Naandika haya kama mwananchi wa kawaida (common citizen) wala si kama mwanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa kuzingatia kwamba CCM ni chama tawala.
Ukweli usio na ubishi wana CCM wamegawanyika hawajui wasimame upande upi wa Musiba au wa Makatibu wao wastaafu.
Kuna baadhi wanasema Makamba na Kinana wametenda kosa kubwa, la kumuhujumu Mkiti wao ambaye pia ni rais wa nchi, wanasema kumuhujumu Mkiti ni usaliti na kumuhujumu rais ni uhaini, wengi wa hawa wako upande wa Musiba.
Kundi lingine linasema Makatibu wao wastaafu wako sahihi, wao ndio wanaokijua chama zaidi ya Mkiti wao, kwa hiyo wanataka kukirudisha chama mikononi mwa wanachama hasa waliokipigania usiku na mchana. Wanaona kama Mkiti wao anakimilikisha chama kwa wageni na kuwasahau wenyeji.
lnawezekana kila upande una hoja lkn watu wanahoji taratibu walizotumia kuyaweka madai yao hadharani ni kama kukidhalilisha na kukigawa chama. Damage imeshatokea nini kifanyike ili kukinusuru chama na nchi, kiujumla lazima chama kikubali ku take risk.
Ikithibitika Musiba anasema uongo kwa lengo la kukigawa chama aadhibiwe kulingana na sheria za nchi za uchochezi na madai, na ikithibitika Makamba na Kinana kweli wana mpango wa kumhujumu Mkiti ambaye ni Rais wa nchi, wavuliwe uanachama au kufunguliwa mashitaka ya uhainI au uhujumu uchumi.
CCM ni chama kikongwe kimepitia misukosuko mingi, haitakuwa mara ya kwanza kwa chama na serikali kuchukua hatua kama hizo, kina Kasanga Tumbo, Kambona, Abdul Jumbe, Maalimu Self, Kolimba, na wengine wengi waliwahi kuchukuliwa hatua hizo.
Enzi za Mwenyekiti Nyerere lilipokuja suala la kuilinda nchi na chama hakukuwa na cha msalie mtume, sote tunakumbuka aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba alipotofautiana na msimamo wa chama.
Suluhu yeyote zaidi ya hayo ni kuacha mbegu izae matunda ya usaliti si tu ndani ya chama bali hata ndani ya serikali ukizingatia watu waliotenda makosa ni viongozi waliowahi kushika nyadhifa kubwa ndani ya chama, serikalini na kwenye majeshi yetu.