Ikiwa CUF hawata chukua hatua yoyote baada ya kususia uchaguzi, mambo yafuatayo yataenda kutokea

vevenononombo

JF-Expert Member
Jun 19, 2015
1,289
420
WanaCUF Zanzibar walifanya sehemu yao kwa uadilifu mkubwa hasa kwa kutii viongozi wao na kutoshiriki uchaguzi, lakini kama chama kikishindwa kwenda mbele zaidi ya hapo na kuamua kukaa kimya, yafuatayo yanaweza kutokea ktk siasa za Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla;

1. Wananchi watakata tamaa na vyama vya upinzani hasa Cuf hivyo kupoteza nafas adimu iliyokuwa imepewa na wananchi kwakuaminiwa kias kile

2. Wananchi wanaweza kuamua kuja na wazo la kuwa na mfumo wa chama kimoja kwakua vyama vingi vimeshindwa kuwasaidia matakwa yao.

3. WanaCUF hasa waliokuwa wameshinda uchaguzi na walikuwa wakikubalika lkn wakasusa kwa amri ya chama wanaweza kuwa chanzo cha migogoro ktk chama na kupelekea chama kugawanyika vipande vipande.

4. Kuna uwezekana wakuibuka mpinzani mwenye nguvu ndani ya cuf visiwani ambaye atakuja na ajenda ya mabadiliko ya kiuongozi kwakudai waliopo sasa wameshindwa kukivusha chama kwa namna yoyote iwe kwa Sera za ngangar au vyovyote vile.

5. Kuna kila dalili ya maalim Seif kuitwa msaliti muda sio mrefu na kuonekana ni pandikizi la chama tawala kupunguza nguvu za upinzani.

6. Umri wa Sharrif umeenda hivyo kutakuwa na vuguvugu kubwa la kutaka kumuondosha kwa kisingizio cha umri na ni wazi kabisa kwa haraka haraka haionyeshi kama kuna MTU anamuandaa kurithi mikoba yake.

7. Mwisho wa CUF unaweza kuwa 2020

Wasalam vevenononombo @ 2016..
 
Mim nauliza tu makubaliano ya Cdm na cuf kuhusu swala la ruzuku uko je maana mim najua labada kuna kamemorandam of understanding hasa kuhusu mgombea wa urais maana ndie mwenye kufanya mgawanyi wa ruzuku uweje ,saasa sijui CUF itajiendesha kivip maana bara amna ruzuk,visiwan nako hamna ruzuku
 
Watakuja kukujibu
 
Sioni kama hoja yako Inamashiko, Inaonekana bado zanzibar na watu wake pamoja na tabia zao hujazielewa,kwa kifup wazanbar wana uchungu wa kweli na nchi ya ndo mana wana misimamo thabit, unazikumbuka kura za Maruhani? Alafu ccm Imechokwa bara na znbr
 
Binadamu pia anatabia ya kubadilika usilisahau hilo
 
hata ww kwenye bandiko lako umesahau au aujafkir kwamba Maalim seif alishinda na wazanzibr wanajua Ivyo na haitafutika mkuu, Pili- kauli za ovyo kabsa za ccm juu ya ushnd wa cuf znbr kwamba mpaka wafanye mapinduz ndo wapewe nchi, ila kwa makaratas hawatoi nchi,. Naweza nikaunga mkono hoja yako kwenye namba6 napo c kwa asilimia 100%
 
WanaCUF Zanzibar walifanya sehemu yao kwa uadilifu mkubwa hasa kwa kutii viongozi wao na kutoshiriki uchaguzi, lakini kama chama kikishindwa kwenda mbele zaidi ya hapo na kuamua kukaa kimya, yafuatayo yanaweza kutokea ktk siasa za Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla;

1. Wananchi watakata tamaa na vyama vya upinzani hasa Cuf hivyo kupoteza nafas adimu iliyokuwa imepewa na wananchi kwakuaminiwa kias kile

2. Wananchi wanaweza kuamua kuja na wazo la kuwa na mfumo wa chama kimoja kwakua vyama vingi vimeshindwa kuwasaidia matakwa yao.

3. WanaCUF hasa waliokuwa wameshinda uchaguzi na walikuwa wakikubalika lkn wakasusa kwa amri ya chama wanaweza kuwa chanzo cha migogoro ktk chama na kupelekea chama kugawanyika vipande vipande.

4. Kuna uwezekana wakuibuka mpinzani mwenye nguvu ndani ya cuf visiwani ambaye atakuja na ajenda ya mabadiliko ya kiuongozi kwakudai waliopo sasa wameshindwa kukivusha chama kwa namna yoyote iwe kwa Sera za ngangar au vyovyote vile.

5. Kuna kila dalili ya maalim Seif kuitwa msaliti muda sio mrefu na kuonekana ni pandikizi la chama tawala kupunguza nguvu za upinzani.

6. Umri wa Sharrif umeenda hivyo kutakuwa na vuguvugu kubwa la kutaka kumuondosha kwa kisingizio cha umri na ni wazi kabisa kwa haraka haraka haionyeshi kama kuna MTU anamuandaa kurithi mikoba yake.

7. Mwisho wa CUF unaweza kuwa 2020

Wasalam vevenononombo @ 2016..
Kwa hiyo unataka CUF wafanyeje?
 
baada ya ccm kuona upinzani ulikua mkali tofauti na walivyodhani kitachofanyika kwa sasa in kwamba itatumika nguvu kubwa kupandikiza mamluki kwenye vyama pinzani, na kusababisha baadhi ya vyama Kupoteza mwelekeo au kufa kabisa
 
Maalim SEIF naye asuse malupulupu yote anayopewa kama WAZIRI kiongozi mstaafu! Vinginevyo nawashangaa wenzake kukubali kususa wakati yeye anakula Kuku kwa mrija!
 
Malupulupu= Marupurupu ni kodi za wananchi na analipwa kwa mujibu wa katiba. Sio fadhila ya serikali ya CCM!
 
Nadhani CUF walisusia kwa maana ya kuuliza nguvu ya umma ila kwakuwa lilitumika jeshi sasa tusubiri mungu maana,anapoishia kuwajibika mtu ndo mungu anapoanzia
Dua la Kuku! Watabaki wakinung'unikia kwenye shuka! Vinginevyo watakuwa wanampima amiri jeshi MKUU kama kiberiti kimejaa njiti au vinginevyo!
 
Malupulupu= Marupurupu ni kodi za wananchi na analipwa kwa mujibu wa katiba. Sio fadhila ya serikali ya CCM!
Kwani hao wenzake kama wasingesusa wangelipwa na pesa za nani? Wote wanalipwa kwa kodi ya wananchi!
Itakuwaje ushawishi wenzako wasuse wakati wewe unaendelea kufaidi? Poleni maana hamjielewi!
 
Back
Top Bottom