Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Siku zote tunakuwa na vitu kwa sababu tunavihitaji. Tutakuwa watu wa ajabu sana ikiwa tunarundika vitu kwenye nyumba zetu mwisho wa siku tunaishia kuviteketeza. Israf.
Kwa zaidi ya miaka 34 tangu Tanzania ipate uhuru, nchi yetu iliendeshwa kwa mfumo wa chama kimoja na mambo yalienda. Nakumbuka mwaka 1992 tulipo move kutoka single party system kwenda multparty, Watanzania wengi hawakuafiki mabadiliko hayo. Kwa hakika wakati ule tulishikwa na butwaa pale asilimia 80 walipokataa mfumo wa vyama vingi na asilimia 20 tu ndio waliafiki. Tuliwaona watu wa ajabu sana. Hata hivyo, kwa kuwa wakubwa waliamua, tukaamua kupingana na principle ya democracy inayosema wengi hutawala, wachache husikilizwa. Tukaenda kinyume ambapo wachache wakatawala na wengi hawakusikilizwa. Sasa tunajuta.
Nadiriki kusema kuwa sijaona umuhimu wa wabunge wa vyama vya upinzani nchini. Hawa wabunge wamegeuka kuwa kero hasa kutokana na kushindwa kabisa kutimiza wajibu wao bungeni. Hata hivyo, nina mashaka na jinsi wanavyopatikana. Wabunge wengi wa upinzani wanapatikana kwa kujuana, unasaba na hata mahusiano na wenye vyama. Ndio maana wanakosa kabisa misimamo na wengi wao wamekuwa wakifuata mkumbo bila ya kutumia akili. Yaani wakiambiwa leo wekeni pamba masikioni, wanaweka bila kujiuliza kwa nini wanafanya hivyo. Akiambiwa leo zungusheni mikono wanazungusha na hawahoji kwa nini wanafanya hivyo. Wakiambiwa leo zibeni midomo wanaziba na hawajui kwa nini wanafanya hivyo. Na anayewaendesha wala hafanyi hivyo na hayupo Dodoma jwa wakati huo. Remote control.
Wabunge wa upinzani wamekuwa wakitoka bungeni kwa lengo la kushinikiza jambo fulani hata hivyo kutokana na idadi yao kuwa ndogo, ni dhahiri kuwa wanatwanga maji kwenye kinu. Na haya ni matokeo ya kutofanya vizuri kwenye uchaguzi. Yaani ukipigwa kwenye uchaguzi basi ukubali kuvumilia maumivu kwa miaka mitano. Whether you like or not. CCM itaendelea kutawala na kila mtakachofanya ni kupoteza muda na kujiburudisha. Ukishakuwa mnyonge ni mnyonge tu. namna nzuri ya kupambana na aliyekuzidi ni kujipanga. Hii style ya kujitutumua ilhali mpo wachache hakika ni kupoteza muda.
Walitoka kwenye Bunge la Katiba, mijadala ikaendelea na Katiba Pendekezwa imepatikana. Wamesusia Bunge la Bajeti, hakika kususa kwao hakujawasaidia na Bajeti imepita. Ndipo ninapojiuliza, uwepo wao Bungeni una faida gani? Na hapa ndipo ninapoona tofauti ya wapinzani wa Tanzania na wa nchi nyingine. Sidhani kama Malema wa South Africa angekuwa na tabia za kususa angefanikisha Rais Jacob Zuma kutingishwa kutokana na ufisadi aliofanya. Malema alipigana Bungeni kuhakikisha kuwa sauti yake inasikika na si kujiziba midomo ili usiongee. Utoto
Mwisho, niwatakie maisha mema wapinzani ya kususa Bungeni. CCM tunao wapinzani wa kweli ambao wanatimiza vema wajibu wao. Hussein Bashe, Kangi Lugola, Ayesh nk. Hawa ndio wanafanya kazi zenu na hakika wanatimiza vema wajibu wenu. Muwepo msiwepo hamna faida yoyote. Full Stop