMG
 
Jibu hayo juu.Alimfanyia kampeni Mubunge yupi??Katika watu wanaodharauliwa na dunia leo ni huyo jamaa yenu Dr.Slaa naye akafie mbali hana tofauti na washika SMG
hajasoma hapo juu kaz alizofanya katika ujenzi wa chama?
 
Back
Top Bottom